Sasa inapotokea neva hizi za viungo vya pembezoni mwa mwili yani kwenye mikono na miguu kutofanya kazi ndipo mtu huanza kupata ganzi na wakati mwingine maumivu. Hapo unaweza kushika kitu na usijue kama umeshika kitu ama ukahisi maumivu wakati hakuna kitu kinachokuumiza
Nini Maana ya Peripherial Neuropathy?
Peripheral neophathy ni ugonjwa unaotokea pale neva za kwenye maeneo ya pembezoni mwa mwili hasa miguu na mikono kushindwa kufanya kazi kutokana na kupata majeraha. Kujeruhiwa kwa neva kunasababisha mwili kutumwa kwa taarifa ya maumivu wakati hakuna maumivu, au kutotuma taaria ya maumivu wakati kuna kitu kinachokuumiza. Neva hizi zinaweza kujeruhiwa kutokanana na- Ajali
- Kuumwa magonjwa
- Kupata maambukizi
- Au kurithi
Dalili za Tatizo la Ganzi kwenye Miguu na Mikono.
- Kutetemeka kwa mikono na miguu
- Kupata hisia kama umevaa kitu cha kubana kwenye mikono au miguu
- Kuangusha vitu mara kwa mara kutoka kwenye mikono
- Ngozi kuwa nyembamba
- Kushuka kwa shinikizo la damu
- Kupungua uweo wa tendo la ndoa hasa kwa wanaume
- Tumbo kujaa gesi na kukosa choo
- Kuharisha na
- Kutokwa na jasho jingi
Nini Kinachosababisha Ganzi kwenye Miguu na Mikono?
Magonjwa
Kisukari ni ugonjwa unaoongoza kwa kuathiri neva za fahamu na kisha kupelekea mwili kuwa na ganzi kwenye mikono au miguu. Kisukari husababisha kujeruhiwa kwa neva kutokana na kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu kutodhibitiwa. Magonjwa mengine yanayoweza kujeruhi neva za fahamu na hivo kupelekea ganzi miguuni na mikononi ni pamoja naMagonjwa ya figo ambapo figo zisipofanya kazi vizuri hupelekea kiwango kikubwa cha sumu kujikusanya mwilini na kuathiri neva
Kupungua uwezo wa tezi ya thyroid (hypothyroidsm) kunakopeleka mwili kuhifadhi maji kwenye eneo linalozunguka neva
Upungufu wa vitamin E, B-1, B-6 and B-12 ambazo ni vitamini muhimu katika kuimarisha afya ya neva.
Ajali
Ajali ni moja ya sababu kubwa inayopelekea kuathirika kwa neva. Ajali hizi ni pamoja na ajali za magari, kuanguka au kuvunjika kwa viungo.Pombe na Sumu
Pombe hupelekea kuchelewa kwa taarifa zinazosafirishwa na kuleta athari kwenye neva. Watumiaji wa pombe waliokithiri wapo kwenye hatari zaidi ya kuugua ganzi kwenye miguu na mikono.Watu wanaofanya kazi kwenye maeneo ya sumu na kemikali mfano sumu za kuulia wadudu,wanaweza kuugua tatizo hili la kupata ganzi ya mikono na miguu.
![Tokeo la picha la alcohol and peripheral neuropathy](https://www.healthline.com/hlcmsresource/images/imce/alcohol-related-neurologic-disease_thumb.jpg)
Maambukizi na Magonjwa ya Kinga
Baadhi ya bateria na virusi wanaweza kushambulia neva. Wagonjwa wa Ukimwi pamoja na wagonjwa wa tetekuwanga na mkanda wa jeshi wapo kwenye hatari ya kuugua tatizo hili la ganzi,Matumizi ya Dawa kwa muda mrefu
Matumizi ya baadhi ya dawa yanaweza kusababisha kuathirika kwa neva. Hii ni pamoja na- Dawa za kutibu kifafa
- Antibiotics
- Baadhi ya dawa kwa ajili ya presha na
- Dawa kwa ajili ya saratani
Nini cha kufanya kwa Mgonjwa wa ganzi
Moja ni kurekebisha tabia na mazingira yanayosababisha kama kisukari, ulevi na mazingira yenye kemikaliMazingira, tabia na Makundi yaliyopo kwenye Hatari zaidi kuugua Ganzi
- Kisukari
- Matumizi ya pombe kwa muda mrefu
- Kupungukiwa na Vitamin hasa Vitamin B
- Wagonjwa Ukimwi, mkanda wa jeshi na tetekuwanga
- Magonjwa ya kinga kushambulia tishu (autoimmune diseases)
- Kuwa na magonjwa ya figo, ini na tezi ya thyroid
- Familia zenye historia ya kuugua ganzi.
Fanya mazoezi ya viungo mara kwa mara. Weka ratiba ya kufanya mazoezi mara 4 kwa week nusu saa kwa siku.
Epuka mazingira yanayoweza kujeruhi neva kama . Kufanya kazi kwenye mazingira yenye kemikali kwa muda mrefu, kuvuta sigara na matumizi ya pombe kupita kiasi
No comments