JINSI YA KUFAHAMU DAWA SALAMA KUTUMIA KWA MJAMZITO



Madawa yanayotumika sana kipindi cha ujauzito ni yale yaliyo katika makundi haya. Yale ya kuzuia kutapiaka(antemetics), kuzuia uzalishaji tindikali(antacid), anthistamine, analegesics, antimicrobial, tranquilizers, hypnotic, diuretics, na madawa ya kulevya.

 

Shirika la dawa na chakula duniani FDA limeweka madawa katika makundi 5 kulingana na usalama wake kutumika kipindi cha ujauzito.Makundi haya ni A, B, C, D na X.

 

Tafiti chache za dawa zimefanyika kuonyesha usalama wa dawa kipindi cha ujauzito. Taarifa nyingi kuhusu usalama wa dawa kwa mama mjamzito zimefanyika kwa wanyama wengine, mara baada ya madawa haya kuonekana yapo salama basi huweza kutumiwa na wamama wajawazito na madhara yanapoonekana, taarifa hizo hutumika kama sehemu ya tafiti ya madhara ya dawa.

 

Wakati wa ujauzito dawa hutumika katika matibabu ya baadhi ya magonjwa au shida Fulan. Ingawa kuna wasiwasi wa usalama wa matumizi ya dawa kipindi cha ujauzito, madawa mengi yameripotiwa kusababisha madhaifu kwa mtoto kwa asilimia 2 hadi 3 ya madhaifu ya kiuumbaji yanayotokea kwa watoto bila kuhuisha pombe.

 

Si kwamba madawa yote yanaweza kupita kwenye kitovu cha mtoto na kuingia kwa mtoto wakati yupo ndani ya mama. Madawa yenye uwezo wa kupita na kuingia kwa mtoto huweza kusabaisha matatizo ya kiuumbaji wa mtoto. Madawa ambayo hayapiti pia huweza kumdhuru mtoto kwa kusinyaza kitovu na hivyo kuzuia uingiaji wa damu na chakula kwa mtoto akiwa tumboni kwa mama, pia huweza kusababisha kusinyaa kwa mfuko wa kizazi na kusababisha mtoto kukandamizwa na kukosa hewa, au kusababisha matatizo kwa mama kama shinikizo la chini la damu.

 

Madhara ya dawa kwa kichanga hutegemea umri wa kichanga tumboni, dozi ya dawa, ukali wa dawa. Daw zinazotumiwa kabla ya wiki 20 za ujauzito baada ya uchavushwaji huwa na madhara mengi au haina madhara kipindi cha ujauzito.

 

Madhara ya kiuumbaji yanaweza yasitokee kipindi hiki.Kipindi cha uumbaji wa viungo vya binadamu(Siku ya 14 hadi 56) dawa zilizo sumu zikitumika huweza kusababisha matatizo ya kiuumbaji kwa kichanga. Dawa zinazoingia kwa kichanga kipindi cha ujauzito zinaweza kusababisha mimba kutoka,madhara ya kimaumbile na anatomia, madhara ya uchakatuzi seli(huweza kutokea kabla, wakati au miaka mingi baada ya kuzaliwa)

 

Dawa zinazotumika mara baada ya uumbaji wa viungo vya binadamu yaani miezi mitatu ya pili na mitatu ya mwisho kipindi cha ujauzito huweza zisisababishe madhara au zinaweza kusababisha utendaji kazi mbaya wa organi zilizotengenezwa.

 


MAKUNDI YA DAWA KULINGANA NA USALAMA WAKE>



kundi A

Dawa hizi zimeonyesha hazina madhara kwa kichanga tumboni kutokana na tafiti zilizofanyika kwa binadamu

KUNDI B
Kwa tafiti za wanyama dawa zimeonyesha hazina madhara kwa kichanga, hakuna tafiti zilizofanyika kwa binadamu au tafiti kwa wanyama zimeonyesha madhara ila kwa binadamu hazijaonyesha madhara kwa kichanga

KUNDI C
Hakuna tafiti za kutosha zilizofanyika kwa binadamu au wanyama, au tafiti zimefanyika kwa wanyama na kuonyesha madhara lakini kwa binadamu hakuna tafiti zilizofanyika

KUNDI D
Ushahidi wa madhara kwa kichanga kwa binadamu upo lakini faida ya kutumia dawa inaweza kuwa kubwa kuliko madhara kwa mtoto endapo mfano(ugonjwa wa kufisha mama,ugonjwa mbaya amabapo dawa salama haziwezi kutibu ila ile isiyo salama inaweza)

KUNDI X
Imethibitishwa Madhara ni makubwa kwa mtoto kuliko faida zinazoweza kupatikana kwa matumizi ya dawa kipindi cha ujauzito.

Baadhi ya Madawa yanayojulikana au kushukiwa kuwa sumu kwa kichanga ni haya yafuatayo;

 

Dawa jamii ya ACE, Pombe, Aminopterin, Androgens, Carbamazepine, Coumarins, Danazol, Dethylstilbestrol, Etretine, Isotretinoin, lithium, Methimazole, Methotrexate, Phenytoin, radioactive Iodine, Tetracycline, Trimethadione, Valproate



VYEMA KUPATA USHAURI WA DAKTARI KABLA YA KUTUMIA DAWA YOTYOTE.

No comments