Picha ya mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 13
Tatizo
la kuota matiti kwa wanaume na watoto limekuwa kubwa sana katika dunia
ya leo. Inawezekana kabisa wakati unatembea njiani ukaona wanaume au
watoto wadogo wa kiume wakiwa na matiti makubwa ambapo watu wengi
huchukulia kama ni kawaida. Kitaalamu gynecomastia ni kukuwa kuliko
kawaida yake kwa tishu ya kwenye titi inayojulikana kama glandular
tissue. Tatizo hili huonekana sana kwa watoto wachanga na wanaume
waliokatika umri wa kubaleghe, lakini pia huonekana kwa watu wazima na
wazee.
Ukubwa wa tatizo (epidemiology)
Asilimia
60-90 ya watoto wachanga wanapata tatizo hili la kukuwa kwa matiti kwa
mpito linalojulikana kitaalamu kama transient gynecomastia kutokana na
kuwepo kwa kichocheo cha aina ya estrogen kwa wingi wakati wa ujauzito
wa mama.
Kati
ya asilimia 4-69 ya vijana walio katika umri wa kubaleghe imeonekana
wanapata tatizo hili kutokana na kuwepo kwa wingi kwa kimengenyo aina ya
estradiol.Mara nyingi huonekana katika umri kati ya miaka 10-12 na
hupotea taratibu ndani ya miezi 18, si kawaida yake kuonekana kwa vijana
walio na umri ya zaidi ya miaka 17. Asilimia 24-65 ya watu wazima
hupatwa na tatizo hili, hii hutokana na kubadilishwa kwa wingi kwa
kichocheo aina ya testerone kuwa estradiol na kutolewa kwa uchache kwa
kichocheo hiki cha testerone kutoka kwenye korodani zinazoanza
kuzeeka..Ikumbukwe ya kwamba kichocheo hiki testerone hutengenezwa
katika korodani za mwanamume.
Pathofiziolojia (Nini hutokea?)
Kuongezeka
ukubwa wa matiti kwa wanaume hutokana na kuharibika kwa mfumo wa
vichocheo unaojulikana kama estrogen-androgen balance na hivyo
kusababisha estrogen kutolewa kwa wingi ama kuongezeka kwa msisimko
(sensitivity) wa matiti kwa kiwango cha zaidi ya kawaida kwa kichocheo
aina ya estrogen kilicho kwenye mzunguko wa damu.Estrogen husababisha
chembechembe zinazojulikana kama ductal epithelia kuongezeka kwa wingi,
kurefuka (ductal elongation) na kugawanyika, kuongezeka kwa chembechembe
za mafuta (ductal fibroblasts) na kuongezeka kwa mfumo wa damu kwenye
matiti (increase vascularity).Estrogen hutengenezwa kutoka kwenye
vichocheo vya testerone na androgen kwa kutumia kimengenyo
kinachojulikana kama aromatase.
Aina za gynecomastia
•Puffy nipples – Kuongezeka ukubwa wa chuchu za matiti kutokana na kuongezeka kwa tishu aina ya glandular tissue.
•Pure
glandular gynecomastia – Huonekana sana kwa wale wanaofanya mazoezi ya
kujenga mwili (bodybuilders), kutokana na matumizi ya dawa za kujenga
mwili (anabolic steroids) ambazo zinakuwa na kiwango kikubwa cha
kichocheo aina ya testerone, ambacho hubadilishwa kuwa estrogen. Kwa
wanaume wembamba, tatizo hili hutokea kutokana na kuongezeka kwa breast
tissue gland pamoja na kuwepo/kutokuwepo kwa tishu aina ya adipose
tissue.
Ni nani aliyekatika hatari ya kupata tatizo hili?
•Wanaume walio na umri zaidi ya miaka 50.
•Wenye uzito uliopitiliza (Obesity)
•Unywaji pombe kupindukia
•Magonjwa sugu ya figo au ya Ini
•Kuwepo kwa historia ya tatizo hili katika familia.
Visababishi vya kukuwa kwa matiti kwa wanaume
•Pseudogynecomastia
– Kuongezeka kwa tishu zinazozunguka chuchu za matiti na huambatana na
kuwepo kwa wingi wa tishu aina ya adipose. Mazoezi na kula vyakula venye
virutubisho sahihi huondosha tatizo hili.
•Unilateral/asymetrical
gynecomastia – Ni kuongezeka kwa titi moja pekee au la upande mmoja wa
mwili wa mwanamume kutokana na sababu mbalimbali. Titi la upande wa pili
huwa kwenye umbile na saizi ya kawaida. Bilateral gynecomastia ni
kuongezeka kwa matiti yote mawili.
•Hypogonadism
– Kutofanya kazi kwa korodani vizuri na kuwa ndogo. Hii husababishwa na
magonjwa mbalimbali kama klinifelter'rs syndrome, pitituary insuffiency
na nk.
•Umri
– Kuzeeka pia kumehusishwa kutokea kwa tatizo hili kutokana na kutolewa
kwa uchache kwa kichocheo cha testerone na kuongezeka kwa juhudi za
kutengeneza kwa wingi kwa kimengenyo aina ya estradiol kutoka kwenye
kichocheo aina ya testerone. Pia mabadiliko ya mfumo mzima wa vichocheo
mwilini hasa kwa wale wenye uzito uliopitiliza.
•Uzito
uliopitiliza (Obesity) – Watu wenye uzito uliopitiliza hupatwa na
tatizo hili kutokana na kuharibika kwa mfumo wa vichocheo mwilini na
hivyo kuongezeka kwa kichocheo aina ya estrogen mwilini mwao na wakati
huohuo kupungua kwa kichocheo kingine aina ya testerone.
•Saratani
– Baadhi ya saratani kama saratani ya kwenye korodani, kwenye tezi
lililojuu ya figo (adrenal gland), saratani ya tezi la kichwa (pitituary
tumor), huharibu mfumo mzima wa vichocheo mwilini hasa wa kuweka sawa
vichocheo kati ya uanaume na uanawake (male-female hormonal balance).
•Hyperthyroidism – Kukuwa kwa ukubwa wa tezi la koo (thyroid gland) na hivyo kutengeneza kwa wingi kichocheo aina ya thyroxine.
•
Tatizo la figo kushindwa kufanya kazi (Renal/Kidney failure) - Nusu ya
wagonjwa wote wanaotibiwa tatizo la figo kushindwa kufanya kazi kwa
kutumia hemodialysis hupatwa na tatizo hili la kukuwa kwa matiti
kutokana na kuharibika kwa mfumo wa vichocheo mwilini (hormonal
imbalance).
•Matatizo
ya Ini – Dawa za kutibu magonjwa ya kwenye Ini kama liver cirrhosis,
liver failure husababisha kutokea kwa tatizo hili kutokana na kukosekana
kwa uwiano sawa wa mfumo wa vichocheo mwilini.
•Utapia
mlo, ukame – Utapia mlo, ukame au kujikondesha husababisha kupungua kwa
kichocheo aina ya testerone na kuongezeka kwa kichocheo aina ya
estrogen na hivyo kuharibu mfumo wa vichocheo mwilini. Hii hutokana na
kukosekana
kwa virutubisho sahihi mwilini ambavyo vingi husaidia kurekebisha mfumo
wa vichocheo mwilini na hivyo kumuepusha mtu na magonjwa mbalimbali
pamoja na tatizo hili.
•Madhara ya dawa za kurefusha maisha (Antiretroviral therapy) kwa wagonjwa wa ukimwi.
•Utumiaji wa madawa ya kulevya kama bangi/marijuana.
Vipimo vya Uchunguzi
Vipimo hivi vitafanywa kulingana na historia ya mgonjwa, dalili na viashiria vya mgonjwa baada ya kupimwa na daktari.
•Kipimo
cha damu (Complete Blood Count) – Kuangalia wingi wake, aina mbalimbali
za chembechembe za damu na uwepo wa maambukizi ya bakteria.
•X-ray
ya matiti (Mammogram) – Hutumiwa kuangalia tishu za kawaida na zile
ambazo si za kawaida zilizo kwenye matiti. Husaidia kugundua uwepo wa
saratani, cysts, na calcifications kwenye matiti.
•Liver
function test – Mjumuiko wa vipimo vya damu kuangalia aina mbalimbali
za vichocheo na vimengenyo ili kuweza kutambua kama mgonjwa ana ugonjwa
wowote ule wa Ini na chanzo chake, vipimo hivi huangalia albumin,
Alanine transaminase (ALT), Aspartate transaminase (AST), Alkaline
phosphatase (ALK), Total bilirubin (TBIL), Direct bilirubin (Conjugated
Bilirubin), Gamma Glutamyl Transpeptidase (GGT), Lactate Dihydrogenase
(LDH).
•Tumor markers – Kipimo cha damu cha kuangalia viashiria vya saratani ya korodani kama AFP alpha feto 1 protein, Beta-HCG, LDH.
•Kipimo
cha damu cha kuangalia wingi wa kichocheo cha aina ya testerone (Total
and Free Testerone) Hufanyika asubuhi ambapo kiwango cha testerone huwa
juu. Kiwango cha kawaida cha kichocheo cha testerone ni 300 - 1000 ng/dl
(Kiwango hiki hupungua kwa asilimia 13 wakati wa mchana).
•Kipimo
cha damu cha kuangalia vichocheo vinavyoonekana kwenye ugonjwa wa kukua
ukubwa wa tezi la koo ( hyperthyroidism) kama kichocheo aina ya Thyroid
Stimulating Hormone (TSH) ambacho huwa katika kiwango kidogo
wakati
wa kuugua ugonjwa wa hyperthyroidism, hutolewa na tezi la kwenye kichwa
aina ya pitituary gland, vichocheo vyengine aina ya anti-TSH receptor
antibodies (kwa wenye ugonjwa wa Grave’s disease), anti-thyroid –
peroxidase
(kwa
wenye ugonjwa wa Hashimoto’s disease), na pia kuangalia wingi wa
vichocheo aina ya T3 na T4. Kipimo cha Thyroid Scintigraphy pia huweza
kutumiwa kutofautisha kati ya ugonjwa wa hyperthyroidism na ugonjwa wa
thyroiditis. Kipimo hiki hutumia madini ya mionzi ya iodine (Iodine-131
ama Iodine-123).
•Vipimo vya kuangalia kama figo zimeshindwa kufanya kazi vizuri kama;
a)Kipimo
cha utendaji kazi wa figo (Renal function tests) ambacho husaidia
kuchunguza kiwango cha urea (blood urea nitrogen (BUN) katika damu.
Aidha husaidia pia kuchunguza ongezeko la kiwango cha creatinine katika
damu.
b)Uchunguzi wa kiwango cha madini mbalimbali katika damu (blood electrolytes)
c)Kupima kiasi cha mkojo kinachotolewa na mgonjwa katika masaa 24
d)Uchunguzi wa mkojo (Urine analysis): Rangi ya mkojo, kiasi cha electrolytes, uwepo wa usaha au damu au casts.
e)Ultrasound ya figo na kibofu cha mkojo
f)Renal biopsy.
Tiba ya Gynecomastia
Kama
nilivyosema hapo awali, tatizo hili kwa vijana waliokatika umri mdogo
au wa kubaleghe hupotea lenyewe taratibu ndani ya miezi 18. Kwa mzazi
unatakiwa usihofu, lakini kama litaonekana kwa mtoto zaidi ya miaka 17,
basi hapa mzazi unatakiwa kuchukua hatua za haraka ambazo ni kumuona
daktari ili aweze kukusaidia kwa ufasaha zaidi.
1.Tiba ya madawa
•Tiba
ya kutumia vichocheo (Testerone Replacement Therapy) – Kichocheo aina
ya testerone hutolewa kwa mgonjwa kwa njia ya mdomoni, kwenye dripu, au
kipachiko (patch forms). Hii hutolewa kwa wagonjwa ambao hawawezi
kutoa
testerone kutoka kwenye korodani zao kutokana na kupata ajali, ugonjwa
au wale ambao hawana korodani kutokana na sababu mbalimbali.
•Dawa
aina ya Selective Estrogen Receptor Modulator (SERMs) kama Tamoxifen,
raloxifen, husaidia kupunguza ukubwa (volume) wa matiti lakini haziondoi
tishu zote kwa ujumla. Aina hii ya tiba hutumiwa kwa wale wenye
tatizo
sugu la gynecomastia au wale wenye kupata maumivu makali sana. Dawa
hizi zina madhara na hivyo ni vizuri kutumia kwa maelekezo ya daktari.
•Dawa
aina ya Aromatase Inhibitors kama anastrozole, hufanya kazi kwa kuzuia
kimengenyo aina ya aromatase na hivyo kuzuia utengenezwaji wa kichocheo
aina ya estrogen. Tafiti nyingi zilizofanywa zimeshindwa kutoa majibu
ya
uhakika juu ya matumizi ya dawa hizi katika kutibu tatizo hili la kukuwa kwa matiti kwa wanaume.
2.Tiba
ya Upasuaji – Kwa wale wenye tatizo hili sugu, upasuaji wa kurekebisha
matiti unaweza kufanyika. Hii humuongezea mwanamume hali ya kujiamini na
hivyo kuwa katika hali nzuri kisaikolojia, na huongeza ufanisi wa
maisha yake ya kila siku.
3.Kupunguza uzito kwa kufanya mazoezi mara kwa mara na kula mlo wenye virutubisho vyote muhimu.
4.Kutibu chanzo au magonjwa mbalimbali kama hyperthyroidism, ugonjwa wa figo kushindwa kufanya kazi, saratani mbalimbali na nk.
5.Kuacha kunywa pombe na matumizi ya madawa ya kulevya kama bangi/marijuana.
6.Daktari
kumbadilishia mgonjwa dawa baada ya kuona dalili za tatizo hili kwa
wale wenye kutumia dawa za kutibu ugonjwa wa Ini, dawa za kurefusha
maisha. Kwa wagonjwa wa Ukimwi, ni vizuri kwa daktari kabla ya kumpa
mgonjwa
dawa, kumfanyia mgonjwa kipimo cha fasting lipid profile, ili uweze
kutambua kama dawa unazotaka kumpa zitamletea madhara au la. Na
inashauriwa
kurudia kipimo hiki kati ya miezi 3 hadi 6 baada ya kuanza dawa hizi za
kurefusha maisha au baada ya kumbadilishia mgonjwa dawa. Hata hivyo sio
dawa zote za kurefusha maisha zilizo na madhara haya, kwani zipo
nyingine zinazopunguza kiwango cha mafuta mwilini na kwenye tishu.
Madhara ya Gynecomastia
1.Uwepo
wa tatizo hili kwa muda wa zaidi ya miezi 12 au mwaka mmoja,
husababisha matiti kutengeneza makovu au kwa kitaalamu scarring/fibrosis
na hivyo kufanya tiba kwa kutumia dawa kuwa ngumu sana.
2.Wanaume
wenye tatizo hili wapo kwenye hatari zaidi ya mara tano ya kupata
saratani ya matiti ikilinganishwa na wanaume ambao hawana tatizo hili.
3.Kuathirika
kisaikolojia (kuona aibu, kutojiamini, kujihisi tofauti na wanaume
wenzake). Hali hii inaweza hata kumfanya mtu kuishi maisha ya huzuni au
kushindwa kujumuika na watu katika shughuli mbalimbali kama michezo na
nk
No comments