Suala la kupunguza tumbo ama uzito mara
baada ya kupata operesheni ya uzazi, limekuwa ni changamoto miongoni mwa
wanawake wengi.
Wengi wamekuwa wakishindwa kurudisha maumbo
yao ya awali mara watokapo kujifungua. Hii inatokana si tu kushindwa kupangilio
milo yao kwa kuchagua vyakula vyenye afya, bali pia na kushindwa kufanya
mazoezi kwa ajili ya kujenga miili yao.
Kama ilivyo kwa wazazi wengine huwa na uchu
wa kurudisha miili yao haraka iwezekanavyo, na muda mwingine kupangilia vyakula
maalumu vyenye afya vitakavyokuongoza kufikia malengo yako hakikisha unakuwa na
programu maalumu ya mazoezi salama itakayokurahisishia zaidi lengo lako hilo.
Kabla ya kuanza mpango wako huo wa
kuboresha umbo lako, kumbuka kwamba mwili wako umetoka katika utaratibu
mwingine wa kumleta kiumbe duniani tena kwa njia ya upasuaji. Hivyo suala la
kupungua kwako au kurudi kwako katika hali ya kawaida linatakiwa liende
taratibu ili kutoathiri afya yako. Kamwe usijifananishe na yule aliyejifungua
kwa njia ya kawaida.
Kama umetoka katika operesheni ya uzazi, ni
wazi kuwa utakuwa na kovu. Ni muhimu sana kukinga kovu hilo na kulipa muda
lipone taratibu.
Ni vyema ungeanza mpango wa kupunguza uzito
ama tumbo lako mara baada ya kupata ushauri wa daktari. Yeye ndiye mwenye
mamlaka ya kukuruhusu kuanza, hasa baada ya kurudhika na maendeleo ya afya
yako.
Madaktari wengi wamekuwa wakiwashauri
wanawake kusubiri hadi wiki sita hadi nane kabla ya kuanza mazoezi rahisi
yatakayokuwa na lengo la kupunguza uzito yakiambatana na ale ya kupunguza
tumbo.
Kukinga kovu lako
Ni kweli kabisa wanawake wengi wamekuwa
wakipenda kuvaa suruali maalumu ili kuficha kovu katika tumbo, lakini pia
wengine hufanya hivyo wakilenga kuficha hata tumbo lenyewe ambalo limetokea
kukua visivyo kawaida baada ya operesheni. Hii ni sawa. Lakini pia unashauriwa
kupata ushauri wa daktari kabla ya kuamua kuvaa hivyo.
Mazoezi
Ikiwa wewe ni mmoja kati ya wanawake
waliofanyiwa operesheni na unazingatia kula vyakula bora na kufanya mazoezi
sahihi tayari utakuwa uko kwenye njia sahihi ya siyo tu kupunguza uzito wa
mwili, bali pia ukubwa wa tumbo lako.
Mazoezi ya viungo kama vile kukimbia,
kuogelea, kutembea hata kuendesha baiskeli yatakusaidia kuunguza mafuta na pia
kupunguza uzito.
Unaweza pia kuanza kufanya mazoezi madogo
madogo ya tumbo kwa kulala na kunyoosha na kukunja misuli yako ya tumbo. Misuli
yako itakapokuwa imejengeka unaweza kuanza mazoezi ya ‘sit-ups’
Ikiwa utaamua kufanya mazoezi kwenye darasa
maalumu au hata gym hakikisha unamweleza mwalimu wako kuwa umefanyiwa
operesheni hivyo itakuwa rahisi kwake kukupa mazoezi yanayoendana na hali yako.
Kwa upande wa chakula, kila mara unatakiwa
kuwa karibu na daktari wako ili uende katika mstari sahihi katika huo ulaji
wako. Yeye anaweza akakushauri ni chakula gani ule na kipi uache.
Mazoezi yafanye kwa muda gani
Kutokana na utofauti tulionao mara nyingi
kila mmoja inamchukua muda wake kupunguza ukubwa wa tumbo ama uzito wa mwili
wake.
Mwanamke aliyewahi kuzaa mara nyingi
anahitaji kazi ya ziada ukilinganisha na yule anayezaa kwa mara ya kwanza. Pia
wanawake wembamba wana uwezo wa kufanya vizuri zaidi kuliko wale wanene.
Si vyema kujilinganisha na mtu katika
mpangilio wako huu wa mazoezi, kwani wakati mwingine unaweza ukajilinganisha na
mtu ambaye si sahihi kwako.
Unachotakiwa kufanya ni kuelekeza nguvu
zako katika kufanikisha lengo lako.
Ni mud a gani Mama aliejifungua kwa operation kupata mimba salama
ReplyDeleteNi mud a gani Mama aliejifungua kwa operation kupata mimba salama
ReplyDeleteJe waweza kufungua tumbo kama umejifungua Kwa upasuaji
ReplyDeleteJe waweza kufunga tumbo kama umejifungua Kwa upasuaji
ReplyDelete