KUKAUKIWA NA MATE MDOMONI (xerostomia)


Hii ni hali ya kukauka kwa  mate kinywani na kufanya kinywa kuwa kikavu isivyo kawaida. Hii hutokana na kupungua  kwa uzalishaji wa mate katika tezi mbalimbali kinywani.Hali hii imekuwa ikitokea sana kwa wazee ukilinganisha na watu wengine.Hali hii inaweza kusababishwa na vitu mbalimbali kama;
  • utumiaji wa mionzi ya x-ray kwenye matibabu ya saratani mbalimbali(radiotherapy) zinazotokea kwenye maeneo ya kichwa na shingo ambapo tezi za mate zinaweza kudhurika.
  • matatizo ya saikolijia kama vile sonona.
  • Uvutaji wa sigara
  • Magonjwa kama UKIMWI,kisukari (poorly controlled diabetes)
  • upungufu wa maji mwilini,
  • matumizi ya madawa ambayo hutumika kutibu magonjwa mbalimbali (mf.antihistamines,decongestants,antihypertensives and antidepressants)

dalili zake zikoje


  • Kuchanika na kuvimba kwa mdomo(splitting and cracking of lips)
  • Kuwa na harufu mbaya mdomoni
  • Kushindwa kutafuna pia kumeza chakula hasa vyakula vikavu
  • Kukosa ladha ya chakula
  • Kuchanika na maumivu kwenye ulimi,mashavu kwa ndani na pembeni ya midomo
  • Kuongezeka kwa matatizo ya fizi na kutoboka kwa meno
  • Kushindwa kuongea vizuri kutokana na kinywa kuwa kikavu
  • Kuongezeka kwa hamu ya kunywa maji hususani usiku.
  • Maambukizi ya fangasi za mdomo

matibabu yake ni yapi?

Matibabu ya kinywa kuwa kikavu isivyo kawaida yamejikita hasa katika dalili zinazoonyeshwa na hali hii. Kuongeza uzalishaji wa mate katika kinywa kama vile kunywa maji mengi,kupunguza dozi ya dawa au kubadilisha kama inawezekana,kutumia dawa ya kuongeza uzalishaji wa mate kwa mfano pilocarpine(sialagogues),kuwa na kinywa kisafi

No comments