KUWA NA VIPINDI VINGI VYA HEDHI NA KUWA NA VIPINDI VICHACHE KWENYE HEDHI
POLYMENORRHEA & OLIGOMENORRHEA
Kwa
kawaida mzunguko wa hedhi huchukua siku 21 mpaka 35 lakini wastani wa
wanawake wengi huenda siku 28 kama inavyotumiwa katika vitabu vingi.
Kama
mwanamke anaenda mzunguko wa siku 21 basi katika mwaka wenye siku 365
ataenda mizunguko 17 (365/21=17) na yule mwenye mzunguko wa siku 35
atakuwa na vipindi 10 vya hedhi( 365/35=10) katika mwaka
Nini husababisha kuona vipindi vingi katika mwezi(polymenorrhea)?
Kuna
sababu mbalimbali, zipo sababu za kawaida zisizo za hatari kama msongo
wa mawazo, mazoezi makali, matumizi ya dawa mbalimbali na matatizo ya
mwanamke akiwa anaanza kuacha kuona siku zake. Sababu zingine ni
matatizo/magonjwa kwenye mfumo wa uzazi. Baadhi ya sababu hizo
zimeelezewa hapo chini.
-
Kuharibika/kutokuwepo kwa uwiano wa vichochezi mwili
Hili
linaweza kusababishwa na mambo mbalimbali kama vile chakula unachokula
endapo hakina virutubisho vya kutosha, kubadili chakula, kubadili mfumo
wa maisha ya kila siku na kubadili ratiba ya kulala kila siku.
Tatizo
hili huweza kuwa kubwa na kusababisha mwanamke kuongezeka uzito
kubadilika tabia na hulka yake kuhalibika, ni vema kupata ushauri na
msaada wa kiafya endapo hili litatokea.
-
Kujipandikiza nje ya kizazi kwa chembe za ukuta wa ndani ya mfuko wa kizazi(endometriosis)
Chembe
za ndani ya uzazi huweza kujipandikiza katika mayai, nje ya misuli ya
mfuko wa kizazi, kwenye mirija ya kupitisha mayai n.k. kuwepo kwa chembe
hizi nje ya kizazi husababisha kuvuja kwa damu ya hedhi ndani na
madhara yake ni michomo na kushikamana kwa organi ndani ya nyonga.
Mwanamke anapata dalili za maumivu makali wakati wa hedhi pamoja kuwa
na vipindi vingi vya hedhi katika mwaka.
-
Vimbe kwenye ukuta wa uzazi(uterine Fibroids)
Kuwepo
kwa vimbe ndani ya ukuta wa kizazi huufanya ukuta unaotengenezwa kila
mwezi (kwa ajili ya kupokea yai endapo limechavunshwa)kutokuwa imara na
hivo husababisha ukuta huu kuvunjika kabla ya mzunguko kukamilika na
mwanamke anakuwa na vipindi vingi vya hedhi.
-
Kuanza kukoma kwa Mzunguko wa Hedhi (perimenopause)
Kukoma
kwa mzunguko wa Hedhi ni jambo la kawaida kwa mwanamke anapofikia umri
zaidi ya miaka 45. Dalili zake ni kama kutokwa na jasho wakati wa usiku,
kubadilika kwa tabia au hulka ya mtu na kuwa na vipindi vingi vya hedhi
katika mwezi. matatizo haya huletwa kutokana na mabadiliko ya
vichochezi mwili(hormone) yanayotokea kwa mwanamke anapokuwa anazeeka.
-
Magonjwa ya zinaa
Ni yapi matibabu ya tatizo hili?
Tatizo
la kuwa na vipindi vingi vya hedhi huweza kutibiwa endapo sababu
imejulikana ni nini, kama tatizo ni msongo wa mawazo, dawa za mpango wa
uzazi,mazoezi makali, uzito na mengine, matibabu yake ni kukabiliana na
mambo hayo. Na endapo utaenda hospitali basi utapimwa vipimo mbalimbali
na kutibiwa tatizo lako.
Kumbuka ni vema kwena hospitali kwa mtaalamu wa afya ili kupata ushauri na matibabu ya tatizo lako.
Endapo unasumbuliw na tatizo hili waweza kuwasiliana nasi kupitia barua pepe na namba za simu hapo chin
No comments