UTE UNAOASHIRIA SIKU ZA HATARI YA KUPATA MIMBA

 

Hormone zinazochochea  mayai kutengenezwa ndo hizo hizo zinachochea kutengenezwa,kwa ute unaosaidia mbegu za kiume zijongee vizuri.
Hormone ya estrogen ndo inahusika na hili. Endapo una estrogen kidogo huwez pata ute au kama mfumo wa estrogen na progesterone haujakaa katika uwiano mzuri huwezi pata ute.

Ute unaovutika huanza kutokea siku chache kabla ya yai kuachiliwa. Japo wengine wenye tatizo la Polycystic ovarian syndrome wanakua wanapata ute huu zaidi ya mara moja katika mizunguko yao.

Ute huu unapozalishwa unaambata na joto kupanda. Kama unapata ute na joto hakuna mabadiliko bas inaweza kua yafatayo
1.haupevushi mayai
2.hau chart vizuri


JINSI YA KUANGALIA UTE
1.nawa mikono
2.weka kidole cha kati ukeni ndani. Kama unatoa ute mwingi basi haina haja ya kuingia ndani
3.toa kidole na kuangalia ute ukoje

AINA ZA UTE

1.MKAVU /DRY PHASE
Uke siku zote hauwi mkavu kabisa,Unapokuwa katika kipindi hiki unakua tu na majimaji kiasi na hayavutiki wala kunata.
Ute huu uanza kutokea ndani ya Siku 1  hadi 3 tokea umalize period.



2.STICKY
Siku ya nne hadi 6 baada ya kumaliza hedhi unaanza kutengeneza ute unaokua unanata kama gundi fulani. Ute huu unapokuwepo hauwezi kupata mimba kwani unaathiri kujongea vizuri kwa mbegu za kiume.



3.CREAMY
Ndani ya siku ya 7 hadi 9 Unaanza kutengeneza ute ambao unakua mithili ya lotion na haunati.
Kipindi hiki ndio mwili unakua unajiandaa kuingia katika hali ya hatari.kwa watu wanotafuta watoto basi anaweza kuanza kushiriki tendo la ndoa kwa ajili ya kutafuta mtoto.




4.EGGY WHITE
Kuanzia siku ya 10 hadi 15 hapa ukeni unakuwa na ute unaovutika uko mithili ya ute wa yai Bichi.Unapopata ute  huu ni dalili  kwamba upo katika siku za hatari na yai limepevuka.



Baada ya siku za hatari unarudia tena kupata ute ulio kama lotion(creamy) hadi utapofikia hedhi ya mwezi unaofatia.


No comments