HATUA ZA UKUAJI NA MAENDELEO YA MTOTO

Jinsi ya kutumia chati hizi za maendeleo ya mtoto

Watoto hukua katika nyanja kuu zifuatazo: kimwili, kiakili, kimawasiliano (kutoa ishara au kuongea), na kijamii (kuhusiana na watu wengine). Baadhi ya stadi ambazo mtoto hujifunza hujumuisha nyanja zote hizi. Kwa mfano, mtoto anapotoa mikono wake kwa mtu mwingine, anakuwa anatumia:
  • stadi ya kimwili – kuinua mikono yake.
  • stadi ya kiakili – anakutambua.
  • stadi ya mawasiliano – anakuambia kile anachotaka.
  • stadi ya kijamii – anafurahia kubebwa na wewe.


Chati zifuatazo zinaonesha baadhi ya stadi ambazo watoto hujifunza na lini hujifunza. Unaweza kutumia chati hizi kupata taarifa za jumla kuhusu jinsi gani watoto huendelea kutoka hatua moja hadi nyingine na kukusaidia kuamua stadi gani ambazo mtoto anahitaji kujifunza.
miezi
6
miezi
12
miaka 2
Chati zinaonesha jinsi stadi za watoto za kimwili hubadilika kadri wanavyokua.

Kukusaidia kuamua stadi gani ambazo watoto wanahitaji kujifunza

Chagua chati ambayo inakaribia sana umri wa mtoto. Kwenye chati, chora na kuzugushia mdwara stadi ambazo mtoto wako alizonazo. Unaweza kugundua kuwa mwanao hana baadhi ya stadi ambazo watoto wengine wenye umri kama wake wanazo. Kulijua hili kunaweza kukusaida kuamua mazoezi gani ambayo unataka kumshirikisha mtoto.


Miaka
2
Stadi za mawasiliano
Stadi za kiakili
Stadi za kijamii
Stadi za kimwili
hutumia maneno 2 na sentensi zenye maneno 3
Cheza mpira
Baba
Baba
hutumia maneno mepesi
huiga neno mojamoja au ishara
kikombe
hulinganisha vitu mbalimbali
hutumia vitu mbalimbali vinavyohusiana
hujishughulisha kwa makini na jambo fulani kwa muda mrefu
hucheza pembeni na watoto wengine
humuiga mtoa huduma/mlezi
hutoa rai kwa wengine anapohitaji msaada
hupanga pamoja vitu vikubwa vikubwa
hutembea
huchotama
Katika chati iliyooneshwa juu,mama amezungushia midwara stadi ambazo mtoto wake wa miez 20 anaweza kuzifanya. Mtoto wake anahitaji shughuli za kumsaidia kupata stadi za kimwili na mawasiliano.




Kila sehemu ya mdwara huu inaonesha nyanja tofauti ya maendeleo. Picha na maneno ni mifano ya stadi ambazo watoto wengi wanakuwa nazo wanapofikisha miezi 3.

Miezi
3
Stadi za mawasiliano
Stadi za kiakili
Stadi za kijamii
Stadi za kimwili


huonyesha hisia kwa sauti au nyuso alizozizoea
huonyesha hisia kwa sauti au matendo ya ghafla
huwatambua wanaomhudumia
hulia anapokuwa na njaa au kutojisikia vizuri
huweza kutulizwa kwa sauti au mguso/kupapaswa
hutabasamu anaposhirikishwa kwenye mchezo
anatambua mikono
hunyonya ziwa
huinua kichwa juu akiwa amelalia tumbo lake
Watoto ambao hawawezi kutenda stadi 2 katika sehemu mojawapo kwenye mduara watanufaika kutokana na shughuli ambazo huwasidia watoto kuendelea katika nyanja hiyo. Lakini picha hizi ni mifano tu ya stadi. Kwa mfano, katika sehemu ya mawasiliano kwenye mduara: siyo lazima upulize zumari! Swali la kujiuliza ni iwapo mtoto wako huitikia sauti ya ghafla(isiyo ya kawaida).
Usisahau kwamba mtoto atajifunza vizuri zaidi kwa kufanya shughuli ambazo watoto wengine wa umri wake hufanya katika jamii yako.




Kila sehemu ya mdwara huu inaonesha nyanja tofauti ya maendeleo. Picha na maneno ni mifano ya stadi ambazo watoto wanakuwa nazo wanapokuwa na umri wa miezi 6.

Miezi
6
Stadi za mawasiliano
Stadi za kiakili
Stadi za kijamii
Stadi za kimwili
hutoa sauti na tendo rahisi kuonesha hisia
aaah
hugeuza kichwa kuelekea sauti au tendo
huokota vitu na kuviweka mdomoni
hucheza na vidude vya kuchezea kwa njia mbalimbali
huvutiwa na vitu
huonesha woga mbele ya watu wapya kwake
huonesha rai kutaka uangalizi au huduma
hutambua watu kadhaa
hujiviringisha kutoka tumboni hadi mgongoni na kutoka mgongoni kurudi kulalia tumbo
huweza kukaa kwa msaada
huchezesha na kurusha mikono na miguu
Watoto ambao hawawezi kufanya stadi 2 kutoka sehemu mojawapo ya mdwara watanufaika na shughuli za kumsaidia mtoto kuendelea katika Nyanja hiyo. Lakini picha hizi ni mifano tu ya stadi. Kwa mfano, katika sehemu ya stadi za kimwili kwenye mdwara: mtoto wako siyo lazima achezee kinya’nga. Swali la kujiuliza ni iwapo mto wako huchezesha na kurusha viungo vyake.
Kumbuka kwamba mtoto atajifunza vizuri zaidi kwa kufanya shughuli amnbazo watoto wengine wenye umri kama wake wanazofanya katika jamii hiyo.


Kila sehemu ya mdwara huonyesha nyanja tofauti ya maendeleo. Picha na maneno ni mifano tu ya stadi ambazo watoto wanakuwa nazo wanapokuwa na umri wa miezi 12.


Miezi
12
Stadi za mawasiliano
Stadi za kiakili
Stadi za kijamii
Stadi za kimwili


huelewa maneno na ishara nyepesi
Nipatie mimi
huanza kutamka majina ya vitu
huunganisha sauti
ba-ba
ga-ga
wa wa
hujifunza kwamba vitu vipo hata kama havioni kwa macho
hujibidisha kutatua matatizo mepesi
huanza kuelewa sababu (chanzo) na matokeo yake
hutumia matendo au ishara kuonesha hisia
hulia mhudumu wake anapoondoka
huanza kufurahia kucheza na watu wengine
hukaa mwenyewe bila msaada
hutambaa
hujivuta na kusimama mwenyewe

Watoto wadogo ambao hawawezi kutenda stadi 2 kutoka mojawapo ya sehemu kwenye mduara watanufaika kutokana na shughuli ambazo husaidia watoto kuendelea katika nyanja hiyo. Lakini picha hizi ni mifano tu ya stadi. Kwa mfano, katika nyanja ya stadi za kijamii: hulazimiki kucheza na mtoto wako. Swali la kujiuliza ni iwapo mtoto wako anafurahia kucheza na wengine.
Kumbuka kuwa mtoto atajifunza vizuri kwa kufanya shughuli ambazo watoto wengine wenye umri wake katika jamii yake wanafanya.




Kila sehemu ya mduara huu inaonesha nyanja tofauti ya maendeleo. Picha na maneno ni mifano ya stadi ambazo watoto wengi wanakuwa nazo wanapokuwa na umri wa miaka 2.

Miaka
2
Stadi za mawasiliano
Stadi za kiakili
Stadi za kijamii
Stadi za kimwili
hutumia maneno 2 na sentensi zenye maneno 3
Cheza mpira
Baba
Baba
hutumia maneno mepesi
huiga neno mojamoja au ishara
kikombe
hulinganisha vitu mbalimbali
hutumia vitu mbalimbali vinavyohusiana
hujishughulisha kwa makini na jambo fulani kwa muda mrefu
hucheza pembeni na watoto wengine
humuiga mtoa huduma/mlezi
hutoa rai kwa wengine anapohitaji msaada
hupanga pamoja vitu vikubwa vikubwa
hutembea
huchotama
Watoto ambao hawawezi kutenda stadi 2 kutoka mojawapo ya sehemu kwenye mduara watanufaika kutokana na shughuli ambazo husaidia watoto kuendelea katika nyanja hiyo. Lakini picha ni mifano tu. Kwa mfano, katika sehemu ya stadi za kiakili katika mduara: mtoto wako halazimiki kupiga ngoma. Swali ni iwapo mtoto wako anaweza kutumia vitu 2 kwa mpigo.
Kumbuka kuwa mtoto atajifunza vizuri kwa kufanya shughuli ambazo watoto wengine wenye umri wake katika jamii yake wanafanya.




Kila sehemu ya mduara huu inaonesha nyanja tofauti za maendeleo. Picha na maneno ni mifano ya stadi ambazo watoto wengi wanakuwa nazo wanapokuwa na umri wa miaka 3.

Miaka
3
Stadi za mawasiliano
Stadi za kiakili
Stadi za kijamii
Stadi za kimwili
Onesha mdomo wako?
huwasiliana kwa kueleweka
Nataka kwenda na Baba
huelewa sehemu kubwa ya lugha nyepesi


huchomeka vipande vya vitu kwenye mashimo au nafasi zinazoendana
huchambua vitu
hutenganisha vitu na baadaye kuviunganisha pamoja
hupenda kusifiwa baada ya kufanya kazi nyepesi
Ahsante kwa kusaidia
hufurahia kusaidia na kazi za nyumbani
anatambua hisia za watu
hukimbia, huruka na hupanda
hutumia mikono yake kwa kazi zisizo rahisi
hurusha mpira
Watoto wadogo ambao hawawezi kutenda stadi 2 kutoka sehemu mojawapo sehemu kwenye mduara watanufaika kutokana na shughuli ambazo husaidia watoto kuendelea katika nyanja hiyo. Lakini picha hizi ni mifano tu ya stadi. Kwa mfano, katika nyanja ya stadi za kijamii: mtoto wako halazimiki kufagia. Swali la kujiuliza ni iwapo mtoto wako anafurahia kusaidia na kazi za nyumbani.
Kumbuka kuwa mtoto atajifunza vizuri kwa kufanya shughuli ambazo watoto wengine wenye umri wake katika jamii yake wanafanya.




Kila sehemu ya mduara huu inaonesha nyanja tofauti ya maendeleo. Picha na maneno ni mifano ya stadi ambazo watoto wengi wanakuwa nazo wanapokuwa na umri wa miaka 5.

Miaka
5
Stadi za mawasiliano
Stadi za kiakili
Stadi za kijamii
Stadi za kimwili
Nilianguka kwenye maji.
huuliza maswali mengi
Nani wapo kule? Wanafanya nini ?
huzungumzia au kuonesha ishara ya kile alichokifanya


hufuata malekezo rahisi
hutanzua chemshabongo nyepesi
huelewa kuhesabu
huelewa kanuni au amri
hucheza na watoto wengine
Nasikitika.
Pole sana.
huonesha hisia nyingi
hunakili na kuchora sura au umbo rahisi
huweza kutembea kinyumenyume kwa urahisi
huruka kwa mguu mmoja


Watoto wadogo ambao hawawezi kutenda stadi 2 kutoka sehemu mojawapo sehemu kwenye mduara watanufaika kutokana na shughuli ambazo husaidia watoto kuendelea katika nyanja hiyo. Lakini picha hizi ni mifano tu ya stadi. Kwa mfano, katika nyanja ya stadi za kijamii: mtoto wako hapaswi kufanya tendo la kumsikiliza mwalimu. Swali la kujiuliza ni iwapo mtoto wako anaelewa kanuni au amri kama ilivyo kwa watoto wengine.
Kumbuka kuwa mtoto atajifunza vizuri kwa kufanya shughuli ambazo watoto wengine wenye umri wake katika jamii yake wanafanya.

No comments