TATIZO LA URIC ACID KUZIDI KIASI KWENYE DAMU



Kupanda kwa uric asidi kwenye damu ni hali ambayo hutokea endapo kiwango cha uric asidi kimekuwa kikubwa kuliko kiwango cha kawaida. Figo kuferi ni kisababishi kinachoongoza kusababisha kupanda kwa uric asidi kwenye damu kwa asilimia 85 hadi 90, wakati asilimia 10 hadi 15 huchangiwa na matatizo mengine yanayosababisha kuongezeka kwa uzalishaji wa uric asidi kwenye damu.
Uric asidi hutokea wapi?
Uric asidi hutengenezwa kwenye damu kutokana na kuvunywavunywa kwa kiungo kimojawapo kinachotengeneza vinasaba kiitwacho purine ambacho hupatikana kwenye vyakula na pia huzalishwa mwilini. Baada ya kuzalishwa uric asidi husafilishwa kwa njia ya damu na kuelekea kwenye figo kwa ajili ya kutolewa kwenye mkojo kwa kiasi kukubwa na kuacha kiasi kidogo kwenye damu ambacho hakina madhara.
Inasemekana mtu mmoja kati ya watano huwa na kiwango cha juu cha uric asidi kwenye damu. Kuwa na kiango cha juu cha uric asidi huambatana/husababisha matatizo ya gauti na kufanyika kwa mawe kwenye figo, licha ya hivyo watu wenye kiwango cha juu cha uric asidi huwa hawaonyeshi dalili.



Vihatarishi ni vya kupanda kwa uric aside kwenye damu na hatari ya kupata tatizo la gauti ni
  • Kunywa pombe kupita kiasi (bia na pombe jamii ya spiriti)
  • Kula vyakula vyenyenyama, au nyama kwa wingi na viumbe wa baharini, uyoga, maharage makavu, kunde, ini na vingine
  • Matumizi ya dawa za kupunguza maji mwilini
  • Dawa jamii ya beta blocker
  • Dawa jamii ya ACE na ARB(isipokuwa lorsatan)
  • Presha kuwa juu(shinikizo la damu lililopitiliza)
  • Uzito kupita kiasi
  • Matumizi ya dawa za kushusha kinga za mwili

Visababishi vya kupanda kwa uric aside kwenye damu kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa purine na kemikali ya urate ambavyo vimegawanyika katika makundi mbalimbali ikiwa pamoja na
Matatizo ya kurithi kama
  • Upungufu wa kimeng’enya HGPT(hypoxathine guanine phosphoribotransferase)
  • Kuongezeka kwa utendaji kazi wa kimeng’enya cha PTS
  • Upungufu wa kimeng’enya cha Glucose-6-phosphate
 Magonjwa kama
  • Udhaifu katika Uzalishaji mwingi wa chembe hai za myeloid, lymphocyte
  • Saratani mbalimbali
  • Madhaifu ya uvunjwaji wa chembe nyekundu za damu
  • Ugonjwa wa ngozi wa psoriasis
  • Uzito kupita kiasi
  • Kukosa hewa ya oksigeni
  • Tatizo la down syndrome
  • Magonjwa ya uhifadhi wa glycogeni aina ya III, V na VII
Dawa, chakula, na sumu
  • Pombe ya ethanol
  • Kula vyakula vyenye purine kwa wingi(kama nyama nyekundu)
  • Upungufu wa vitamin B12
  • Madawa ya kutibu saratani (yanayo uwa seli)
  • Matumizi ya sukari aina ya fructose
  • Dawa ya ethylamino-1,3,4 thiadiazole
  • Dawa aina ya 4 amino-5-imidazole carboxamide ribose

Visababishi vya kupanda kwa uric aside kwenye damu kutokana na kupungua kwa uondolewaji wa uric asid kwenye damu
Visababishi hivi vimegawanyika katika makundi mbalimbali yakiwa pamoja na
Mgonjwa kama
  • Tatizo sugu la figo kufeli
  • Magonjwa ya figo yaliyo sababishwa na sumu ya madini risasi
  • Kupungukiwa na maji mwilini (moyo kuferi, au kupoteza maji)
  • Kupanda kwa ketone kunakosababishwa na kisukari(DKA) au mfungo wa chakula
  • Kupanda kwa kiwango cha lactic asidi kwenye damu
  • Shinikizo la damu linaloelekea kuwa kifafa cha mimba(preeclampsia)
  • Uzito kupita kiasi cha kawaida
  • Kiwango cha homoni ya parathyroid kuwa juu
  • Kiwango cha homoni ya thyroid kuwa chini
  • Tatizo la sarcoidosis
Dawa na chakula
  • Dawa za jamii ya thiazide
  • Dawa ya cyclosporine na tacrolimus
  • Dozi kidogo ya dawa jamii ya aspirini
  • Dawa ya Ethambutol
  • Dawa ya pyrazinamide
  • Pombe
  • Dawa ya levodopa
  • Dawa ya methoxyflurane
  • Matumizi yaliyokithiri ya vilegeza mwili
  • Kutokutumia chumvi

Madhara
Madhara ya kupanda kwa uric asidi kwenye damu huweza kupelekea matatizo ya
Kuganda kwa uric asidi kwenye ogani mbalimbali za mwili ambayo hupelekea matatizo ya
  • Gauti
  • Ugonjwa sugu wa figo
  • Kufanyika kwa mawe ndani ya figo

Matatizo yasiyotokana na kuganda kwa uric asidi kwenye ogani mwilini
  • Presha ya juu ya damu( shinikizo la damu la juu)
  • Ugonjwa sugu wa figo
  • Magonjwa ya moyo
  • Kuonekana kwa dalili za kisukari
Wakati gani wa kumwona daktari
Kupanda kwa uric asidi huwa hakuambatani na dalili maranyingi, endapo kiwango chako cha uric asidi kimepanda kupita kiasi unaweza kuanza kuepuka visababishi na endapo umepata madhara ni vema kuonana na daktari ili muongee kuhusu matibabu.

Post a Comment

No comments