Mtoto
wa jicho kwa lugha nyingine cataract hutokana na kufanyika kwa ukungu
katika lensi ya jicho, mtu aliye na ukungu huu kuona kwake ni sawa sawa
na mtu anavyoona nje kupitia dilisha la kioo lenye ukungu wa barafu au
maji dilishani mvua inapokuwa inanyesha.
Ukungu
katika lensi ya jicho husababisha mtu kusindwa kufanya kazi zake kama
kuendesha gari, kusoma sana sana usiku au kuona nyuso za watu vyema.
Ukungu huu hutokea na kuendeea kufunika jicho zima pole pole kwa muda
Fulani na hatimaye mtu anashindwa kuona kabisa.
Kwa
mara ya kwanza ukungu unapoendelea kutokea mtu anaweza kupata miwani
inayoweza kumsaidia kuona lakini baada ya muda Fulani kupita mtu anaweza
asione kabisa mpaka afanyiwe matibabu mengine ya upasuaji.
Matibabu
ya upasuaji ni salama rahisi yenye uhakika na ni ya muda
mfupi, huchukua mda mfupi mgonjwa kupona na kurudia kazi zake za
kawaida.
Jinsi ukungu wa jicho unavyotokea
Aina
nyingi za ukungu machoni au mtoto wa jicho huwa ni tatizo linalotokea
kama mabadiliko kwenye lensi ya jicho kadri mtu anavyozeeka.
Baadhi ya watu hurithi hali ya kupata tatizo hili la ukungu kwenye macho na huwa hatarini kupata mapema zaidi.
Ukungu kwenye jicho unaweza kusababishwa na mambo mengine mengi kama
-
magonjwa-kama kisukari,
-
jeraha au
-
kufanyiwa upasuaji wa jicho,
-
madawa aina ya steroid pia husababisha kufanyika kwa ukungu kwenye lensi ya jicho
Mtoto
pia anaweza kuzaliwa na ukungu kwenye jicho au kupata ukungu
anapoendelea kukuwa unaotokana na maambukizi kwa mama wakati wa
ujauzito.
Ukungu
huu kwenye lensi mara nyingi haudhuru kuona kwa mtoto lakini kama
ukigunduliwa mapema unabidi kuondolea mara baada ya kugunduliwa.
Jinsi gani ukungu unafanyika kwenye lensi ya jicho
Lensi-(ambapo ukungu huu hutokea)huwa nyuma ya sehemu nyeusi ya jicho inayoonekana mtu akitazamwa kwenye jicho.
Lensi
hii hufanya kazi ya kuelekeza mwanga sehemu ya jicho inayoitwa rentina
ambapo hapa mwanga huo hubadilishwa na kufanywa kuwa umbo la kitu kama
vile tunavyoona tukiangalia vitu vinavyotuzunguka.
Ukungu
huu unapofanyika husababisha kutawanywa kwa miali ya mwanga na hivyo
haiingii kwenye rentina hatimaye mtu anaona ukungu na dalili zingine
zinazompata mwathilika wa tatizo hili.
Mtu anapoendelea kuongezeka umri na kuzeeka kuta za lensi huongezeka upana na kusababisha uwezo mdogo wa kupitisha mwanga.
Kwenye
umri mkubwa pia, chembe hai za lensi huvunjika na kutuwama pamoja
kutengeneza ukungu sehemu moja wapo ya ndani, ukungu unapoendelea
kufanyika basi mtu anapoteza hali ya kawaida ya kuona.
Ukungu
kwenye jicho unaweza kutokea kwenye jicho moja tu, lakini mara nyingi
hutokea kwenye macho yote mawili . Mara nyingi pia si lazima macho yote
mawili yapatwe na dalili zinazofanana hivyo ukungu kwenye jicho moja
unaweza kuwa na dalili mbaya zaidi ya jicho jingine.
Vihatarishi vya kupata ukungu kwenye lensi ya jicho
Mambo yafuatayo yanamuweka mtu hatarini kupata mtoto wa jicho;
-
Kuongezeka umri(umri mkubwa-uzee)
-
Kisukari
-
Kunywa pombe kupita kiwango
-
Kukaa sana kwenye mwanga wa jua
-
Kupatwa maranyingi na mionzi kama ya X-ray au matibabu saratani kwa njia ya mionzi
-
Historia ya mtoto wa jicho kwenye familia
-
Shinikizo la juu la damu
-
Kitumbo-obesity-uzito kupita kiwango
-
Kuumia jicho au michomo kwenye jicho
-
Kufanyiwa Upasuaji wa jicho/macho
-
Matumizi marefu aina ya steroids
-
Uvutaji wa sigara
Dalili za mtoto wa jicho-Cataract
Dalili za mtu mwenye mtoto wa jicho au ukungu
kwenye jicho huwa ni kati ya zifuatazo;
- Kuona ukungu au vitu vimefifia
- Kupata shida kuona wakati wa usiku
- Kuumizwa macho kwa mwanga au miali ya mwanga ambapo mtu wa kawaida haoni kwamba ni tatizo
- Kuona nusu duara au duara kwenye mwanga unaongaa au miali ya mwanga kama vile upinde wa mvua unayokaa.
- Kubadilisha mara kwa mara kwa lensi ya miwani kutokana na hali ya macho kuwa mbaya
- Kuona rangi zimefifia au rangi ya vitu kuwa njano
- Kuona kitu kimoja kwamba ni viwili katika jicho moja
Mwanzo wa tatizo hili la ukungu kwenye lensi
ya jicho huweza kudhuru sehemu ndogo sana ya jicho kiasi kwamba hautapata
dalili zozote, muda unapoendelea na ukungu huu kutanda kwenye sehemu kubwa ya
lensi ya kicho ndio utakapoanza kupata dalili hizo
Wakati gani uonane na dakitari?
Fanya mipango ya kuonana na dakitari endapo unaona
kuna mabadiliko yoyote katika macho yako kama kuona kitu kimoja kuwa marambili,
kuona ukungu n.k
Vipimo vya kufanya
kupima kujua kama una mtoto wa
jicho dakitari atafanya vipimo vifuatavyo mara baada ya kuchukua historia ya
ugonjwa wako
·
Kukuomba usome
charti yenye maandishi makubwa na madogo kuona kiwango chako cha kuona
kitaalamu huitwa visual acuity test. Jicho moja hufunikwa na baada ya
kupimwa hivyo hivyo jingine hufunikwa na kupimwa pia
·
Kutumia kifaa cha
kamera na mwanga kuangalia jicho na lensi ya jicho kifaa kinajulikana kama
microscopy
·
Kutanua dilisha
la jicho kwa ajili ya kuchunguza rentina
·
Dawa aina Fulani
ya matone inawekwa na dakiatri kwenye macho inayosaidia kutanua mlango wa jicho
na kumrahisishia kuona vyema kwa lensi ya jicho na baadae atatumia kifaa
kinachoitwa ophthaloscope na kuona kama kuna ukungu wowote au tatizo jingine
Matibabu ya cataract
Matibabu
ya ukungu kwenye lensi ya jicho kwa njia ya upasuaji hutegemea maamuzi
ya mgonjwa na dakitari kwamba ni lini afanyiwe matibabu hayo.
Ukungu
kwenye lensi ya jicho mara nyingi hausabaishi matatizo yoyote na hata
kama mtu akichelewa kufanyiwa matibabu hakutadhuru uwezo wa kuona
atakapofanyiwa upasuaji wakati wowote ule.
Matibabu
ya tatizo hili hutegemea dalili alizonazo mgonjwa jinsi zinavyoathiri
mfumo wa maisha yake kama kusoma au kuendesha gari wakati wa usiku. Mara
baada ya kufanyiwa upasuaji dakitari atakuomba uwe unaludi kliniki ili
kutathmini maendeleo yako
Upasuaji
Upasuaji
wa kuondoa ukungu kwenye macho au cataract hufanywa kwa kuondoa lensi
ile iliyohalibika na kuwekwa lensi nyingine bandia.
Lensi hii huwekwa mahali lensi ya asili ilipokuwa na mara baada yakuwekwa hukaa kwa muda wote unaoishi
Kwa
baadhi ya watu baada ya kuondolewa kwa lensi asilia ya jicho, uwekaji
wa lensi ya bandia hauwezi kufanyika na hivyo mtu atapewa miwani tu
kumsaidia kuona
Upasuaji
wa kuondoa lensi hii ya asili na kuweka ya bandia hufanyika kwa muda
mfupi na mgonjwa anaweza kuruhusiwa siku hiyo hiyo kwenda nyumbani.
Upasuaji
unapokuwa unafanyika mgonjwa anapewa ganzi sehemu ya jicho ili
kutosikia maumivu, hivyo mgonjwa huwa macho wakati wote wa upasuaji
Madhara yanayoweza kutokana na upasuaji mara chache huwa ni
-
kuharibiwa kwa rentina ya jicho hivyo kusababisha upofu
-
kutokwa na damu
Baada
ya upasuaji utajisikia hali isiyo ya kawaida baada ya siku chache na
baada ya wiki nane utakuwa umepona kabisa. Kama una ukungu katika macho
yote mawili basi dakitari atapanga matibabu ya jicho jingine baada ya
mwezi 1 au 2 kupita tangu kufanyiwa upasuaji wa jicho moja
Habar doctor naitwa happiness sospeter naomba kuuliza nilifanyiwa operation ya jicho mwaka 2016 December nilikuwa nasumbuliwa na mtoto wa jicho. Lakn mapaka sasa napata shida kuona wakat wa usiku alaf nikitumia dawa ya macho gentamycin eye ointment jicho linaweka ukungu . he nitumie dawa gan
ReplyDelete