UKWELI KUHUSU ENERGY DRINKS | INAVYOFANYA KAZI NA MADHARA YAKE.

Vinywaji vya kuongeza nguvu, visivyo na kilevi, kisayansi vinaelezwa vina kiasi kikubwa cha kafeini, vitamini pamoja na kemikali za taurine, glucuronolactone.Wakati mwingine pia huongezewa dawa aina ya guarana pamoja na mitishamba aina ya ginseng kwa lengo la kusisimua akili na kuongeza nguvu za mwili.

  vinywaji hivi vina kiasi kikubwa cha kafeini ambayo ni dawa inayosisimua ubongo na kwa kuvichanganya na pombe athari zake kwenye mfumo wa fahamu za mwili huongezeka.

Baada ya kuchanganya vinywaji hivi, kafeini katika vinywaji vya kuongeza nguvu, hupunguza athari za kilevi na kumfanya mtumiaji asibaini haraka kuwa amekunywa kiasi kikubwa cha kilevi. Hili ni jambo la hatari
 
Matokeo ya utafiti mmoja yaliyowasilishwa katika mkutano wa mwaka 2013 wa Chama cha Afya ya Moyo cha Marekani (American Heart Association) uliofanyika katika mji wa New Orleans, ilibainika kuwa kunywa kopo moja hadi matatu ya vinywaji vya kuongeza nguvu, kunaweza kusababisha maoigo ya moyo kudunde bila mpangilio na kuongeza shinikizo la damu, na kusababisha kifo cha ghafla.
Hii ni kwa mujibu wa utafiti wa T. Van Batenburg-Eddes na wenzake uliochapishwa katika jarida la Front Psychology toleo la 5, mwaka 2014.

Maelekezo yaliandikwa kwenye cupa za vinywaji hivi yana umuhimu mkubwa sana japo walio wengi hatuna tabia ya kusoma maelekezo kabla ya kutumia

JINSI GANI ENERGY DRINKS ZINAVYOFANYA KAZI KATIKA MWILI WA BINADAMU NDANI YA MASAA 24

Kwa ufupi  ni kwamba kiungo kikubwa kwenye energy drinks ni caffeine,Caffeine inafanya kazi ya kuzuia uzalishwaji wa kichocheo cha mwili kinachohusika na kulala na kuhisi uchovu.Caffeine inapozuia uzalishaji wa kichocheo hiki mfumo wa fahamu huhisi kwamba mwili umepata matatizo hivyo kufanya kazi kwa kasi sana kuliko kawaida.Katika hali ya kuhisi mwili upo katika hatari ubongo kupitia tezi ya pituitary unazalisha kichocheo kinachojulikana kama ADRENALINE,hiki kinahusika kuufanya mwili kuwa tayari kwa kupigana au kukimbia wakati wa hatari(Fight or flight response).Kichocheo hiki sasa baada ya kuzalishwa kwa wingi kinafanya mapigo ya moyo kwenda kasi,shinikizo la damu kuongezeka na mboni za macho kutanuka( pupil dilatation).Hapa sasa mtu hujihisi mwili umechangamka.

DAKIKA KUMI ZA KWANZA BAADA YA KUNYWA
Unapokunywa energy drink yoyote inachukua muda wa Dakika kumi (10) Caffeine kuingia kwenye mzunguko wako wa damu matokeo yake mapigo ya moyo na shinikizo la damu linaongezeka na kufanya mtu ujisikia mchangamfu hata kama ulikua mchovu uchovu utasikia kama umeisha.


DAKIKA 15-45
Hapa kiwango cha Caffeine kwenye damu inafikia kiwango cha juu kabisa(Peak level) hapa mtu ndo anajihisi uchangamfu wa mwili zaidi.

DAKIKA 45-50
ndani ya kipindi hiki Kiwango chote cha Caffeine uliyokunywa kinakuwa tayari kimeingia kwenye mzunguko wa damu,Hapa ini linakabiliana na Caffeine kwa kufanya mwili kufyonza sukari zaidi hata ile iliyokuwa imetunzwa sehemu mbali mbali za mwili kuirudisha kwenye mzunguko wa damu.

SAA 1
Baada ya saa moja tokea unapokunywa vinywaji hivi,Kiwango kikubwa cha sukari kilichoingia kwenye mzunguko wa damu kwa ghafla na Kiwango chha caffeine kinaanza kushuka hali inayopelekea mwili kuanza kuishiwa nguvu ,hapa mtu anaweza kuanza kujihisi mchovu.

MASAA 5 HADI 6
Caffeine inachukua muda wa saa 6 hadi 5 kuwa imetolewa mwilini kwa asilimia 50%,(half life) kwa hiyo ndani ya muda huu kiwango cha caffeine kinakua kimepungua ndani ya mwili kwa asilimia 50%

MASAA 12
Hapa kiwango chote cha caffeine kinakuwa kimeisha kabisa mwilini

MASAA 12-24
Kutokana na Caffeine kuisha,mwili unaanza kuzoea hali mpya ya bila caffeine,Hivyo mtu anaanza kupata kitu kinachoitwa Caffeine withdrawl sydrome,Mtu anapata matatizo yafatayo Kichwa kuuma,kushtukashtuka,kusahau,kukosa choo au kapata choo kigumu,misuli kuuma

MADHARA YA KIAFYA YANAYOWEZA KUTOKEA KUTOKANA NA MATUMIZI YA VINYWAJI HIVI

1.SHAMBULIO LA MOYO(CARDIAC ARREST)
Matumizi ya caffeine kwa kiasi kikubwa inapelekea kufanya misuli ya moyo kusinya na kutanuka kwa kasi sana ili kuongeza mapigo ya moyo hali inayoathiri utendaji kazi wa moyo na kusababisha moyo kushindwa kufanya kazi.
Soma hapa report ya utafiti uliofanyika nchini Canada na kuonesha kuwa kweli energy drinks zinasababisha shambulio la moyo: CANADIAN JOURNAL OF CARDIOLOGY RESEARCH ON ENERGY DRINKS
NDIO MAANA KATIKA CHUPA ZAKE UNASHAULIWA USINYWE WAKATI UNAENDA KULALA ILI UTAPOPATA SHIDA HII UWEZE KUOMBA MSAADA.
 Image result for CARDIAC ARREST
2.KIPANDA USO
Kama tulivyoona awali kiwango cha caffeine kinapoisha mwilini mtu anapata caffeine withdrawl sydrome inayoambatana na maumivu ya kichwa.Mtu anavopata caffeine withdrawl syndrome mara kwa mara inapelekea tatizo la kipanda uso

2.SHINIKIZO LA DAMU KUWA JUU( PRESHA YA KUPANDA)
Utumiaji wa vinywaji hivi inaweza kupelekea mtu kupata tatizo la shinikizo la damu kuwa juu(High blood pressure) Kwa inaathiri utendaji kazi wa misuli ya moyo

3.ADDICTION
Watu wengine wanaweza kupata caffeine addiction kwamba anakuwa hawezi kufanya kazi kwa ufanisi mpaka atumie energy drinks.

4.KISUKARI
kama nilivyoelezea awali jinsi gani energy drinks zinaathiri sukari mwilini,hii inapelekea kuvuruga utendaji kazi wa kongosho hasa sehemu inayozalisha Insulin na kupelekea mtu kupata tatizo la kisukari.

5.KUHARIBU MIMBA
Ndio maana kinywaji hiki hakiruhusiwi kutumiwa kwa mama mjamzito kwani kinaweza kupelekea kuharibu maumbile ya mtoto (kuzaa mtoto mwenye ulemavu) au kuharibu kabisa mimba


Kama ilivyo unapotumia kitu chochote kwa kiwango zaidi na ulichoelekezwa ni  hatari kwa afya yako.Tutumie energy drinks kama ilivyoelekezwa kwamba ndani ya masaa 24 usizidishe chupa zaidi ya mbili.

Watu wengine wamekuwa wakihoji mamlaka za vyakula na dawa(TFDA),TBS kwa nini waruhusu vinywaji hivi kuuzwa kwa watu.tunachosahahu ni kwamba mamlaka hizi zinaifanya kazi yao vizuri kwa kudhibiti kiwango cha caffeine na viambata vingine vilivyo katika bidhaa hizi ndani ya chupa moja haviko katika wingi unaoweza kudhuru mwili. tatizo ni kwa watumiaji pale unapoelekezwa usizidi kiwango fulani ukazidisha.
AFYA YAKO NI JUKUMU LAKO.




19 comments:

  1. Sasa kama ukitoka kufanya mazoezi kisha ukanywa nini kitafanyika ndani ya mwili wako kwa muda huo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Unawez kufa kwa kuw mapig ya moy yanaend mbio sna alaf pia kinywji iki kinashtua ADRENALINE HORMONE

      Delete
  2. Je mama mjamzito ikatokea akanywa chupa tatu itakuwaje

    ReplyDelete
    Replies
    1. Italeta madhara kwa mtto atakaezaliwa au hta kuharibu mimba kabisa

      Delete
  3. asante kwa ushauri kweli jukumu la afya ni juu ya mtumiaji mwenyewe

    ReplyDelete
  4. Tufanye nn ili tuache kunywa Mara Kwa mara

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwa ushaur wa kiafy ni kwamba unapopatwa na ham ya kutumia kinywaj icho basi jitahid unywe juice za matunda kwa wing ili kuondokan na uteja wa kinywaj icho angamizi

      Delete
  5. Vp ukinywa nusu na unaujauzito? Je Kuna madhara ?

    ReplyDelete
  6. Vip kwenya tendo la ndoa kunamathara!

    ReplyDelete
  7. Ok nimeelewa from now I stop it to drink again energy drinks....

    ReplyDelete
  8. Km umefnya abortion hailet mazara ukitumia energy drink

    ReplyDelete
  9. kama ulikunywa ukiwa na ujauzito wa kama mwezi inaweza kuwa na madhara?

    ReplyDelete
  10. Je mimba ya umri gani ndio hatari zaidi kuharibika baada ya kutumia energy

    ReplyDelete
  11. Hv kuna ukwel wote ya kuwa energy drinks humfanya m2 kuzeeka haraka?

    ReplyDelete
  12. Kunabaadhi ya vinywaji ya paswa kudhuiliwa kwa manufaa ya watu wote

    ReplyDelete
  13. Je Kam uko kwenye siku atalii na ukawa umefanya MAPENZI kunauwezakno wa kupata mimba???

    ReplyDelete
  14. Vp mjamzito mwenye mimba changa akanywa energy nne kwa xk nn kitatokea

    ReplyDelete