Ni aina ya ukatili unaohushisha mwanaume na mwanamke,
unaotokana na jinsi wanavyohusiana na hali ya kutokuwepo kwa uwiano kati yao.
Ukatili huu hufanywa kwa mtu kwa sababu tu ya jinsi yake.
Ukatili wa kijinsia huathiri wanawake zaidi kuliko wanaume.
a)
Ukatili wa kimwili
Ni kitendo
anachofanyiwa mtu kinachohusisha kuumizwa mwili na huweza kuonekana moja kwa
moja au mwathirika kuhisi maumivu bila watu wengine kutambua kitendo hicho.
Mifano ya ukatili wa kimwili ni vipigo, shambulio la mwili, kuchomwa mwili
moto, matumizi ya silaha, kuvuta nywele, kusukuma, kunyonga mkono au mguu,
kumpiga kichwa ukutani/sakafuni na kuchomwa na kitu chenye ncha kali sehemu
yoyote ya mwili
b)
Ukatili wa
kisaikolojia
Ni ukatili ambao mtu
anatendewa na unamsababishia maumivu kiakili/kihisia ambapo mtu mwingine hawezi
kutambua kuwa mwenzake ametendewa ukatili hadi mazingira yatakapojitokeza na
mtendewa akajieleza. Mifano ya ukatili wa kisaikolojia ni matusi kwa njia ya
maneno au ishara yenye lengo la kudhalilisha, vitisho na kutishia kufanya fujo,
maneno ya kufedhehesha, kudharauliwa hadharani, kutishia kutoa siri, kuingiliwa
faragha, kutishiwa kuuawa, wivu wa kupindukia, kunyang'anywa watoto kwa
makusudi.
c)
Ukatili katika
uhusiano wa kingono
Ukatili
huu huambatana na vitendo vinavyohusiana na masuala ya ngono. Mfano
unyanyasaji/bughudha za kijinsia, kujamiiana kwa maharimu, ubakaji ndaniya
ndoa, ulawiti,utekaji na usafirishaji wa wanaume au wanawake na watoto kwa
ajili ya ngono, utumwa wa kingono, mashambulio na kuingiza vitu vigumu kwenye
sehemu za siri.
d)
Ukatili wa kiuchumi
Ni aina ya ukatili ambao unamnyima fursa za kiuchumi
mwanamke au mwanaume katika kujiongeza kipato na kuchangia katika maendeleo.
Aina hii ya ukatili huwapata wanawake kutokana na hali yao ya kuwa tegemezi kwa
wenzi wao . Mifano ya ukatili huu ni kunyang'anywa mali, ubaguzi katika fursa
za kiuchumi na umilikiwa mali, ubaguzi katika fursa za kujipatia mahitaji
muhimu ya chakula, malazi na mavazi, kunyimwa haki za kurithi, elimu duni na
mianya finyu ya fursa za kujielimisha, kunyimwa sehemu ya mapato ambayo ni
jasho lako na kukatazwa kufanya kazi.
e)
Ukatili unaotokana na
tamaduni au mila potofu
Huu unatokana na mila
na desturi za jamii zetu ambazo zinakinzana na haki za binadamu hivyo kuchangia
kuwepo kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia. Kwa mfano ndoa za kushurutisha,
ndoa za utotoni, kutakasa wajane, kurithi wajane, ukeketaji, matambiko ya
kingono kwa watoto, ndoa za maharimu, kufungiwa au kuwekwa ndani kwa shuruti, ndoa
za ushirika, miiko ya chakula na ukatili utokanao na mahari
a)
Athari kwa mtu binafsi
i.
Athari ya kisaikolojia
ii.
Athari ya kimwili
b)
Athari katika ngazi ya
familia
Ukatili wa kijinsia
unaweza kusababisha madhara mengi katika familia. Baadhi yake ni kupotea kwa
amani na upendo, kujenga uhamasa kati ya wanafamilia, watoto kutoroka nyumbani,
kupoteza pato la familia kwa kutibu majeraha yanayotokana na vitendo vya
ukatili, kupoteza wazazi au watoto.
c)
Athari katika ngazi ya
jamii
Kupoteza nguvu kazi ya jamii, muda na mali katika
kushughulikia maswala ya ukatili wa kijinsia, ongezeko la watoto wa mitaani,
migogoro na umaskini.
d)
Athari katika ngazi ya
taifa
Madhara ya ukatili wa kijinsia hapa ni pamoja na kupoteza
nguvukazi ya taifa, ongezeko la watoto mitaani, ongezeko la uhalifu, maendeleo
duni, kupoteza rasilimali na kuongezeka kwa umaskini.
-Afisa Ustawi wa Jamii -Afisa maendeleo ya jamii -Polisi
dawati la jinsia -Afisa mtendaji kata
-Paralegal



No comments