Wataalamu
wa afya wanasema fenesi huongeza ufanisi wa mfumo wa kinga mwilini na
kusaidia kuongeza kinga dhidi ya kifua, mafua na kikohozi. Hii ni kwa
sababu ya kuwa na vitamini za aina mbalimbali.
Fenesi
ni miongoni mwa matunda ya msimu yenye umbo la kipekee na ladha tamu ya
aina yake. Tunda hili linatajwa kuwa na faida lukuki kiafya kwa mwili
wa mwanadamu. Kula gramu 100 tu ya fenesi huweza kuupatia mwili nguvu ya
kalori 95.
- Tunda hili lina nyama laini iliyojaa sukari aina ya fructose na sacrose inayoweza kuupatia mwili nguvu na kuuhuisha kwa haraka.
- Fenesi limejaa ufumweli au fibre, sifa inayosaidia kulainisha choo.
- Tunda
hili lina virutubisho kadha wa kadha vyenye faida kubwa mwilini. Baadhi
ya virutubisho hivyo ni vitamini A, C, B complex, vitamin B6, folic
acid, niacin, riboflavin na madini za aina mbalimbali kama vile
potassium, magenesium, manganese na chuma. Katika tunda la fenesi kuna
protini, mafuta, wanga na antioxidants. Fenesi pia linatajwa kuwa chanzo
kizuri cha nishati kisichokuwa na mafuta. Si hayo tu, bali pia kwa kuwa
na virutubisho vyenye uwezo wa kuondosha sumu mwilini.
- Ttunda hilo linaweza kuukinga mwili dhidi ya saratani na magonjwa mengine
- Pia kuongeza uwezo wa kuona.
- Kiasi
kikubwa cha madini ya potassium kinachopatikana katika fenesi hulifanya
tunda hili liwe na uwezo pia wa kuimarisha mifupa na afya ya ngozi.
Wataalamu
wa afya wanasema fenesi huongeza ufanisi wa mfumo wa kinga mwilini na
kusaidia kuongeza kinga dhidi ya kifua, mafua na kikohozi. Hii ni kwa
sababu ya kuwa na vitamini za aina mbalimbali. Faida nyingine ni
kurekebisha msukumo wa damu na pia husaidia kurahisisha mmeng'enyo wa
chakula tumboni pamoja na kuukinga mwili dhidi ya magonjwa ya moyo na
kupooza. Sio vibaya kuelewa kuwa inasadikika kwamba tunda hili lina
uwezo wa kuukinga mwili dhidi ya ugonjwa wa pumu na kupunguza makali ya
ugonjwa huo. Si hivyo tu, bali fenesi lina vitamini muhimu
zinazohitajika kwa ajili ya utengenezaji wa damu mwilini
No comments