Kinyesi huweza kuwa na rangi aina tofautu tofauti, Aina nyingi hizo hutokana na chakula ulichokula au ugonjwa fulani ndani ya mwili na hata kinyesi cha rangi ya kijani huchukuliwa kama rangi za kawaida.
Aina chache za rangi ya kinyesi hushukiwa kwamba kuna kitu Fulani mwilini hakiko sawa ama kuna ugonjwa ndani ya mwili unaotakiwa kutibiwa
Rangi ya kinyesi mara nyingi huathiriwa na nini unachokula na kiasi cha nyongo- majimaji yenye rangi ya njano-kijani yanayotumika kumen’genya chakula cha mafuta.
Nyongo inapokuwa inasafili kwenye utumbo hubadilishwa na vimengenya vingine na kubadilika rangi kutoka kijani kwenda Kahawia
Kama kinyesi chako kina rangi nyekundu ambapo inamaanisha kuwepo kwa damu tafuta haraka matibabu ya daktari.
Aina tofauti ya rangi ya kinyesi na maana zake na nini kinachosababisha rangi hiyo
Rangi ya kijani
Inamaanisha nini?
Kuwa na rangi ya kijani inaweza kumaanisha kuwa chakula wakati kipo kwenye utumbo kilikuwa kinapita kwa kasi zaidi, mfano kwa sababu ya kuhara n.k. Kupita kwa kasi hiyo husababisha nyongo kutopata muda wa kumen’genya chakula hicho ipasavyo
Chakula madawa yanayoweza kusababisha kinyesi kuwa na rangi ya kijani ni nini?
Kula Mboga za kijani kwa wingi, vyakula vyenye rangi ya kijani kama vyakula/vinywaji vyenye rangi ya kijani na vidonge vya madini chuma
Rangi mpauko ama rangi ya udongo
Nini huweza kusababisha?
Kukosekana kwa nyongo katika kinyesi. Hii inaweza kumaanisha kuwa mirija inayopitisha nyongo imeziba. Mtu pia anaweza kuwa na manjano endapo mirija ya nyongo imeziba
Chakula au madawa yanayoweza kusababisha hali hii ni nini?
Aina Fulani za madawa, kama bismuth subsalicyclate na madawa mengine ya kuzuia kuhara husababisha mtu kuwa na kinyesi cha rangi hii.
Rangi ya njano na ya uterezi au inayonuka kama mnyama aliyekufa
Inamaanisha nini?
Kuwepo kwa mafuta mengi katika kinyesi, kama vile kwa sababu ya matatizo ya ufyonzaji wa chakula katika utumbo, kama ugonjwa wa celiac
Chakula kinachoweza kusaabisha ni nini?
Protini aina ya gluten kama inayopatikana kwenye chakula kama mkate na nafaka tofauti. Mwone dakitari kwa vipimo zaidi endapo unapata choo hiki kwa muda mrefu
Rangi nyeusi
Inamaanisha nini?
Kuvia kwa damu katika sehemu za mwanzo za utumbo kama vile kwenye tumbo, hali hii ya kuvia huweza kusababishwa na vidonda vya tumbo au majeraha ndani ya utumbo
Dawa ama vyakula vinavyoweza kusababisha hili ni nini?
Dawa za kuongeza damu zenye madini chuma, bismuth subsalicylate, ama matunda meusi kama furu n.k huweza kusababisha choo kuwa cheusi
Rangi nyekundu
Humaanisha nini?
Kuvia kwa damu sehemu za mwisho za utumbo mdogo kama vile utumbo mpana na mkundu mara nyingi husabaishwa na bawasiri
Dawa/vyakula vinavyoweza kusababisha rangi hii ni kama
Vyakula vyenye rangi nyekundu, nyanya, ama juisi yake na vyakula vingine vyenye rangi nyekundu huweza kusababisha hali hi pia.
No comments