MZIO/ALEJI YA DAWA

Madhara ya madawa yapo mengi na ya aina nyingi, na kila mtu hupata matokeo tofauti kwa dawa ileile, mwingine anaweza kupata vipele mwili mzima, au kuvimba au hata kupoteza maisha wakati mtu mwingine asipate madhara kabisa na badala yake Dawa ile ikamtibu vizuri. Asilimia 5-10% ya madhara ya madawa hutokana na alleji za dawa.
Alleji ya dawa hutokea pale ambapo kinga ya mwili hushambulia chemikali za dawa.
Dawa ziletazo alleji
Baadhi ya dawa zinazoweza kusababisha aleji ni: Antibiotiki, mf, penincilini Aspirini na dawa za kutuliza maumivu kama Ibuprofen Dawa za kuzuia degedege mf, lithium, phenobarbitone n.k Dawa za kuongeza kinga ya mwili (Monoclonal antibody therapy) Dawa za cancer (chemotherapy). Dawa za rheumatoid.
Watu gani wapo katika hatari?mtu yoyote anaweza kupata alleji ila hawa wapo kwenye hatari zaidi.:
·         Mtu mwenye alleji na kitu kingine, mfano chakula au dawa fulani.
·         Kuwa na historia ya alleji katika familia.
·         Kutumia dawa mara kwa mara, kwa muda mrefu au katika dozi ya juu sana.
·         Magonjwa mbalimbali ambayo huweza kusababisha alleji za dawa mf. HIV, EBV, n.k.



Dalili ni zipi?
Dalili kwamba una alleji na dawa:
·         Kutokwa na vipele mwilini.
·         Kuwashwa na mwili kuwa mwekundu.
·         Kuvimba uso, mdomo au mwili mzima.
·         Kupata homa.
·         Kupata mafua ghafla.
·         Kupata shida kupumua
·         Macho kuwasha na kutoa machozi bila sababu.
·         Kichefuchefu hata kutapika na kuharisha
·         Tumbo kuuma sana.
·         Kupata degedege na kupoteza fahamu.
Kumbuka!
Dalili hizi zinafanana na dalili za magonjwa mengi hivyo ni muhimu kufika hospitali kwanza na kumueleza daktari jinsi dalili zilivyoanza kabla ya kujiamulia kwamba una alleji na dawa.
Unapogundua kwamba una alleji, hakikisha unamwambia daktari kila unapoenda kutibiwa ili akupatie dawa mbadala.
"Upatapo Dalili zozote za Alleji ya dawa rudi ACHA kunywa dawa hiyo na rudi hospitalini mara moja kupata matibabu!!!!"

No comments