FAHAMU TATIZO LA VIFO VYA GHAFLA KWA WATOTO WACHANGA /SUDDEN INFANT DEATH

·        
Kitaalamu huitwa Sudden Infant Death Syndrome(SIDS) AU Crib death.Vifo vya ghafla kwa watoto wachanga imekuwa ni ngumu kwa wazazi kujua nini ni chanzo chake.Kwenye jamii zetu za kiafrica watu wengi huusisha vifo vya watoto na mambo ya ushirikina pale mtoto anapofariki bila kuumwa haswa akiwa usingizini,sababu wengi hawana elimu ya kutosha juu ya vifo vya ghafla .Takwimu inaonesha watoto wa kiume ndio wanaadhiriwa sana kuliko watoto wa kike.  Vifo Vingi huwapata sana watoto wenye umri wa 0 mpaka miezi 6 na kiasi kidogo kwa wa miezi 6-12.

     Chanzo chake haijajulikana moja kwa moja ila kuna vitu vinavyochochea kwa kiasi kikubwa ambavyo ni;

1.Kumlaza kwa tumbo ni hatari sababu upumuaji wake unakuwa wa tabu .Akilalia mgongo ni rahisi kupitisha hewa kuliko akilalia tumbo kwa njia ya koo la hewa. 

Tokeo la picha la SUDDEN INFANT DEATH
2.Sigara,uvutaji wa sigara ndani ya nyumba au eneo alilopo mtoto ni hatari. Mapafu yake hayaja komaa kupokea moshi mkali wenye sumu(NICOTINE) na kumuathiri kwa haraka.

3.Watoto wanaozaliwa chini ya wiki 38 (Njiti) wapo kwenye hatari ya kupata vifo vya ghafla.

4.Mama kama alitumia sigara ,pombe au bangi kipindi cha ujauzito anauwezo mkubwa wa kumsababishia mtoto kifo cha ghafla.
                          5.Watoto wenye maambukizi (infection) kwenye mfumo wa hewa.
NJIA ZA KUEPUKA KIFO CHA GHAFLA
1.Mlaze mtoto kwa mgongo –usimlaze ubavu au tumbo ili kumrahisisha apate hewa kwa kiasi kikubwa ifike mpaka kwenye ubongo ,hii itapunguza vifo vya ghafla.
2.Mama anaenyonyesha mtoto kwa kipindi cha mwaka na kuendelea anapunguza hatari ya kifo cha ghafla kwa mtoto kwa asilimia 50 kuliko mtoto anaepewa maziwa ya kopo.
3.Epuka matumizi ya sigara ndani ya nyumba au sehemu alipo mtoto.
4.Mnunulie Pacifier zile chuchu za kunyonya mdomoni zinazuia kifo cha ghafla.
Tokeo la picha la pacifier
5.Utakapo mlaza kitanda cha watu wazima hakikisha asijigonge ukutani au kusiwe na mpenyo kati ya kitanda na ukuta anaweza ingia kati na kukosa hewa na kubanwa.
6.Hakikisha kitandani hakuna nguo ,mashuka,toys au mto vikamziba pua akakosa hewa wakati wa kujigeuza na kumbuka mtoto mchanga hana uwezo wa kujitoa shuka iwapo litamfunika uso.
7.Mtoto kulala kitandani kwake anakuwa salama kumuepusha kujigonga kwenye ukuta ,pembe au kona za kitanda na kuanguka.
8.Epuka kumfunika shuka kubwa au zito .Mtoto anahitaji shuka jepesi na iwapo utalala nae hakikisha humfuniki na nguo zako au shuka puani akakosa hewa au mwili ukachemka sana .
MUHIMU:
Ni muhimu kumuangalia mtoto mara kwa mara pindi akiwa amelala unaweza ukamnunulia baby monitor inasaidia kumsikia akiwa anapumua ,Analia au anacheka inakuwa rahisi kujua kama kuna lolote linalo endelea chumbani.
Usimlaze mtoto moja kwa moja mara tuu anapotoka kunyonya ,hakikisha unamuweka begani mpigepige mgongoni abeuwe hata kucheuwa kwanza ,subiri baada ya dakika 5-10 sasa unaweza mlaza kitandani.

No comments