MZUNGUKO WA HEDHI USIOPEVUSHA MAYAI (ANOVULATORY CYCLE)




Hii ni hali ya mifuko ya mayai ya mwanamke (ovari) kutokomaza mayai na kuyaachilia ili yarutubishwe na mbegu za kiume.

Hata kama unapata hedhi haimaanishi kwamba kila unapopata hedhi yai limeachiliwa. Unaweza kupata hedhi na wakati yai halikupevuka na kuachiliwa. Dalili kubwa ya tatizo hili ni pale mwanamke anapata hedhi vizuri ila hashiki ujauzito.

DALILI
Mara nyingi wanawake wenye tatizo hili wanakua na mzunguko usioeleweka. Kama unapata mzunguko wenye siku chini ya 21 au zaidi ya 35 unaweza kuwa na tatizo hili. Na kama mzunguko wako una cku kati ya 21 hadi 34 lakini znabadilika kila mwezi inaweza kua ni tatizo hili.

Mfano mwezi fulan umepata mzunguko wa siku 28 ulofata siku 30 ulofata siku 34.

TATIZO HILI NA UGUMBA
Tatizo hili ni mojawapo ya ugumba kwa wanawake. Ina maana usipovusha yai kunakua hakuna yai la kurutubishwa ili kutengeneza mtoto. Hvyo huwezi kupata ujauzito yai lisipopevuka. Mwanamke anapokua na Ovulation isiyoeleweka anakua na chance ndogo ya kushika ujauzito.

DALILI ZA TATIZO HILI
1.Kukosa ute unaovutika kama ute wa yai
2.utando unaotengenezwa kwenye mji wa mimba kua mwembamba sana
3.kiwango kidogo cha hormone ya progesterone
4.kuwa na kipindi kifupi cha lutea (luteal phase) hiki ni kipindi baada ya kuachiliwa ambapo kinapaswa kua si chini ya siku 14.
4.kutokua na mabadiliko ya Joto la mwili (basal body temperature)

VISABABISHI
1.Mvurugiko wa hormone ,hii ndo chanzo kikubwa.
2.uzito ulopita kiasi
3.kufanya mazoez sana kupitiliza
4.hormone ya maziwa (prolactin hormone ) kuwa juu
5.ukomo wa hedhi
6.matatizo ya tezi ya thyroid
7.Stress,mfadhaiko na msongo wa mawazo

VIPIMO
Unaweza kugundua tatizo hili kwa kujipima mwenyewe nyumbani. Kwa kufata chart ya joto na ute( nligundisha) unapoona hakuna mabadiliko ya joto baada ya cku ya 14 basi ina maana hujapevusha yai. Pia unapokosa ute unaovutika ina maana hujapevusha yai.

Vipimo vingine ni
1.kiwango cha hormone ya estrogen baada ya siku ya 14
2.Ultrasound kuangalia kizazi na mifuko ya mayai

MATIBABU

Matibabu yanategemea chanzo chake. Baadhi ya sababu zinatibika kwa kubadili mfumo wa maisha. Mfano kula mlo kamili wenye vyakula vyenye glycaemic index ndogo. Kutofanya mazoezi kupita kiasi. Kupunguza uzito uliozidi.

Matibabu ya dawa.
Vyema kufika hospital uonanae na mtaalamu wa afya kabla ya kutumia dawa.

Dawa ya tatizo hili ni Clomifene. Inaonekana asilimia 80 ya wanawake waliotumia dawa hii imewasaidia kupata ujauzito.
Dawa hii inafanya kazi ya kuongeza uzalishwaji wa kichocheo cha mayai (follicle stimulating hormone)

Dawa hii unapotumia inabd kuwa mvumilivu kwani unaweza kupata matokeo baada ya kutumia kwa miez kadhaa. Unaweza kutumia kwa miez kadhaa usipate mafanikio hvyo unapaswa kuendelea kutumia kwa mzunguko unaofata. Endapo umetumia kwa miez sita kila mzunguko bila mafanikio ndo unapaswa kubadilishiwa dawa.

Kwa wanawake wenye tatizo la Polycystic ovarian syndrome  kutumia dawa ya METFORMINE inasaidia kupevusha mayai.

No comments