Watu wengi hupenda kuchanganya soya kwenye
mchanganyiko wa unga wa lishe ya mtoto. Wengine hawachanganyi kwa madai kwamba
zina madhara ya kiafya kwa mtoto.katika makala hii tutaona ukweli kuhusu jambo
hili.
Je ni salama?
Awali ya yote tukumbuke kwamba kitu
chochote kinapotumika kwa kiasi zaidi ya kiasi kinachopendekezwa kwa siku
kinaweza kuleta madhara ya kiafya katika miili ya watoto wetu.
Soya zina viambata aina ya Isoflavones
ambavyo vinafanana na hormone ya eostrogen. Viambata hivi vinapoingia mwilini
vinaweza kufanya kazi kama hormone ya estorogen na kushusha kiwango cha hormone
ya testoterone na kusababisha matatizo mengine kama kuota matiti au kwa watoto
wa kike kupelekea hali ya kuota matiti mapema. madhara haya hutokea pale
tusipozingatia viwango vinavyopendekezwa kuchanganya kwenye lishe ya mtoto.
VIPI KUHUSU MAZIWA MBADALA YA SOYA (SOY
BABY FORMULA)
formula hizi ni salama kwani kiwango cha
virutubisho kimewekwa sawa na formula/maziwa mbadala mengine mfano ya ng'ombe
nk. Japo formula zenye soya hazipaswi kutumika kwa makundi yafatayo
1.watoto njiti.
2.watoto wenye matatizo ya mzio(allergy)
3.watoto wenye wanaopata matatizo ya tumbo
wanapotumia maziwa ya aina yoyote.
JE SOYA INA VIRUTUBISHO VINGI?
Ni kweli soya ina kiasi kikubwa cha protein
ambayo ni muhimu kwa ukuaji wa mtoto.pia soya ina kiasi kikubwa cha madini
chuma.kwa hiyo inapowekwa katika kiwango sahihi inasaidia ukuaji wa mtoto.
KIASI GANI KINAFAA KWA MTOTO.
inashauriwa gram 5 hadi 10 protein ya soya kwa siku ambayo ni sawa na nusu kikombe cha maziwa ya soya,nusu kikombe cha maharage ya soya yaliyopikwa, au kijiko kimoja cha chakula cha unga wa soya.
ifatayo ni jinsi ya kuchanganya nafaka kwa ajili ya unga wa lishe ya mtoto.
No comments