Watoto huzaliwa na uzito tofauti na kila mtoto anaweza kukua tofauti kutegemea chakula anachokula mama na idadi ya kunyonya mtoto. Hata hivyo kama hali zote za kina mama na watoto zikiwa zinafanana watoto hao hukua katika kiwango sawa. Hapa chini kuna maelezo namna mtoto anavyotakiwa kuongezeka uzito na urefu kwa mwaka wa kwanza wa maisha yake;
- Mtoto hupoteza uzito wake kwa asilimia 5 hadi 10 wiki la kwanza baada ya kuzaliwa na baadae hujirudia uzito wake ndani ya wiki mbili
- Mtoto anapozaliwa mpaka miezi sita, mtoto atakuwa kwa sentimeta 1.5 hadi 2.5 kwamwezi, and kuongezeka uzito wa gramu 140 hadi 200 kwa wiki. na mtoto anapofikisha umri wa miezi mitanoanakuwa na uzito mara mbili wa ule aliozaliwa nao.
- Miezi sita na kuendele hadi mwaka 1. Mtoto huongezeka urefu wa sentimita 1 kila mwezi na uzito wa gramu 85 hadi 140 kwa wiki moja. Kwa ujumla mtoto huwa na uzito mara tatu zaidi ya kilo alizozaliwa nazo anapofikisha umri wa miezi 12(mwaka 1)
- Kati ya umri wa mwaka mmoja na miaka miwili mtoto atakuwa kilo 2.2 tu
- Kuanzia miaka 2 hadi mi 5 mtoto atakuwa kwa kilo 2.2 kila mwaka
- Kati ya miaka 2 hadi 10 mtoto hukua taratibu sana, lakini huanza kukua haraka sana kuanzia miaka 10 na kuelekea wakati mwingine huanza kukua haraka kuanzia miaka 9
- Mtoto anapoanza miaka mitatuhadi kumi ataongezeka sentimita 6 kila mwaka
Kwa kawaida mtoto hupimwa urefu na uzito kila anapohudhuria kliniki, uzito na urefu huchorwa kwenye kadi ya mtoto ili kuangalia ukuaji wake. Ni vema mama akaangalia ukuaji wa mtoto wake na kufuata ushauri wa daktari endapo moto hakui vema.
Mambo yanayo pelekea mtoto asikue vema ni haya yafuatayo
- Magonjwa ya kuzaliwa kama magonjwa ya moyo(tundukwenye moyo), mgongo wazi, mtindio wa ubongo n.k
- Magonjwa ya kuambukiza- mfano Kuharisha, kutapika sana, homa, malaria, n.k
- Kutonyonya maziwa kwa kiwango cha kutosha- Kwa kawaida mtoto anatakiwa kunyonya miezi sita mfululizo bila kuacha maziwa ya mama. Endapo mtoto ataanza kula vyakula kipindi hiki basi anaweza kupata magonjwa ya kuambukizwa
- Kutopata chakula bora chenye virutubishi muhimu
Kumbuka
- Mtoto hukua kiakili na kimwili, endapo mtoto hapati chakula vema basi atadumaa kiadili na kushindwa kujifunza darasani, kuelewa na kuwa na maisha yasiyo na mafanikio. Mlishe mtoto chakula bora na asilia chenye virutubishi vyote vya muhimu kutoka kwenye makundi yote ya chakula na si bora chakula.
- Mtoto anatakiwa kupewa vyakula vya aina tofauti ili aweze kuchagua kile kinachomfaa
- Mtoto asipopewa chakula aina tofauti ataweza kupendelea chakula aina moja tu kwenye maisha yake
- Mzazi unatakiwa kuonyesha mfano wa kula chakula bora ili mwanao aige kutoka kwako
Enter your comment...Dr. mbona hukuweka tena muendelezo wa suala la utosi wa mtoto hasa katika umbo la kichwa?
ReplyDelete