FAHAMU NI MUDA GANI UNATAKIWA KUMNYONYESHA MTOTO ILI ASHIBE

 


Mama anapomweka mtoto kunyonya ziwa moja huzalisha aina mbili za maziwa.
Maziwa ya mwanzo ambayo yanakuwa na maji mengi.
Maziwa ya mwisho ambayo haya yanakuwa mazito kuzidi yale ya mwanzo na yanakuwa na virutubisho vingi.

Maziwa ya mwanzo huwa ni maalumu kwa kukata kiu ya mtoto ndo maana yana maji mengi na virutubisho vichache.
Maziwa ya mwisho yanakuwa kwa ajili ya kumshibisha mtoto kwa kumpatia virutubisho vyote muhimu.

Ndio maana ili kuhakikisha mwanao ameshiba unashauriwa katika ziwa moja mtoto anyonye kwa dakika 15 hadi 20 kupata aina hizi zote za maziwa.

JINSI YA KUMPATIA MTOTO MAZIWA YA MWISHO.
Unashairiwa kumyonyesha mtoto kwenye ziwa moja kwa muda wa dakika 15 hadi 20 ili apate maziwa ya aina zote mbili. Katika siku za mwanzo baada ya kujifungua inaweza kuchukua muda mrefu maziwa kutoa maziwa ya mwisho hvyo inashauriwa zaidi kumpa ziwa mtoto kwa muda mrefu zaidi.

ATHARI ZIPI ZINATOKEA MTOTO ASIPOPATA MAZIWA YA MWISHO?
mtoto akiwa anapata maziwa ya mwanzo tuu anakosa virutubisho muhimu na kupelekea mtoto kutoongezeka uzito na kudumaa.

Pia mtoto anaepata maziwa ya mwanzo tu anaweza kupata dalili hizi
1.tumbo kujaa gesi
2.chango
3.kuharisha au kupata choo laini na chenye rangi ya kijani
4.mtoto kutoongezeka uzito.

No comments