Fragil inafanyaje kazi?
Dawa hii ni ya kuua vijidudu vilivyo kwenye
group la gram negative.. dawa hii inafanya kazi kwa kuharibu au kuvuruga
mpangilio wa vinasaba vya wadudu hawa (DNA) na kuwaua.
Inapoingia mwilini haibadiriki inabakia
kuwa hvyo hivyo Metronidazole na inasambaa sehemu zote za mwili ikiwemo
damu,mate,kizazi, placenta(kwa wajawazito) na ubongo.
Baada ya masaa 7 inaanza kupingua mwilini
kwani Ini linaitoa kupitia mkojo ndani ya masaa 24 inakua imeisha. Na inapokua
kwenye mkojo inatoka vile vile haibadiliki kuwa kitu kingine.
JE INAWEZA KUZUIA MIMBA?
ili kuzuia mimba inahitaji kubadili hali ya
ute uwe mzito kuruhusu mbegu kufikia yai na kuongeza hali ya asidi ya ute wa
ukeni na kwenye kizazi. Mbegu za kiume zinaweza kustahimili PH kuanzia 2.5
kuendelea ute unapokua na PH ndogo zaidi ya hapo basi mbegu hizi zikiingia
zinakufa. Ndo hvo dawa za uzazi wa mpango za dharura na dawa za kuua mbegu
zinavofanya kazi.
Baada ya kuangalia hayo tuone Fragili
(metronidazole) ina PH ya ngapi? Kama nlivosema inapoingia mwilini inasambaa
kama ilivyo haibadiliki kuwa kemikali nyingine Na Dawa hii inapoyeyuka kwenye
maji inakua na PH ya 6.5 hvyo hata ikiingia kwenye ute haishushi PH kuathiri
mazingira rafiki ya mbegu. Na pia haiathiri ute wa uke kuzuia mbegu kuweza
kuogelea.
Hivyo basi dawa hii haizuii mimba.
Bali inakuweka kwenye hatari ya kuzaa mtoto
mwenye mapungufu endapo mimba itatunga kipindi umemeza dawa hii.
No comments