Mkojo unakuwa na rangi mbali mbali.Ni wazi kuwa kila rangi
inaashiria kitu Fulani katika miili yetu.
Katika picha hii ina rangi mbali mbali za mkojo na chini ni
maana ya kila rangi.
1.HAKUNA RANGI/ANGAVU
Unakunywa maji mengi sana
2.RANGI YA MAJANI MAKAVU YA NGANO
Uko sawa kiafya
3.NJANO ANGAVU
Uko sawa kiafya
4.NJANO ILIYOKOZA WEUSI
Uko sawa lakini jitahidi kunywa maji ya kutosha.
5.RANGI YA ASALI
Mwili wako haupati maji ya kutosha
6.KAHAWIA ILIYOKOZA WEUSI
Uenda una tatizo la ini
Uenda hunywi maji ya kutosha.Jitahidi kunywa maji ya kutosha
sasa na endapo itaendelea mwone Daktari
7.WARIDI YENYE WEKUNDU
Je umekula matunda au vyakula vyenye rangi hivi karibuni?
Kama hapana inawezekana kuna damu kwenye mkojo
Yawezekana una matatizo ya Figo au sehemu nyingine za mfumo
wa mkojo.
Yawezekana umeathiriwa na madini ya zebaki au
risasi.Inashauriwa kumwona daktari
8.MACHUNGWA
Yawezekana hunywi maji ya kutosha
Inaweza kuwa una matatizo ya ini au tezi ya nyongo
Yawezekana ikawa sababu ya rangi ya chakula.Inashauriwa
umwone daktari
9.KIJANI AU BLUU
Kuna matatizo ya kimaumbile yanayoweza kupelekea hali
hii.Pia kuna aina ya bakteria wanaoathiri mfumo wa mkojo na kupelekea hali
hii.Inawezekana pia kutokea kwa sababu ya dawa au rangi ya chakula ulichokula.Mwone
daktari
10.ZAMBARAU
Hii ni nadra sana kutokea.ila vyema umwone daktari mapema
ufanyiwe vipimo
11.MKOJO UNATOA POVU
Hii haina madhara inaweza kutokana na Protini nyingi kwenye
mlo. Inaweza kuwa matatizo kwenye Figo.Inapozidi mwone daktari
VISABABISHI VYA NJE
Vitu unavyokula vinaweza kusababisha mabadiliko kwenye
mkojo.Pia matumizi ya dawa yanaweza kupelekea rangi au kiwango na harufu ya
mkojo kubadilika.
No comments