MADHARA YA KUMKATA MTOTO KIMEO

Wakati mtoto akiwa na kikohozi kisichoisha huwa ni utamaduni wa baadhi ya jamii kumfungua mtoto mdomo na kuangalia urefu wa Kimeo ambacho wengine katika pwani ya Kenya hukiita kilimi.
Ikiwa ni kirefu husemekana kuwa ndio sababu ya kikohozi sugu hivyo sharti kikatwe na wataalam wa kijadi.
Sasa  operesheni hii ya kijadi ni hatari na inaweza kusababisha madhara makubwa kiafya.

Kimeo (uvula) ni nini?Kimeo ni sehemu ndogo ya kinywa inayoning’inia mkabala na mwisho wa ulimi. Hivyo kila mtu huzaliwa na kimeo na kimeo sio ugonjwa.  

Kazi ya kimeo ni ipi?
  • Husaidia kinga ya mwili
  • Husaidia kulainisha koo
  • Husaidia kutoa sauti.
Je kwanini watu hukata kimeo?Kutokana na elimu potovu juu ya kimeo; mfano: Kimeo kimevimba na kikipasuka tu mtoto ndo anakufa, Kimeo kina usaha, Kimeo ni kirefu sana. n.k.

Watu wengine hufikiri kuwa kimeo kinasababisha magonjwa kama vile:- Kukohoa muda mrefu, au Kukonda au Kutapika mara kwa mara au Mtoto kulialia bila sababu. Hii si kweli. 

Je ni sahihi kukata kimeo? HAPANA! Kimeo hakipaswikukatwa kutokana na sababu yeyote ile!  

Nini madhara ya ukataji wa kimeo?Mtoto anaweza kupoteza damu nyingi na kupoteza maisha Maambukizi ya magonjwa mbalimbali kutokana na kutumia vyombo ambavyo si salama kukatia kimeo; mfano:- Pepopunda, Homa ya mapafu, Maambukizi ya VVU, Mototo kupata maumivu makali au Kupaliwa na chakula kupitia puani. 

Tufanyeje/Jitihada gani zifanyike ili kuzuia madhara haya yasitokee? Watoto wanao kohoa muda mrefu, wasiokua vizuri, wanaotapika mara kwa mara, n.k. wapelekwe kwa daktari kwa ajili ya uchunguzi na tiba

No comments