UGONJWA WA MINYOO AINA YA ASCARIS (ASCARIASIS)

Ugonjwa huu uathiri utumbo na unasababishwa na Minyoo inayojulikana kama Ascaris Lumblicoides.Ni aina ya minyoo inayowapata watu wengi.Asilimia 10 ya watu katika nchi zinazoendelea hupata ugonjwa huu kila mwaka(Report ya WHO). Ugonjwa huwapata sana watu wasiozingatia usafi wa mazingira na vyakula,pia watu wasiotumia maji safi na salama.
Mara nyingi mtu mwenye ugonjwa huu haouneshi dalili zozote lakini minyoo hii inapozaliana na kuwa mingi huweza kusababisha madhara kwenye utumbo,mapafu na hata inni.

NINI KINASABABISHA UGONJWA HUU
Unaweza kupata ugonjwa huu baada ya kula mayai ya minyoo ya Ascaris, ambayo yanaweza kuwa kwenye udongo,au chakula kilichochafuliwa na kinyesi cha binadamu mwenye ugonjwa huu.Watoto wanapata ugonjwa huu wanapoweka mikono yao mdomoni baadaya ya kuchezea udongo uliochafuliwa na mayai ya minyoo hii.


  1. Baada ya kula mayai ya minyoo hii upitia hatua zifatazo hadi kukomaa na kuleta madhara mwilini
  2. Mayai yanapofika kwenye utumbo mwembamba au mpana yanaanguliwa na kutengeneza Lava
  3. Lava walioanguliwa uingia kwenye mziunguko wa damu na kusafiri hadi kwenye mapafu ili kukomaa, Kipindi hiki mtu hupata kikohozi kikavu ambacho hata akitumia dawa za antbiotics hakiponi. Wengi huwatokea wakti wa usiku.
  4. Lava hawa wanapokomaa hupanda kupitia koo la hea hadi kwenye koromeo na kurudi tena kwenye utumbo na kuwa minyoo iliyokomaa na kuanza kutaga mayai.hapa mtu hujisaidia mayai ya minyoo hii kwenye kinyesi chake.


WATU GANI WAKO KWENYE HATARI YA KUPATA MINYOO HII
Ugonjwa huu unaonekana sana katika nchi zinazoendelea ikiwemo  bara la Africa,Latin America na Asia.Hasa hasa sehemu zisizokua na miondombinu mizuri ya usafi na maji safi na salama.
Vitu vifatavyo vinaongeza hatari ya watu kupata ugonjwa huu

1. Uhaba wa maji safi na salama
2.Kutumia kinyesi cha binadamu kama mbolea kwenye mazao ya vyakula kama mboga mboga  na matunda
3.Kutozingatia usafi wa mazingira na chakula
4.Miundominu mibovu ya maji taka

DALILI ZA UGONJWA HUU
Mara nyingi mtu mwenye minyoo hii haoneshi dalili.Dalili huonekana pale minyoo hii inapozaliana na kuwa mingi tumboni.Mtu huweza kupata dalili zifatazo.

Inapokuwa kwenye mapafu mtu hupata dalili:
1.Kikohozi au kubanja, mgonjwa huweza kupata dalili kama za ugonjwa wa Homa ya mapafu(Pneumonia)
2.Homa

Inapokua kwenye utumbo Mtu hupata:
Kichefuchefu
kutapika
maumivu ya tumbo
Kukosa choo au kuharisha
Kuhisi tumbo limejaa
Kupungua uzito
Image result for ascariasis


MADHARA YA UGONJWA HUU
Ugonjwa huu usipotibika mapema,minyoo inapozidi kukua na kuzaliana huweza kusababisha madhara yafatayo

1.Kuziba kwa utumbo. Minyoo hii inaweza kutengeneza mkusanyiko ambao unaweza kuziba utumbo.Tatizo hili ni hatari hivyo mtu anahitaji kupata msaada wa haraka,ikiwemo kufanyiwa upasuaji.

Image result for ascariasis

2.Kuziba kwa mrija wa nyongo(Bile duct) Minyoo hii inaweza kuingia kwenye mrija wa nyongo na kusababisha mrija huu kuziba

3.Ugonjwa wa kidole tumbo(appendicitis),minyoo hii inaweza kuingia kwenye kidole tumbo (appedix) na kuleta shida.

4.Kwa watoto minyoo hii hupelekea utumbo kushindwa kumeng'enya na kufyonza chakula na kupelekea utapiamlo kwa watoto.

MATIBABU
Ugonjwa huu hutibikwa kwa dawa za minyoo kama Mebendazole na albendazole.
Muhimu: Unapomeza dawa hakikisha unarudia tena baada ya week 2 kwani dawa hizi zinaua minyoo iliyokomaa na haziui mayai yake,Unaporudia kumeza tena baada ya miezi mitatu unaua na minyoo itakayokuwa imeanguliwa kutoka kwenye mayai yaliyokuwemo tumboni wakati unameza dawa mara ya kwanza.

JINSI YA KUJIKINGA
Njia kubwa ya kujikinga na tatizo hili ni kuzingatia usafi wa chakula na mazingira,
Kutumia choo kujisaidia na sio mbugani
kuosha kwa maji safi matunda na mboga mboga kabla ya kula
Kunawa mikono na maji safi na sabuni unapotoka kujisaidia
kuepuka matumizi ya kinyesi cha binadamu kama mbolea ya vyakula.

No comments