Neno CHIKUNGUNYA ni neno la kimakonde likiwa na maana ya kitu kilichobadilika umbile lake na kuwa tofauti na awali, wakichukulia dalili ya kuvimba kwa joint kunakosababishwa na ugonjwa huu.
Ugonjwa huu kwa mara ya kwanza uligundulika mwaka 1952 ambapo mlipuko wa ugonjwa huu ulitokea maeneo ya kusini mwa Tanzania hasa Mkoa wa Mtwara.Lakini kwa sasa ugonjwa huu umezikumba nchi nyingi duniani takribani nchi 60 kwenye mabara ya ASIA,ULAYA NA AMERICA. Hivi karibuni Ugonjwa huu umeripotiwa kutokea Mombasa nchini Kenya.
Ugonjwa huu unasabishwa na kirusi kilichopewa jina la chikungunya na kirusi huyu anatokea kwenye kundi la virus linalojulikana kama ALPHA VIRUSES.Kwenye kundi hili wapo pia virusi kama Dengue fever virus na zika virus.Ugonjwa huu eunezwa kupitia mbu,aina ya Aedes Egyptiae,tukumbuke kwamba mbu huyu ndo yule yule anaeeneza magonjwa ya zika na homa ya Dengue.
Mbu aina ya Aedes Egypti
DALILI ZA CHIKUNGUNYA
Dalili huanza kuonekana kwa mtu aliumwa na mbu mwenye virusi hivi ndani ya siku 4 hadi 8,Dalili za ugon jwa huu ni kama zifuatzao
- Homa kali
- Maumivu ya joint,Maumivu haya huwa makali hali inayoweza kupelekea mgonjwa kushindwa kutembea
- Maumivu ya misuli
- Maumivu ya kichwa
- Kichefuchefu na kutapika
- pia mtu anaweza kutokewa na mapele(Rash)
Asilimia kubwa ya wagonjwa wa ugonjwa huu upona kabisa ila kwa baadhi ya watu ugonjwa huu huweza kusababisha matatizo ya muda mrefu ya joint,kusababisha matatizo kwenye mfumo wa neva ,Matatizo ya moyo na upofu.
VIPIMO
Ugonjwa huu hupimwa kwenye damu kwa kutumia kipimo kinachojulikana kama ELISA(enzyme linked immunosorbent assays)
MATIBABU
Ugonjwa huu hauna tiba wala chanjo ,ila mgonjwa anaweza kupatiwa msaada wa kupunguza makali ya dalili za ugonjwa huu kama ifatavyo
- Kuongezewa maji ili kuepusha upungufu wa maji mwilini
- Dawa za kutuliza maumivu na homa kama Paracetamol
Muhimu:Usimpe mgonjwa wa aina hii dawa zenye aspirine ndani yake mfano aspirine,diclofenac na diclopar kwani unaweza kumletea madhara makubwa mfano mgonjwa kuazna kutokwa damu kila sehemu na kifo.
- Kupumzika vya kutosha
JINSI YA KUJIKINGA NA UGONJWA HUU
1. Kutumia dawa au mafuta ya kufukuza mbu
Ushauri wa kwanza kabisa ni kuepukana na mbu. Kituo cha Kudhubiti na Kuzuia Maradhi (CDC) nchini Marekani kinapendekeza watu wajipake mafuta yenye kemikali za kufukuza mbu kama vile N, N-diethyl-meta-toluamide (DEET) au picaridin.
Mafuta haya yanafaa kujipakwa mara kwa mara, kwa kufuata maagizo kwenye mikebe, au mtu anapoanza kuumwa na mbu. Mtu anafaa kujipaka baada ya kujipaka mafuta ya kukinga ngozi dhidi ya miali ya jua.
Mafuta mengi ya kufukuza mbu ni salama hata kwa kina mama waja wazito, lakini ni vyema kutafuta ushauri wa daktari kabla ya kuanza kuyatumia.
2. Kuvalia mavazi ya kufunika mwili
Wataalamu pia wanakubaliana kwamba inafaa kuvalia mavazi yanayofunika mwili vyema. Mfano shati au nguo zenye kufunika mikono na pia suruali au long’i ndefu. Mavazi yanafaa kuwa mazito kuzuia mbu kufikia ngozi.
Katika baadhi ya mataifa, mavazi huwekwa dawa maalum aina ya permethrin, ambao hufukuza mbu.
Iwapo utajipaka mafuta ya kufukuza mbu, usijipake na kisha kufunika maeneo uliyojipaka kwa nguo unazovalia.
3. Kuzuia mbu kuingia nyumbani
Ikiwezekana, wataalamu wanawashauri watu walale ndani ya nyumba zilizojengwa vyema na kuwekwa kinga ya kuzuia mbu kuingia.
Usiku, lala chini ya neti zilizotibiwa.
Lakini usitahadhari usiku pekee kwani mbu aina ya Aedes aegypti, wanaoeneza virusi hivi, hupenda sana kuuma watu mchana.
4. Chunga mimea inayokua ndani ya nyumba
Ingawa ni muhimu kuzuia mbu kuingia, ni muhimu hata haidi kuzuia mbu kuzaana. Na mbu huhitaji maji.
Watu wanashauriwa kuchunga sana maeneo yenye maji yaliyosimama kwani huko ndiko viluwiluwi wa mbu huwa. Maeneo haya ni pamoja na mikebe, maeneo ya kuwapa mifugo na wanyama wengine lishe, jagi za kuweka maua, vibanda vya kufugia ndege na mimea ya kupandwa ndani ya nyumba.
Ni vyema pia kusafisha mifereji ya maji mara kadha kila wiki, mufunika matangi ya mali na vidimbwi la sivyo kuweka dawa ya krolini (krolini huwafukuza mbu).
Maji ambayo yametulia kwa zaidi ya siku tano yanafaa kutupwa kwa kumwagwa ardhi kavu, kwani viluwiluwi wa mbu watafariki baada ya maji kukauka. Kiasi kidogo tu cha maji kinatosha kwa viluwiluwi hao kukua kwa hivyo, ni vyema kuosha na kukausha vyema maeneo hatari.
5. Kufunika taka
Maeneo ya kutupwa taka mara nyingi huwa na maji na hutumiwa sana na mbu kuzaana.
Ili kuzuia hili, ni vyema kufunika taka, hasa katika mifuko ya plastiki.
Tairi kuukuu na vitu vingine vya ujenzi pia vinafaa kuwekwa vyema, kwani sana huhifadhi maji ambayo yanaweza kutumiwa na viluwiluwi wa mbu.
This comment has been removed by the author.
ReplyDelete