Tatizo hili linajulikana kitaalamu kama hair Loss and Male pattern baldness.
NINI HUSABABISHA TATZO HILI
tatzo hili linasababishwa na vitu viwili
ambavyo ni matatizo ya hormones na kurithi kutoka kwa wazazi(kijenetiki),
Kwa wanaume hormone za kiume (androgens)
zina kazi ya kufanya mtu abalehe na kutokea kwa mabadiliko ya mwili baada ya
balehe. Mfano kukua kwa uume,mabadiliko ya sauti na ukuaji wa nywele na ndevu.
Sababu nyingine ni Lishe mbovu,Ukosefu wa
Vitamin B6 na Kuwa na stress, mfadhaiko na mshuko
wa moyo kwa muda mrefu
L
Kwa nn tatizo hili linaitwa male pattern
baldness
Tatzo hili linaitwa pattern baldness kwa
sababu mtu mwenye tatzo hili nywele zake hupukutika kwa kufata mlolongo au
mstari,kama inavyoonekana katika mchoro huo hapa chini.aina ya kwanza (type 1) ni
kiasi kidogo cha nywele kilichotoka kwa mbele.hadi kufikia stage ya tano (V) unaweza
kuona ni sehemu kubwa imepoteza nywele.
MATIBABU
Upara hauathiri afya mtu,
Umekua ukitolewa ushauri mbali mbali kuhusu
dawa za upara.lakini dawa zilizoonesha matokeo katika kutibu tatzo hili ni
mbili ambazo ni
1.minoxidil hii hufanya kazi kwa kuchochea
kuota na kukua kwa nywele.dawa hii inapakwa sehemu iliyoathirika.
2.finasteride dawa hii pia inasaidia
katika.ukuaji wa nywele.dawa hii yenyewe inakua katika mfumo wa vidonge.
Kumbuka kabla ya kutumia dawa yoyote fika
hospiali upate ushauli wa daktari.
No comments