KWA kawaida mwanaume ana korodani mbili ambazo zimehifadhiwa
katika mfuko maalum wenye tabaka tatu na ndani kuna kiasi kidogo cha
maji kinachozunguka korodani ili kuilinda. Mwanaume endapo atakuwa na
korodani moja ni tatizo na pia akiwa hana kabisa korodani ni tatizo
kubwa.
Kazi ya korodani ni kuzalisha mbegu za kiume, mwanaume
anaweza kuwa na korodani zote mbili lakini akashindwa kuzalisha mbegu za
uzazi kutokana na matatizo mbalimbali.
Mwanaume mwenye korodani
moja anaweza kuzalisha mbegu au asizalishe kabisa, kitu cha msingi
akapimwe hospitali kuona uwezo wa hiyo moja. Mwanaume ambaye hana
korodani kabisa hawezi kuzalisha mbegu za uzazi hivyo hana uwezo wa
kumpa mimba mwanamke. Tatizo la kuwa na korodani moja au kukosa kabisa
tutakuja kuliona katika makala zijazo.
JINSI TATIZO LINAVYOTOKEA
Maumivu ya korodani hutokea katika korodani au haswa moja au zote
mbili endapo zitaumizwa kwa kuumia au maambukizi. Maambukizi haya
yanaweza kuwa makali na ya muda mfupi,yanakuwa makali kwa muda fulani
halafu yanapoa yenyewe au kwa dawa baadaye yanarudi tena yakiwa makali
sana kama mwanzo au pia huwa sugu yaani unakuwa na maumivu ambayo siyo
makali ila ni ya muda mrefu na yanayokunyima raha.
Maumivu ya
korodani yanaweza kuwa makali kiasi kwamba yatahitajika matibabu ya
dharura mfano korodani inavimba kama jipu kubwa, ikiambatana na maumivu
makali na homa, tatizo hili kitaalam huitwa ‘Fournier's
gangrene' au inatamkwa ‘Fonias gangrini'.
Vilevile
inaweza kutokea korodani ikajinyonga yenyewe na kusababisha ukapata
maumivu makali ya ghafla yanayoelekea hadi tumboni, tatizo hili linaitwa
Testicular Torsion. Matatizo haya kwa ujumla wake tutakuja kuyaona katika makala zijazo.
CHANZO CHA TATIZO
Maumivu ya korodani yana vyanzo mbalimbali, lakini maumivu sugu ni
yale yanayochukua takriban zaidi ya miezi mitatu. Maumivu makali na ya
ghafla huwa hayavumiliki na huwa na tiba ya dharura. Maumivu haya sugu
huwa kwa kipindi fulani hasa kwa wanaume ambao wametoka kufunga uzazi Vesectomy
lakini baadaye hupoa. Vilevile husababishwa na maambukizi katika
korodani na kusababisha magonjwa kama Epididymits, Prostatis na Orchitis
ambayo yote ni maradhi ya viungo vya uzazi vya mwanaume na husababisha
ugumba.
Vilevile korodani inaweza kuwa na vivimbe kwa ndani,pembeni au
juu ya kokwa au kuizunguka. Uvimbe au vivimbe hivi vinaweza kuwa na
mishipa ya damu iliyojikunja humo, kujaa maji isivyo kawaida, mbegu za
kiume kujikusanya na kushindwa kutoka na mengine ya kitaalam ambayo pia
tutakuja kuyaona.
Yote haya humsababishia mwanaume ugumba.
Maumivu pia husababishwa na kuumia korodani au baada ya kufanyiwa
upasuaji kama tulivyokwishaona hapo awali.
Maumivu yatokanayo na
korodani au kende kujinyonga huwa makali sana na korodani zikiguswa
huuma sana na kawaida huendelea hivyo kwa masaa yasiyozidi sita.
Unapoona dalili kama hizo wahi kamuone daktari kwa ajiri ya uchunguzi zaidi.
Kwa
kawaida maumivu ya korodani hupanda juu zaidi na kuacha mfuko wake
mtupu. Tatizo hili huwatokea zaidi vijana chini ya umri wa miaka 25
ingawa pia inaweza kutokea katika umri zaidi ya huo.
Tatizo hili huhitaji upasuaji wa dharura.
Wakati mwingine tatizo hili hutokea kwa korodani kuwa na tabia ya
kupanda au kushuka, ikishuka mgonjwa hupata nafuu, hali huendelea
vivyohivyo kwa vipindi fulani. Hali hii inapotokea mgonjwa hutapika na
kukosa nguvu.
Maambuziki ya korodani pia mtakuja kuyaona kwa
undani baadaye lakini pia huambatana na maambukizi katika mkojo au
‘UTI' na homa. Huwa makali kwa vipindi. Kisonono na gono
huchangia tatizo hili kwa kiasi kikubwa.
Uvimbe kama jipu wa
korodani au Fonias gangrini kama tulivyoona hapo awali ni mbaya kwani
korodani inakuwa kama inaoza halafu tatizo hilo lina tabia ya kusambaa
kuelekea uvunguni jirani na njia ya haja kubwa. Uvimbe huwa kama busha
au jipu kubwa lakini ndani yake hakuna maji wala usaha.
Tatizo
hili pia tutakuja kuliona kwa undani kwani nalo huathiri wanaume wengi
na ni tatizo kubwa ambalo mwanaume yeyote ni rahisi kupata pia hupoteza
uwezo wa kuzaa.
KORODANI KUSHINDWA KUFANYA KAZI (TEST CULAR FAILURE)
Kazi ya korodani ni kuzalisha vichocheo au homoni za kiume na mbegu
za kiume. Mwanaume anatakiwa awe na korodan mbili ingawa ukiwa na moja
pia inaweza kufanya kazi kama ni nzima, inatakiwa kama unayo moja nenda
hospitali ukapimwe kuthibitisha ubora wake na uwezo wake.
Katika hali isiyo ya kawaida wapo wanaume wenye korodani tatu. Ukishakuwa na hali hii ni vema ukapimwe hospitali.
Matatizo
mengi ya korodani tumeshayaona kwa kina katika matoleo yaliyopita na
tunamalizia kuyaona leo huku tukiangalia na mada hii.
Matatizo ya
korodani kama tulivyoyaona ndiyo matokeo ya kushindwa kufaya kazi.
Korodani kushindwa kufanya kazi tunaweza kuweka katika makundi mawili,
kwanza ni hali ya uwezo wake kuwa mdogo tangu balehe Hypogonadism' na
tatizo linaweza kutokea ukubwani yaani baada ya balehe au utu uzima
secondary hyponadism.
Tatizo linapotokea katika utu uzima huambatana na upungufu wa nguvu za kiume, kusinyaa korodani na uume kuwa mfupi au mdogo.
Hii
ni kutokana na korodani kushindwa kuzalisha vichocheo au homoni za
kiume kama tatizo ni tangu balehe, basi hali ya matatizo makubwa hutokea
katika mfumo wa uzazi na mwili kwa ujumla. Hayo ni baadhi tu ya
matatizo ila mengi tutaendelea kuyaona.
CHANZO CHA TATIZO
Korodani kushindwa kufanya kazi husababishwa na matatizo mengi kama
vile matumizi ya madawa, baadhi yake ya hospitali kwa muda mrefu hasa
kwa wanaume mfano dawa za jamii ya Glucocorticoids, Ketoconazole, madawa
ya kulevya hasa bangi pamoja na mdawa ya kutibu saratatani.
Matatizo
ya kuzaliwa nayo Chromosome Problems kama klenefelter's syndrome,
magonjwa yanayoathiri korodani mfano Mumps na joto kali na la muda mrefu
katika korodan. Kuumia moja kwa moja kwa korodani Direct Injury na
kuvimba na kujinyonga kwa korodani Testicular Torsion.
Watu ambao
wapo katika hatari kubwa korodani zao kuja kushindwa kufanya kazi ni
wale ambao hufanya shughuli zinazoumiza korodani zao taratibu na kwa
muda mrefu mfano waendesha pikipiki au bodaboda katika barabara mbovu
kwa muda mrefu, huwa kitaalamu huziumiza korodani zao Constant low level
injury to the Scrotum na wale ambao wana korodani moja au hawana
kabisa.
DALILI ZA TATIZO
Endapo korodani zako zinashindwa kuzalisha mbegu za kiume utajikuta
unaishi na mke kwa zaidi ya mwaka mmoja na mnafanya tendo la ndoa kwa
lengo la kutafuta mtoto na mnakosa.
Endapo korodani zinashindwa
kuzalisha homoni za kiume basi utakuwa na dalili zifuatazo, kama ni
mtoto anakuwa harefuki anaendelea kuwa mfupi huku umri unaenda, matiti
ya mtoto wa kiume au kijana yanakuwa makubwa Gynecomastia mwili hauwi na
misuli imara, kukosa hamu ya tendo la ndoa, unakuta vinyweleo vya
kwapani na sehemu za siri havioti au kama vilishaanza kuota havikui hata
kwa zaidi ya mwaka, huoti ndevu na kubadilika kama mwanaume, uume
haukui na korodani zinasinyaa na kuwa kama za mtoto. Sauti haiwi nzito.
UCHUNGUZI
Matatizo ya viungo vya uzazi huchunguzwa katika hospitali za wilaya
na mkoa, uchunguzi wa awali hufanyika kwenye vituo vya afya.Vipimo
mbalimbali hufanyika kadiri daktari atakavyoona inafaa.
USHAURI
No comments