JE KUANGALIA PICHA A NGONO (PORN) ZINAATHIRI VIPI NGUVU ZA KIUME?

 


kuangalia picha za ngono inaweza kusababisha tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume kwani Ubongo unapokua na  mohemko kwa muda mrefu mikali huzoea mihemko hiyo na baada kutopata mihemko hiyo kabisa.

NINI HUTOKEA.
Ubongo huzalisha kemikali inayoitwa dopamine ambayo kazi yake hii inakufanya utamani au huwe na hamu na vitu vinavyouzawadia mwili mfano vyakula na tendo la ndoa. Mfano unapoona chakula ubongo unazalisha hii dopamine ili upate hamu ya kula. Vivyo hvyo unapoona mwanamke mzuri kwako inazalishwa na kukupa matamanio na kupelekea process ya uume kusimama kuanza.

Sasa picha za ngono hiathiri mfumo huu kwa kufanya ubongo kuzalisha kwa wingi sana kuliko kawaida kwa Dopamine hivo kupelekea ubongo kuzoea kiwango kikubwa hiki cha dopamine na hivo kufanya uhitaji kiwango kikubwa zaidi cha mhemko zaidi ya awali ili uume usimame,hali inayopelekea mtu kutopata mhemko wa kutosha kufanya uume kusimama vzuri akiwa na mwanamke.Hai hii humwathiri mtu kwa kumfanya kwamba ubongo uzoee tu kiwango kikubwa cha dopamine anachokipata kwa kuangalia video au picha za ngono na kufanya kiwango cha dopamine kinachosababishwa na akiwa na mwanamke kuwa kidogo kwake kusababisha mhemko au uume kusimama matokeo yake akiwa na mwanamke uume kutosimama vizuri au kutosimama kabisa.Pia anavyozidi kuangalia picha hizi na kujichua kiwango kinachosababishwa na kufanya vitu hivi nacho kinakuwa kimezoeleka na ubongo hivyo anaweza kupata tatizo la uume kutosimama kabisa hata akiwa anajichua au anaangalia picha hizi.
 Dopamine Receptors Break Down

Pia dopamine hii inavyozidi kiasi cha kawaida kwa muda mrefu inaathiri uzalishwaji wa hormone ya testosterone ambayo ni muhimu katika nguvu za kiume na  a ya tendo la ndoa hali inayokuacha na tatizo la kukosa hamu kabisa ya tendo la ndoa.

Kwa wanawake kuangalia picha hizi hupelekea pia ubongo kuzoea kiwango kikubwa cha dopamine na kusababisha mwanamke asiwe anapata raha akikutana na mwanamke au kumsababishia tatizo la kukosa hamu ya tendo la ndoa.

Unaweza kukuta mtu huyo huyo akirudia kuangalia picha au video hiyo hiyo siku inayofata hapati mhemko sana kama jana yake kwa sababu ubongo wake ushazoea kiwango kikubwa cha dopamine kilichozalishwa jana yake na video au picha hiyo anavyoendela kuiangalia inafikia hatua anapoiangalia hapati kabisa mhemko.
Kwa hiyo unaweza kuona kitu hiki kinavyoweza kuathiri uume kusimama unapokuwa na mwanamke.

Vivyo hvyo tatizo la kujichua wengi huamini kwamba linadhoofisha uume,ila ni kwamba nalo linaathiri nguvu za kiume kwa njia hii.
Pia kiwango kikubwa cha dopamine kwa muda mrefu huathiri sehemu ya ubongo inayohusika na  kufanya maamuzi mbali mbali ijulikanayo kama CINGULATE CORTEX
Kiufupi unapotaka kufanya tendo la ndoa au unapokuwa na mwanamke ubongo unazalisha dopamine hii inafanya upate mhemko,na kufanya damu nyingi kwenda kwenye mishipa ya uume na misuli ya uume kuzalisha kemikali ya nitric oxide na kufanya mishipa mikubwa (chambers) za uume kujaa damu na kufanya uume kusimama. Kwa hiyo kusimama kwa uume inategemea sana na jinsi gani ubongo umeipokea kemikali ya dopamine.

HABARI NJEMA.
Ni kwamba suluhisho la hali hii ni kuacha kuangalia picha za ngono ,au kujichua. Unapoacha kufanya hivyo mwili na ubongo huanza kuzoea kiwango cha kawaida cha Dopamine na kurudia katika hali yako ya mwanzo.

No comments