FAHAMU ZAIDI KUHUSU KUKABWA NA JINAMIZI (SLEEP PARALYSIS)

  



KUKABWA NA JINAMIZI NINI MAANAA YAKE?
Kukabwa na Jinamizi katika ndoto kama tunavyoita ni kitendo ambacho kinawatokea watu wengi sana. 
Watu wengi hufikiri kwamba anayewakaba ni Jini lakini Tendo hilo kwa kitaalamu linajulikana kama “Mwili kupooza katika usingizi” (Sleeping Paralysis)
Tendo hilo huwa linakutokea katika muda wa sekunde 20 lakini wewe unayehusika utahisi kama dakika 5 au dakika 10.

Matukio hayo ya kijinamizi yanatofautiana na yanakutokea wakati ukiwa nusu usingizini na nusu macho.
Ukweli ni kwamba hayana madhara yoyote, ila yanakupa hofu kwa muda fulani.
Unapokabwa unakuwa na fahamu nusu. Unaweza kufungua macho, na utahisi kupiga kelele lakini watu hawakusikii, Mwili wako unakuwa hauwezi kufanya lolote na viungo vya mwili wako vinakuwa havifanyi kazi,
Inapokutokea unakuwa huwezi kunyanyua mguu wala mkono wala kichwa. Kwa ujumla unakuwa kama uliyepata “ugonjwa wa Kupooza”.

Hali hii ya kukabwa inapotokea unaweza ukamuona mtu anayetisha akiingia ndani chumbani kwako, wengine wanaona kama wanatekwa nyara au kuchukuliwa, wengine wanahisi wanabakwa, wengine wanaona wakipigwa au kukimbizwa na matukio mbali mbali ya kutisha.



Hali hii hutokeaje?
Wakati unapolala kuna mabadiliko yanatokea kwenye mwili wako. Mabadiliko hayo yanakua katika hatua 2 kama ifatavyo.
A. NON RAPID EYE MOVEMENT(NREM) Hii ndo hatua ya kwanza ya usingizi inayotekea katika dakika 90 za mwanzo za usingizi hapa misuli ya mwili inalegea kiasi baada ya hatua hii misuli inabadirika kutoka katika hali ya kulegea kiasi na kubana hali inayopelekea macho kuchezacheza japo umeyafumba hatua hii ndo kitaalamu inaitwa RApid eye movement stage (REM)

B.RAPID EYE MOVEMENT (REM). Kwa ufupi naweza kusema ni hatua ya usingizi mzito.mtu anakua hajitambui.
katika hautua hii kama nlivotangulia kusema awali misuli inabana na kupelekea  macho kucheza cheza baada ya sekunde 20 misuli yote ya mwili inalegea sana na asilimia kubwa ya mifumo ya mwili inakua imepumzika.katika hatua hii ndipo mtu unapata ndoto.hapa mtu anakua hajitambui ndo maana huwezi kuhisi mabadiliko yoyote katika mwili wako.

Sasa endapo unafikia hatua ya Rapid eye movement (REM) wakati bado unajitambua ndo utahisi huwezi kujongeza mikono,miguu, wala kuongea na kuhisi kama umekabwa.

Kwa hiyo sababu yoyote inayoathiri hatua hizo za usingizi NREM kwenda REM zinaweza kusababisha hali hii ya kukabwa na jinamizi.Kitu chochote kinachokufanya ufikie hatua ya Usingizi mzito (REM) wakati bado unajitambua inasababisha upate hali hii.

VISABABISHI
kukosa usingizi
Kufululiza Kulala muda chini ya masaa 6
Kulala chali
Matatizo ya misuli kubana au maumivu ya miguu wakti wa usiku.
Msongo wa mawazo
Kulala sehemu yenye makelele
Sonona (depression)
Matumizi ya dawa mfano dawa za magonjwa ya akili, dawa zinazoathiri usingizi mfano prednisolone
Madawa ya kulevya
Mwili kuchoka sana

NIFANYE NINI NIKIWA KATIKA HALI HII
Ikikutokea hali hii jaribu kuvutabpumzi nyingi ndani kwa sababu pumzi peke yake ndo inayoweza kuidhibiti hali hii ya kukabwa

JINSI YA KUJIKINGA
Punguza stress
Pata muda wa kutosha kulala usiopungua masaa 8
We ratiba maalumu ya muda wa kulala
Unapolala hakikisha kuna utulivu epuka tabia ya kulala umewasha muziki au TV
Epuka kulala chali.
Endapo unahisi hali hii inataka kukutokea amka kaa kwa dakika 5 kisha lala.b

HALI HII HAINA MADHARA YOYOTE KIAFYA

No comments