TATIZO LA MAUMIVU YA MIGUU WAKATI WA KULALA

 



Maumivu ya miguu wakati wa usiku, kwa jina jingine yakijulikana kama maumivu yanayohusiana na kulala huwa ni maumivu yanayotokea si kwa nadra na husababisha maumivu ambayo yanasababisha mtu kukosa usingizi. Maumivu haya hutokana na kukakamaa ghafla kwa misuri, hali hii huanza ghafla na hudhuru sana misuli ya vigimbi
Sehemu hii tunazungumzia maumivu ya miguu ya aina hii tu.
Epidemiolojiaya tatizo
Maumivu ya miguu wakati wa usiku hutokea sana kwa  wagonjwa lakini haya ripotiwi na wagonjwa kwa madaktari. Kwa kawaida hutokea kwa asilimia 40 kwa watu wenye umri zaidi ya miaka 50 na hutokea sana jinsi umri unavyoendelea.Tatizo hili husababisha matatizo mengi ya kukosa usingizi.
Tatizo hili huweza kutokea kwa watoto wadogo pia lakini kwa asilimia 7 tu haswa kwenye umri wa miaka 16 hadi 18.



Visababishi
Visababishivya maumivu ya miguu mara nyingi huweza kuwa ni sababu zisizojulikana, au yanaweza kusababishwa na hali au magonjwa Fulani mtu aliyonayo.
Hali zinazoweza sababisha ni;
  • Udhaifu wa kuweka miguu katika pozi zuri
  • Madhaifu ya mishipa ya fahamu
  • Madhaifu ya kimetaboliki mwilini(yakiwemo kupungua maji mwilini, kukosekana kwa usawia wa madini na madawa mtu aliyokunywa
Watu wengi wenye maumivu ya miguu wakati wa usiku mara nyingi huwa hawana matatizo haya ya kukosekana kwa usawia wa maji au madini mwilini.
Maelezo ya Sababu zingine zinazoweza kusababisha maumivu ya miguu wakati wa usiku ni kama ifuatavyo
  • Pozi baya
Kukaa mda mrefu sana, kuweka pozi baya wakati umekaa mda mrefu bila kufanya kazi
  • Madhaifu ya mishipa ya fahamu yanaweza kusabaishwa na ugonjwa wa parkinsons, magonjwa ya misuli yasiyotokana udhaifu wa mfumo wa fahamu(mayopathi), nuropathi,radikulopathi, na magonjwa ya mishipa ya fahamu ya misuli
  • Madhaifu ya kimetaboliki yanaweza kusabaishwa na kukosekana kwa usawia wa maji na madini mwilini kwa mfano kwa sababu ya kutumia dawa za kupunguza maji mwilini kama watu wanaotumia dawa za kuongeza kukojoa, kutokwa na jasho jingi, au kufanyiwa usafishaji wa damu na mashine za dialysis.
  • Maumivu yanayotokana na ujauzito yanaweza kusababishwa na upungufu wa madini manganese ambapo mama akipata madini haya maumivu hutoweka
  • Matatzo mengine ya kimetaboliki huhushisha ugonjwa wa kisukari,kushuka kwa sukari mwilini, unywaji pombe uliobobea, kiwango kidogo cha homoni thairoidi, na magonjwa ya misuli
  • Madawa yanayoweza kusababisha maumivu ya miguu wakati wa usiku ni pamoja na dawa za kuvuta puani jamii ya Beta agonist, dawa jamii ya thiazide, spinololactone
  • Dawa zingine ni za kundi la beta agonists, beta blockers, angiotensin II receptor antagonists, benzodiazepines,teriparatite, pyrazinamide, raloxifen, donepezil, neostigmine, tolcapone, clofibrate, ciplastine, vincristine, dawa za kunywa za uzazi wa mpango 
Sababu zingine zinaweza kuwa mazoezi ambapo hutokea mtu akishamaliza kufanya mazoezi na hutokana ka kuchoka kwa misuli.
  • Magonjwa ya mishipa ya damu ya miguu, udhaifu kwenye mishipa ya vena ya miguu kwa nadra sana huambatana na maumivu ya miguu ikiwemo pamoja na upungufu wa damu mwilini, kusinyaa kwa ini, madhara ya kuacha dawa za kulevya jamii ya opioidi, na upasuaji wa kupunguza mafuta mwilini ili kupunguza uzito.
Jamii ya maumivu yanayotokea
Maumivu ya miguu wakati wa usiku huwa ya aina hii
  • Huambatana na misuli kukaza au kubana kwenye paja, kanyagio au mguu na maumivu haya hukaa sekunde chache hadi dakika kadhaa na hupungua endapo mtu atanyoosha mguu unaouma kwa lazima, kukaza misuli ya kigimbi na kunyoosha kanyagio. Baad aya maumivu hayo kutoka, yanaweza kufuatiwa na kipindi cha miguu kuwa na maumivu ya mbali kwa masaa kadhaa hasa kwenye mapaja.
  • Maumivu haya hutokea wakatimtu yupo kitandani, wagonjwa wanweza kuwa wamelala au wapo macho. Ingawa maumivu haya hutokea usiku, asilimia chache ya baadhi ya wagonjwa huweza kupata maumivu haya wakati wa mchana

Utambuzi wa tatizo(dalili)
  • Mgonjwa atachukuliwa historia ya tatizo na kufanyiwa vipimo ili kutambua ni nini kisababishi cha tatizo lake. Wakati mwingine vipimo vya maabara vinaweza kuhitajika lakini havina ulazima.
  • Uchunguzi wa miguu utafanyika pia ili kuangalia kama kuna viashiria vyovyote vile vinavyotoa sababu ya maumivu ya miguu.
Ili mgonjwa aitwe ana maumivu haya ya miguu wakati wa usiku anatakiwa awe ana vigezo vifuatavyo
  • Kuhisi maumivu kwenye mguu au kanyagio yanayotokea ghafla, na yanayotokana na kubana, kukakamaa kwa misuli bila hiari
  • Maumivu ya misuli kutokea wakati mtu amelala kitandani usiku, ingawa yanaweza kutokea akiwa amelala au akiwamacho.
  • Maumivu yanaoisha au kupungua mgonjwa anaponyoosha mguu au kanyagio
Matibabu
Matibabu ya maumivu ya ghafla. Mgonjwa anaweza kunyoosha mguu na kanyagio kwa dakika kadhaa endapo maumivu yapo kwenye misuli ya vigimbi. Aina hii ya mazoezi huweza kupunguza maumivu ya miguu kwa mda. Baadhi ya wagonjwa husimama na maumivu pia hupungua. Mgonjwa atatakiwa kusimama huku kanyagio limekaa chini ya sakafu na kuikandamiza kwa nguvu. Kwa uzoefu kuifanyisha mazoezi miguu hupunguza ukali na mda wa maumivu ya miguu.
Hatua zingine mgonjwa anaweza fanya ni
  • Kutembea, au kunyoosha juu na chini kwa kanyagio
  • Kuoga maji ya uvuguvugu ili yapite kwenye miguu. Pia mtu anaweza kuloweka miguu katika maji ya uvuguvugu kwa mda.
  • Kufanya maseji ya kutumia barafu katika eneo lenye maumivu kwa dakika kadhaa
Kuzuia kujirudia kwa maumivu ya miguu ya wakati wa usiku mtu mgonjwa anaweza kufanya mambo yafuatayo;
  • Mazoezi ya kila siku ya kunyoosha miguu, kwa mtu ambaye matibabu yasiyodawa yameshindika anaweza jaribu kutumia dawa kama quinine ingawa inaambatana na madhara. Tiba ya mazoezi ni nzuri zaidi kuliko ya dawa
Kujua kuhusu matibabu na dawa aina zingine na dozi unaweza kuongea na dr wako au tutafute kwenye mawasiliano yetu kupata tiba na madaktari wetu

No comments