Himoglobini (haemoglobin) ni molekyuli
ambayo ni sehemu ya chembe hai nyekundu zilizoko mwilini.
Himoglobini hufanya kazi ya kuzisaidia
chembe hai nyekundu kubeba hewa ya oksijenu kutoka kwenye mapafu kwenda sehemu
nyingine za mwili.
Kwa kawaida binadamu anapozaliwa huwa na
himoglobini ya kawaida ambayo huitwa himoglobini A (Haemoglobin A) au kwa
kifupi HbA na Himoglobini ya kichanga ambayo huitwa Himoglobini F (HbF).
Himoglobini A ambayo hutengeneza takriban
asilimia tisini na saba ya Himoglobini za mtu mzima imeundwa na jozi mbili za
minyororo (chains) za alfa (alpha) na beta (beta).
Chembe hai nyekundu za damu za kawaida huwa
laini,za duara na huweza kujipenyeza katika mishipa ya damu kirahisi.
Pia huweza kuishi kwa takriban siku mia
moja na ishirini (120) kabla chembe hai nyekendu za damu mpya hazijatengenezwa.
Watu wenye ugonjwa wa sickle cell wao huwa
na chembe hai nyekundu ngumu, zenye umbo la mundu au mwezi mchanga ambazo
hupita kwa shida kwenye mishipa ya damu hasa ile midogo.
Aina hii ya himoglobini huitwa Himoglobini
S (HbS).Tofauti na chembe hai nyekundu za damu za kawaida zenyewe huishi kwa
siku chache zaidi,
kwa kawaida huishi takribani siku kumi na
sita (16) tu.
Ugonjwa wa seli mundu (sickle cell) ni
ugonjwa sugu na wa kudumu.Waathirika waweza kuwa wenye afya njema lakini maisha
yao huandamwa na vipindi vya mashambulizi ya maumivu.
Umri wa kuishi hupungua na baadhi ya tafiti
za nyuma zinaonyesha kwamba waweza kuishi kwa wastani wa miaka arobaini (40)
mpaka hamsini (50).
Ugonjwa huu ni wa kawaida kwa watu wenye
asili ya kiafrika hasa walioko chini ya Jangwa la Sahara lakini waweza athiri
watu wa mataifa mengine pia.
*Namna ugonjwa unavyorithiwa*
Ugonjwa wa sickle cell waweza kurithiwa kama
ilivyo kwa makundi ya damu, rangi ya ngozi, rangi ya macho na tabia ua vitu
vingione vinavyoweza kurithiwa.
Kwa mfano kama mzazi mmoja ana himoglobini
AS, amabyo huashiria kuwepo kwa sickle cell bila kuonyesha dalili na mzazi
akiwa mzima, basi wana uwezekano wa kupata watoto wenye sickle cell ambao
hawataonyesha dalili.
Pia kama mzazi mmoja ana sickle cell na
mwingine ana sickle cell bila dalili, kuna uwezekano wa asilimia hamsini (50%)
ya kupata mtoto mwenye sickle cell au sickle cell bila dalili katika kila mimba
itakayotungwa.
Na kuna takriban asilimia ishirini na tano
(25%) ya kupata sickle cell yenye dalili katika kila mimba.
*Namna ya Ugonjwa wqseli Mundu (sickle Cell
disease) unavyotokea*
Ugonjwa wa sickle cell hutokea kutokana na
mabadiliko (mutations) katika mnyororo wa beta (beta chain) ambapo amaino asidi
(amino acid) aina ya glutameti (glutamate) huitoa amaino asidi ya Valini
(Valine) kutoka kwenye nafasi ya sita ya mnyororo wa beta.
Katika mazingira yenye kiwango kidogo cha
oksijeni, chembe hai nyekundu za damu zenye umbo la kawaida (mviringo)
huharibiwa na kupoteza uwezo wa kutanuka na kusinyaa (elasticity) zipitapo
kwenye mishipa ya damu.
Hali hii hupelekea chembe hai hizo nyekundu
za damu kuharibiwa na mfumo wa damu kwenye bandama (spleen) kwa kitaalamu
unaitwa *reticuloendothelial system.*
Pia hupelekea kuziba kwa mishipa midogo ya
damu (infarction) kutokana na chembe hai nyekundu za damu zenye umbo la mundu.
Hali hii yaweza kupelekea kukosekana kwa
damu na oksijeni ya kutosha katika baadhi ya viungo.
*Dalili za Ugonjwa wa seli mundu (sickle
cell disease)*
Ni mara chache kwa dallili za sickle cell
kuonekana katika miezi sita ya mwanzo baada ya kuzaliwa.
Hii inatokana na kuwepo kwa wingi kwa
himoglobini ya kichanga, himoglobini F, ambayo huzilinda chembe hai nyekundu za
damu zisibadilike umbo.
Ikumbukwe kwambamabadiliko ya kiumbo ya
chembe hai nyekundu za damu ndiyo chanzo cha dalili tutakazoziona hivi punde.
*Dalili za seli Mundu wakati wa utotoni*
-Maumivu ya pingili (dactylitis) za mikono
na miguu
-Kushambuliwa na maradhi kama uti wa
mgongo,
nimonia,mafua,kikohozi n.k
-Kuvimba kwa bandama/wengu (splenomegally)
kutokana na kujaa ghafla
kwa damukwenye bandama
-Kusinyaa kwa bandama(autosplenectomy)
*Dalili za seli Mundu ukubwani*
-Upungufu wa damu
-Maumivu ya tumbo
-Maumivu ya mifupa (viungo)
-Kupooza
-Maumivu ya kifua yafananayo na nimonia
(acute chest syndrome)
-Kubana kwa kifua
-Kukojoa damu
-Vidonda sugu miguuni
-Kusimama kwa uume kuambatanako na maumivu
makali (priapism)
-Kuvimba kwa paji la uso au fuvu
*Vipimo na Uchunguzi*
Vipimo vifuatavyo ni muhimu katika kugundua
sickle cell na magonjwa yaambatanayo na sickle cell
-Kipimo cha Sickling (Sickling Test)
-Kipimo cha damu kama kuna Malaria
-Kipimo cha mkojo kuchunguza uwepo wa
chembe hai nyekendu za damu katika mkojo
-Picha ya kifua (x-ray) kuangalia iwapo
kuna athari katika kifua
-Kipimo cha wingi wa damu (Hb level)
-Kipimo cha kundi la damu (Blood grouping
and cross matching)
*Matibabu*
Aina ya matibabu anayohitaji mgonjwa
hutegemeana na aina ya mgonjwa na tatizo linalomsumbua kwa wakati huo.
Ni vyema kuchukua hatua mapema iwapo una
mtoto mwenye dalili zilizotajwa hapo juu.
*Ushauri*
Ugonjwa wa Sickle cell ni ugonjwa sugu na
wa kudumu.
Watu wenye ugonjwa huu huambukizwa
kirahisi magonjwa mengine kama vile
nimonia, malaria n.k
Wagonjwa wenyewe wanatakiwa kujilinda dhidi
ya baridi, magonjwa ya kuambukiza kama nimonia, malaria, magonjwa ya mifupa n.k
Pia ni vizuri kwa mgonjwa wa nimonia kuoa
au kuolewa na mwenza ambaye hana sickle cell ili kupunguza uwezekano wa kupata
mtoto mwenye sickle cell.
Kwa wakina mama wenye sickle cell na wenye
mpango wa kubeba ujauzito ni vema wakafahamu kwamba upo uwezekano wa mtoto
kudumaa kiakili akiwa tumboni, kutoka ghafla kwa mimba na kupata kifafa cha
mimba.
Pia
ni vizuri kwa wagonjwa wa aina hii kutiwa moyo (kupewa matumaini)
Imeandaliwa na Dr.Sylivester.


No comments