Katika
makala hii nitazungumzia virutubisho ambavyo ni muhimu kwa wanaume
wanotafuta watoto, virutubisho ambavyo vinasaidia kuongeza wingi wa
mbegu za kiume, Virutubisho vinavyo saidia kuzipa uwezo mbegu za kiume
kujongea na kulifikia yai.
Katika ubora wa mbegu za kiume tunaangalia
vitu vifuatavyao
1.wing wa mbegu kwa mshindo mmoja
2.mbegu kiasi gani zinajongea ( motile)
3.maumbo ya mbegu
Baada ya kufahamu hayo tuangalie ni
virutubisho gani muhimu kwa afya nzuri na kuongeza utengenezwaji wa mbegu za
kiume
kawaida kwa kipimo cha millilita moja
inabidi kuwa na mbegu za kiume kati ya million 30hadi mill 300 hivyo ikiwa
chini ya hapo inamaana mtu.anazalisha mbegu chache na inaathiri uwezo wa
kutungisha mimba
Katika kuangalia uwezo wa mbegu
kulifikia yai tunaangalia mbegu kiasi gani zinatembea. Inapaswa angalau
asilimia 60 ya mbegu zilizolishwa ziwe znatembea ndo unaweza kutungisha mimba
Kitu cha tatu ni kuangalia mbegu kama zina
umbo sawa (morphology). Kwa kawaida mbegu ambazo znakua haziko sawa zinakua na
matatzo kwenye sehemu ya kichwa. Na kikawaida kati ya mbegu zote angalau
asilimia 30% kuendelea ya mbegu inapaswa iwe na umbo la kawaida ( normal
morphology). Ili kuweza kutungisha mimba
Je vipimo hivi vinaangali a kwa kutumia
kipimo gani?
Tunatumia kipimo kinachoitwa sperm analysis
Baada ya kufahamu hayo tuangalie sasa ni virutubisho gani muhimu ili kuongeza ubora wa mbegu za kiume.
1.Zinc
Hiki ni kirutubisho muhimu sana kwa
mwanaume kuweza kutungisha mimba. Kinasaidia yafatayo
1.kuongeza kiwango cha hormone ya
testosterone
2.kuongeza idadi ya mbegu za kiume
3.inahusika sana kutengeneza ganda au layer
inayozunguka mbegu za kiume na mkia wake
4.inahusika kuongeza uwezo wa mbegu za
kiume kutembea
vitamin c
Hizi zinasaidia yafatayo
1.kuzuia mbegu kushikana au kugandamana
hivyo kuweza kutembea vzr
2.kuongezea uwezo wa mbegu kukua na kukomaa
vzr
3.kuziongezea kasi mbegu
4.upungufu wa vitamin C mwilini hupelekea
mbegu kuwa na umbo lisilo la kawaida ( abnormal morphology)
Coenzyme Q10
Kinasaidia
yafatayo
1.kuongeza kiwango cha hormone ya
testosterone
2.kuongeza idadi ya mbegu za kiume
3.inahusika sana kutengeneza ganda au layer
inayozunguka mbegu za kiume na mkia wake
4.inahusika kuongeza uwezo wa mbegu za
kiume kutembea
Viatamin E
Hii inasaidia kuongeza idadi ya
mbegu,kukomaa, na kuongeze uwezo wa kutembea
Pia inasaidia kuiongezea mbegu uwezo wa
kupenya kuingia kwenye yai.
Inasaidia kuzikinga mbegu na radikali huru
( free radicals) zisiziharibu
6. Vitamin D
Inasaidia kutengenezwa vzuri kwa nucleus ya
mbegu za kiume.kama tunavojua hii ndo sehemu ya mbegu inayobeba DNA,pia
inaongeza idadi ya mbegu
5. Selenium (Sodium Selenate)
Hii inasaidia mbegu kukomaa, kuingeza idadi
ya mbegu na kuimarisha kuta za sehemu mbegu zinapotunzwa pindi zinapotengenezwa
( epididymis)
7. Vitamin B12 (Methylcobalamin)
Hii pia inasaidia utengenezwaji wa nucleus
ya mbegu za kiume, upungufu wa kirutubisho hiki inaweza kusababisha mapungufu
kwenye vinasaba
8. Folic Acid
Hii inasaidia kuongeza kiwango cha mbegu,
na kuziwezesha kutembea
: Hivyo ndo virutubisho muhimu kwa kuongeza
kiwango na ubora wa mbegu za kiume hivyo kuongeza uwezo kwa kutungisha mimba
9 Manganese (Sulfate)
Inaongeza idadi na uwezo wa mbegu kutembea
na kupenya kwenye yai.
Tuone sasa vyanzo.vingne vya virutubisho
hvi
VYANZO VYA VIRUTUBISHO HIVI:
1.zinc
Mbali na kuwa muhimu kwenye mbegu pia ni
nzuri kuongeza au kuimarisha mbegu za kiume.
Inapatikana kwenye
Mbegu za maboga, nyama ya ng`ombe,kuku,
maharage,spinach,uyoga,maziwa na korosho
Vitamin C
Hii utaikuta kwenye matunda kama
machungwa,chenza,papai,embe ,cabbage,peas,nanasi,pera, na pilipili
Vitamin.E
Hii utaipata kwenye
spinach,mchicha,embe,nyanya na viazi.vitamu
Na avocado
Vitamin D utaipata kwenye Maziwa,uyoga,fish
oil,mayai na mwang wa jua
Selenium
Spinach, mayai, mbegu za alizeti,nyama ya
maini,kuku na maharage
Coenzyme q 10 utaipata kwenye ufuta,mbegu
za alizeti ,dagaa, cabbage,
Folic acid utaipata kwenye avocado,papai,embe,chungwa,mahindi na nafaka
nyingine, maharage, maziwa,maini
No comments