Migraine
ni tatizo ambalo halielezeki mpaka leo nini ni kisababishi, tatizo
hili linapotokea mgonjwa hupata maumivu ya kichwa ya upande mmoja. Mara
nyingi sana, maumivu haya ya kichwa huambatana na dalili kwenye macho au
masikio zikijulikana kama viashilia au kitaalamu Aura ambazo hutokea
maranyingi kabla ya kichwa kuanza kuuma na wakati mwingine wakati wa
kichwa kuuma au baada ya kichwa kuuma.
Kipanda
uso kinatokea sana kwa wanawake na linahusianishwa sana na urithisaji-
pia tatizo hili linaelezewa kitaalamu kwamba kuna mabadiliko katika vina
saba ambayo hutokea na hivyo huweza kutokea kwenye familia fulani.
Nini husababisha maumivu haya ya migraine?
-
Zamani ilijulikana kwamba kipanda uso kinasababishwa na mabadiliko yanayotokea katika mishipa ya damu ya kichwa, inaeleza kuwa kuna wakati mishipa ya damu husinyaa kwa muda na baadae hufuatiwa na kipindi cha kutanuka kwa mishipa hiyo hivo kuleta maumivu wakati wa kitendo hiki kinapotokea. Kwa sasa kuna maelezo yajulikanayo kama neurovascular theory ambapo yanasema kwamba kipanda uso husababishwa na matatizo/mabadiliko yanayotokea katika mfumo wa fahamu na matatizo hayo yanatokana na kubadilika kwa mpitisho wa virutubisho kutoka katika mishipa ya damu kwenda kwenye chembe hai za ubongo na hivo kusababsisha michomo kwenye mishipa ya fahamu kutokana na kukosa virutubisho hivyo.
Kuhusianishwa kwa vinasaba kunaonyesha kwamba asilimia 70 ya watu wenye kipanda uso wana ndugu wa tumbo moja wenye tatizo hili na pia mambo mengi ya kimazingira husababisha kupata kipanda uso kwa mtu aliye na vihatarishi vya ugonjwa huu.
Mgonjwa wa kipanda uso anapata dalili zipi?
Dalili za kipanda uso zinapotokea au kabla hazijatokea huwa na dalili za awali au viashiria kwamba ugonjwa unatokea, viashiria hivyo vimewekwa katika makundi manne kitaalamu prodrome, aura, headache na postdrome
Prodrome
Dalili hii hutokea siku moja au mbili kabla mtu hajashikwa na kipanda uso na huwa na dalili kati ya zifuatazo
-
Choo kikumu au kukosa choo
-
Msongo wa mawazo (depression)
-
Njaa kali
-
Kutotulia kimawazo au matendo
-
Mtoto kulia sana anaposhikwa
-
Kukakamaa kwa shingo
-
Kupata miayo mingi isiyozuilika
Aura
Kipindi
hiki kinaweza kutokea kabla au baada ya kipanda uso kutokea. Aura
hutokea kutokana na maabiliko kwenye mfumo wa fahamu na huja na dalili
zinazodhuru mfumo wa hisia kama vile mtu anaweza kuona mwanga mkali
unammulika wakati hakuna mwanga, kuhisi mguso mwilini. Mabadiliko
mengine ni kwenye mgonjeo wa mwili na mfumo wa maongezi. Watu wengi
wanapata kipanda uso pasipo kupata dalili hizi au aura na dalili hizi
hutokea polepole na kuongezeka na hukaa kwa dakika 20 hai 60. Mifano ya
aura ni
Matatizo ya kuona kama kuona maumbo, mwanga mkali au miali ya mwanga inamulika machoni
-
Kupoteza uwezo wa kuona
-
Kuhisi michomo ya pini au sindano
-
Ugumu katika maongezi kama vile kushindwa kueleweka unachoongea au kutamka maneno
-
Kwa mara chache sana aura inaweza kutokea na ganzi miguuni au kupoeza fahamu kwa miguu
Kushikwa na maumivu ya kichwa ya kipanda uso
Kama
maumivu haya yasipotibiwa hukaa kwa masaa ma 4 hadi 72, lakini namna
maumivu yanavyojirudiarudia kutokea hutofauiana kati ya mtu na mtu. Mtu
mwingine anaweza kupata kipanda uso mara nyingi katika mwezi au mara
chache. Mtu akiwa anapata kipanda uso anaweza kupata mambo kati ya
yafuatayo
-
Maumivu upande mmoja au pande zote za kichwa
-
Maumivu ya kupwita,
-
Kupata shida anapokuwa kwenye mwanga
-
Kichefuchefu na kutapika
-
Kuona kwa mfifio vitu vinavyokuzunguka
-
Kizunguzungu na wakati mwingine hufuatiwa na kuzimia
Postdrome
Hiki
ni Kipindi cha mwisho, hutokea baada ya kupata kipanda uso/maumivu ya
kichwa-migraine, kipindi hichi mwathilika wa kipanda uso anaweza kuhisi
ameisha au mtupu ingawa watu wengine wanaweza kuhisi wanafuraha ya uongo
Nini huchochea tatizo la kipanda uso?
Vitu/sababu zozote zinazoweza kusabaisha maumivu ya kichwa na mambo mengi yanayoweza kuamsha ugonjwa huu kama vile
-
Mabadiliko ya vichochezi mwili-homoni kwa mwanamke. Mabadiliko ya kichochezi mwili cha estrogen huamsha kipanda uso kama inavyoonekana kwa wanawake wengi wanaopata kipanda uso, wanawake wanaopata maumivu ya kichwa ya kipanda uso huripoti kwamba wametoka au wapo kwenye kipindi cha hedhi ambapo homoni hii ya estrogeni huwa imeshuka kwa kipindi hiki. Wanawake mengine wanapata maumivu haya wakati wa ujauzito au wanawake wanapokuwa kwenye kipindi cha kukoma kwa mzunguko wa hedhi(menopause) madawa ya homoni kama madawa ya mpango wa uzazi huamsha kipanda uso ingawa baadhi ya wanawake huweza kupata nafuu wanapopata awa hizi
-
Chakula. Vyakula vilivyochacha, vyenye chumvi nyingi na vyakula vya kusindikwa huweza kuamsha kipanda uso. Kifunga au kuruka mlo kunaweza kuamsha kipanda uso pia
-
Msongo wa mawazo
-
Kulala sana au kidogo
-
Madawa ya kutanua mishipa ya damu (vasodilators)
-
Kuvuta sigara
-
Kukaa kwenye mwanga mkali
-
harufu kali kama ya pafume madawa ya meno na petroli
-
Jeraha kichwani
-
Baridi kama barafu
-
Kutofanya mazoezi
-
Kunywa wine nyekundu (red wine)
Baadhi ya vyakula vinavyosemekana kuamsha kipanda uso ni;
-
Vinywaji vyenye cafeine
-
vinywaji vyenye sukari isiyo asili kama juis kola n.k
-
matunda aina ya citrus kama machungwa ndimu n.k
-
vyakula vyenye kemikali aina ya tyramine kama cheese zilizaokaa muda mrefu n.k
-
nyama yenye kemikali ya nitrates
Matibabu ya kipanda uso
Matibabu
ya kipanda uso huwa ya aina mbili, kuondoa dalili na matibabu ya kuzuia
kupata vipindi vya maumivu ya kichwa.Kwa wagonjwa ambao wanapata
kipanda uso mara kwa mara wanatakiwa kujifunza kujizuia kutoka kwenye
mambo au vitu vinavyowasababishia kupata dalili hizo.
Mgonjwa
wa Kipanda uso anatakiwa kupimwa na kuangaliwa kama anavihatarishi vya
ugonjwa wa moyo, kama anavyo matibabu ya haraka yanatakiwa kufanyika ili
kuzuia madhara yanayoweza kutokea na ikiwa anakuwa na vipindi vya Aura
anatakiwa kupewa elimu juu ya hatari ya kupata kiharusi na wale ambao
wanavuta sigara ni vema wakaambiwa madhara ya sigara katika tatizo
walionalo
Matibabu ya dawa
-
Dawa za maumivu kama mgonjwa anapata maumivu ya kichwa
-
Dawa za kuzuia kipanda uso kutokea mara kwa mara
-
Dawa za kuondoa dalili kama kichefuchefu au kutapika
Matibabu ya kuzuia kupata kipanda uso
Mgojwa
anatakiwa ajifunze vitu/tabia gani zinazosababisha kuamka kwa kipanda
uso, endapo anamatumizi ya dawa zinazoamsha kipanda uso basi anatakiwa
kuacha
Matibabu
mengine anayoweza kupata ni yale dawa za kuzuia kupata dalili ya
maumivu ya kichwa mara anapokuwa katika kipindi cha migraine na pia kuna
dawa mgonjwa anaweza kupata kila baada ya muda flani kupita kwa ajili
ya kuzuia kupata vipindi vingi vya kipanda uso.
Madhara yatokanayo na kipanda uso
-
Maumivu sugu ya kichwa au chronic migraine
-
Kifafa
-
Kiharusi
-
Kupata Aura endelevu dakika 30 hadi 60)
Kiharusi
cha kutokana na kipanda uso ni nadra sana kutokea, lakini kinapotokea
huwa na madhara makubwa yatokanayo na kipanda uso. Katika kipindi cha
aura na maumivu ya kichwa ,mivilio ya damu huweza kutokea ndani ya
ubongo lakini vilevile ni nadra.
Vihatarishi vya kupata kiharusi kwa mtu anayepata kipanda uso ni hivi vifuatavyo
-
Maumivu ya kichwa yanayofuatiwa na kipindi cha aura
-
Kuwa na jinsia ya kike
-
Uvutaji wa sigara
-
Matumizi ya hormoni ya estrogen kama kwa wanawake wanaotumia vidonge vya majira
Kupata tiba mtafute daktari wako au wasiliana nasi
No comments