Je, husababishwa na nini?? Na mazao yapi haswa?
Je, husababishwa na nini?
– Sumu hii husababishwa na ukungu (fangasi) ambao hutokana na hali ya unyevunyevu wakati wa mazao yakiwa shambani, wakati wa kuhifadhi, usindikaji au wakati wa kusaga.
-Vyakula ambavyo hushambuliwa na sumu hii ni kama;
1. Nafaka kama vile mahindi, mtama na uwele.
2. Mbegu za mafuta kama vile karanga.
3. Mazao mengine ni kama korosho na mihogo.
– Sumu hii husababishwa na ukungu (fangasi) ambao hutokana na hali ya unyevunyevu wakati wa mazao yakiwa shambani, wakati wa kuhifadhi, usindikaji au wakati wa kusaga.
-Vyakula ambavyo hushambuliwa na sumu hii ni kama;
1. Nafaka kama vile mahindi, mtama na uwele.
2. Mbegu za mafuta kama vile karanga.
3. Mazao mengine ni kama korosho na mihogo.
Kumbuka;
Sumukuvu haiishi hata kwa kupika. Hivyo muhimu kuchukua tahadhari kuzuia sumu hii.
Dalili zake, Vipimo, Madhara na Jinsi ya kujikinga.
Dalili zake
Dalili
za ugonjwa wa sumukuvu (aflatoxicosis) kwa binadamu ni kama vile;
homa, maumivu ya tumbo, tumbo kuvimba, kutapika, kuharisha, manjano
sehemu mbalimbali za mwili, maji kujaa kwenye mapafu na degedege.
vipimo vyake je?
Ili kuthibitisha kama mtu ana ugonjwa wa sumukuvu, mgonjwa inabidi apimwe kipimo cha mkojo na/damu.
madhara
Haya hutokea baada ya ulaji wa vyakula vyenye sumukuvu kwa kiwango kikubwa. Madhara yake yanaweza kuwa ya muda mfupi au mrefu.
Madhara ya muda mfupi yanaweza kuwa;
Tumbo kujaa maji
Mapafu kujaa maji
Na wakati mwingine kupoteza maisha.
Madhara ya muda mrefu yanaweza kuwa;
-Saratani ya ini.
-Figo kushinxwa kufanya kazi.
-Kinga ya mwili kupungua
-Kudumaa kukua kwa watoto.
-Kupoteza maisha
UTAJIKINGAJE NA UGONJWA HUU?
Jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa sumukuvu;
1. Kausha mazao kikamilifu baada ya kuvuna kabla ya kuyahifadhi.
2. Fuata ushauri wa wataalam wa kilimo juu ya uhifadhi wa vyakula.
3. Usihifadhi vyakula vilivyotobolewa na wadudu.
4. Kula vyakula aina tofauti tofauti.
5. Hakikisha nafaka hazinyeshewi na mvua baada ya kuvunwa.
6. Dhibiti wadudu waharibifu wa mazao baada ya kuvunwa.
7. Unashauriwa kukoboa nafaka kama vile mahindi ili kupunguza kiasi cha sumukuvu wakati wa mlipuko.
8. Teketeza mbegu zilizoharibika au kubadilika rangi wakati na baada ya kuvuna.
9. Kwa kuwa sumu hii haiishi hata kwa kupika, epuka kabisa kutumia vyakula vyenye ukungu.
10. Ghala la kuhifadhia chakula linatakiwa liwe na mzunguko wa hewa ya kutosha.
Vuna mazao shambani mapema baada ya kukomaa kabla ya ukungu kujitokeza.
Kisha anika mazao juani kwenye turubai, mikeka au vichanja mpaka yakauke vizuri na kuyahifadhi vyema sehemu isiyokuwa na unyevu ili kuzuia fangasi au sumu aina ya aflatoxin
No comments