Tatizo hili kitaalamu linajulikana kama
post coital bleeding. Tatizo hili linawakumba wanawake hasa ambao wana matatizo
ya mvurugiko wa hormone hasa hasa hormone ya estrogen na pia wanawake
waliofikia ukomo wa hedhi.
Hali hii inaweza kuambatana na maumivu na
kwa wengine isiwe na maumivu kulingana na chanzo chake.
Ukubwa wa tatizo
Tafiti zinaonesha kwamba ni asilimia 9% ya
wanawake ambao hawajafikia ukomo wa gedhi wanapata tatizo hili na asilimia 63%
ya wanawake waliofikia ukomo wa hedhi wanakumbwa na hali hii.
VISABABISHI VYA TATIZO HILI
hali hii inaweza kutokana na sababu kama
ukavu au uke kuwa mwembamba sana hivyo kupelekea kupata michubuko wakati wa
tendo la ndoa.
Pia hali hii inaweza kuwa dalili ya tatizo
la kiafya hivyo sio ya kubeza.
Yafuatayo ni magonjwa yanayoweza
kusababisha kutoka damu wakati wa tendo la ndoa
1.MAGONJWA YA ZINAA
Magonjwa kama Kisonono na Chylamidia
yanaambata na dalili kama maumivu ya kiuno ,muwasho ukeni,Kutokwa uchafu ukeni
wenye harufu mbaya. Pia magonjwa haya hupelekea mishipa midogo ya damu iliyo
sehemu ya juu karibia na kuta za uke kuvimba hvyo kupasuka wakati wa tendo la
ndoa.
Magonjwa mengine kama kaswende,na pangusa
yanasababisha vidonda sehemu za siri vinavyoweza kupelekea maumivu na kutokwa
damu wakati wa tendo la ndoa.
VIMBE ZISIZOKUWA SARATANI
Vimbe zisizokuwa saratani kwenye shingo ya
kizazi na mji wa mimba znasababisha sana hali hii .VImbe hizi huisha zenyewe
ili zilizo kubwa sana huhitaji kuondolewa kwa upasuaji.
CERVICAL ECTROPION
hii ni tatizo la shingo ya kizazi
ambapo mishipa ya damu ya shingo ya
kizazi inakua kwa juu sana kwenye kuta za ndani za shingo ya kizazi hvyo
inakuwa rahisi mishipa hii kupasuka na kuvuja damu wakati wa tendo la ndoa.
Hali hii inawakumba sana wanawake walio
katika umri wa miaka 20 hadi 35 na wanawake wanaotumia dawa za uzazi wa mpango
na wajawazito.
MAAMBUKIZI KWENYE UKE (VAGINITIS)
Maambukizi kwenye uke mfano fangasi za
ukeni hupelekea kuta za uke kuwa laini sana na kuvimba. Hali hii inapelekea
kuwa rahisi kupata michubuko na kuvuja damu wakati wa tendo la ndoa. Tatizo
hili linaambatana na muwasho pia harufu mbaya ukeni.
SARATANI
Mojawapo ya dalili za saratani ya shingo ya
kizazi ni halii hii ya kutoka damu ukeni wakati wa tendo la ndoa. Inaweza
kuambatana na maumivu au isiwe na maumivu. Pia saratani ya kizazi inaweza
kusababisha hali hii.
Kutokwa na damu ukeni wakati wa tendo la
ndoa sio hali ya kawaida kwa wanawake ambao si bikra. Sio kitu cha kuchukulia poa kwani inaweza kuwa dalili ya tatizo katika
mwili wako. Hivyo basi unapopatwa na hali hii usikae kimya onana na daktari ili
kama kuna tatizo litibiwe mapema.
No comments