NJIA ZA UZAZI WA MPANGO,FAIDA NA HASARA ZAKE

Hakuna kitu kizuri duniani kama mtoto, kuwa na mtoto wako ni kitu kizuri sana. Ila ni muhimu sana mtoto akija wakati muafaka na muda muafaka sio inakuwa surprise… Yes kuna surprise nzuri, ila surprise ya mimba wakati una kichanga cha miezi sita, duh! Hiyo ni balaa.


Kwa nini ukumbwe na balaa wakati kuna njia rahisi ya kujipanga. Inafahamika zaidi kama nyota ya kijani, kwa ufupi ni uzazi wa mpango, hii inahusu walio kwenye ndoa na wasio kwenye ndoa, walianza kuzaa na ambao bado hawajaanza.

Lazima wote tujipange, mtoto wa kwanza aje lini, wa pili aje lini na namba ya mwisho ni ngapi? Ni rahisi ukizijua njia za uzazi wa mpango!

Njia za uzazi wa mpango ni nini??

Njia za uzazi wa mpango ni njia zinazopelekea kuchelewa, kutoa muda au kuzuia mimba. Kuna njia nyingi ambazo ni kwa wanawake na nyingine ni  kwa wanaume.
Kwa ujumla kuna njia za aina mbili, barrier methods aka vizuizi na hormonal methods.
Tofauti kubwa kati ya barrie methods na hormonal methods ni jinsi zinavyofanya kazi. Barrier methods zinazuia yai na mbegu zisikutane kabisa au kuzuia mimba isitunge bila kutumia dawa yeyote, hizi ni kama kondom, kitanzi kisicho na dawa na njia za asili kama kuhesabu siku. Njia hizi ni nzuri sana kwani hamna kemikali inayoingia mwilini wala hormons zako hazibadilishwi ili kuzuia mimba.
Njia za madawa au hormonies ni zile zinazobalidisha hormonies za mwanamke au mwanaume kuzuia mimba kutungwa au kupandikizwa na hivyo kutumia aina Fulani ya dawa. Mara nyingi huwa zinafanya kazi kwa kuudanganya mwili wako juu ya kinachoendelea au kuzuia mayai yasipevuke au kuzuia mazingira ya mimba kupandikizwa.
Kuchagua njia za kutumia ni kazi si lele mama, maana si kila njia inamfaa kila mwanamke. Mfano, mtu msahaulifusahaulifu hafai kutumia vidonge. Hapa nakupa mwangaza tu kidogo, ila ili kuamua njia nzuri itakayokufaa ni vizuri zaidi ukionana na wataalam.

Kumwaga mbegu nje


Hapa mwanaume anaotoa uume wake kutoka kwenye uke kabla ya kumwaga shahawa au kukojoa.


Uwezo wa kuzuia mimba: 72%

Uzuri

  • Haina madhara yeyote
  • Inasaidia mwanaume kuujua zaidi mwili wake na anakua mshiriki mkamilifu kwenye uzazi wa mpango.
  • Haina gharama yeyote

Ubaya

  • Ni vigumu kutambua mara zote muda wa kukojoa au kuwaga shahawa, sometimes mbegu zinapita taratibu bila mwanaume kujitambua.
  • Mwanamke hana control kabisa na njia hii hivyo basi anahitaji kumtegemea sana mwanaume kuzuia mimba.


 Njia ya kalenda aka kuhesabu siku


Hapa mnaamua kufanya mapenzi kutegemea siku za ovulation za mwanamke, kwa kutofanya mapenzi siku za hatari. Yai la mwanamke linapevuka (ovulate) kuanzia siku 10-18 tangu kuanza kwa hedhi yake.
Mahesabu yake sio magumu sana kwa mtu mwenye siku zinazoeleweka, labda mtu mzunguko wako ni siku 32 kila mwezi na haibadiliki, basi ni rahisi kuifata njia hii.
Kama siku zako hazibadilikibadiliki, unatakiwa uzigawe kwa tatu kuanzia siku ya kwanza ya period. Tukitumia huohuo mfano wa siku 32 gawanya kwa tat ni siku siku kumi kasoro mbili. So toka siku ya kwanza ya period hadi ya kumi ni safe days. Siku ya 11 hadi ya 22 ni danger (tumeziongezea zile mbili hapa, better safe than sorry) ya 23 hadi 32 ni safe pia. So unajipanga hivyohivyo kwa kuangalia mzunguko wako.
Kama siku zinabadilikabadilika unahesabu siku ya kwanza ya period hadi siku ya kumi ni safe, then siku kumi zinazofuata ni danger, then zilizobaki hadi period ijayo ni safe. Hapo unakuwa uko safe kabisa.

Uwezo wa kuzuia mimba: 76%

Uzuri

  • Mwanamke anauelewa mwili wake na mzunguko wa hedi yake 
  • Haina gharama yeyote

Ubaya

  •  Mnatakiwa muwe tayari kutofanya mapenzi zaidi ya siku kumi kwenye kila mzunguko; siku za period na zile siku za danger.
  • Uwezekano wa kunasa ni hasa kwa mwanamke mwenye period isiyotabirika au wenye mzunguko mrefu kuliko siku 32 au  mfupi kuliko siku 26.


Condom

Picture
Hii ni njia common sana kwa wapenzi wanaotaka kuzuia vitu vingi zaidi ya mimba tu, kwani ni njia pekee ya uzazi wa mpando inayokinga maambukizi ya STIs &STDs pamoja na VVU. Condom ni barrier method as inazuia mbegu kuingia ndani.

Uwezo wa kuzuia mimba: 86%

Uzuri
  • Ni njia pekee ambayo mbali na kuzuia mimba pia inazuia STIs na STDs, pamoja na VVU
Ubaya
  • Condom mpya lazima itumike kwa kila tendo

Vidonge

Picture
Vidonge huwa na dawa ambazo zina vichocheo vinavyozuia yai kutoka kwenye ovary.

Uwezo wa kuzuia mimba: 95%

Uzuri
  • Inafanya mzunguko wa period kuwa unaoeleweka (regular)
  • Inapunguza uwezekano wa kupata saratani ya ovari na kizazi, na maradhi ya shingo ya uzazi 
  • Inapunguza maumivu ya tumbo na wingi wa damu ya period na kupunguza chunusi

Ubaya
  • Lazima umeze kila siku muda ule ule, ukiwa msahaulifu unaweza kunasa wakati wowote.
  • Zinawesa kusababisha kichefuchefu, kuongezeka kwa hamu ya chakula, kunenepa au kukonda na kichwa kuuma


Sindano

Picture
Sindano huwa na dawa ambazo zina vichocheo vinavyozuia yai kutoka kwenye ovary.

Uwezo wa kuzuia mimba: 99%

Uzuri
  • Inapunguza uwezekano wa kupata saratani ya ovari na kizazi    
Ubaya
  • Usiwe mwoga wa sindano unazotakiwa kuchoma kila baada ya miezi mitatu
  • Zinawesa kusababisha kichefuchefu, kuongezeka kwa hamu ya chakula, kunenepa au kukonda na kichwa kuuma
  • Inasbabisha kuvurugika kwa period, sometimes inaweza ikapotea kabisa miezi ya mwanzo


Vijiti aka vipandikizi

Picture
Hivi ni vijiti vyembamba vidogo vinavyowekwa kwenye sehemu ya juu ya mkono wa mwanamke kwa njia ya upasuaji mdogo. Vijiti vina kichocheo kinachozuia kupevuka kwa yai.

Uwezo wa kuzuia mimba: 99%

Uzuri
  • Ukiweka unakisahau maana kinayofanya kazi kwa muda mrefu (kinazuia mimba kwa muda miaka mitatu hadi mitano tangu kupandikizwa)
  • Kinaweza kutolewa wakati wowote na mwanamke  atarudia hali yake ya kuzaa kama kawaida

Ubaya
  • Kinaitajika kuwekwa na kutolewa hospitali
  • Inaweza kusababisha uharibifu wa mzunguko wa period, mood swings, kunyonyoka kwa nywele na kuongezeka uzito
  • Inahitaji kuchanwa kidogo wakati wa kuweka au kutoa kipandikizi


Kitanzi

Picture
Hiki ni kitu kidogo kilichotengenezwa kwa aina maalumu ya plastiki ambacho huwekwa kwa utaalamu ndani ya mfuko wa uzazi. Kinaweza kufanya kazi hadi miaka 10.

Uwezo wa kuzuia mimba: 99%

Uzuri
  • Ukiweka unakisahau maana kinaweza kufanya kazi hadi miaka 10.
  • kinaweza kutolewa wakati wowote na mwanamke  atarudia hali yake ya kuzaa kama kawaida
Ubaya
  • Kinaitajika kuwekwa na kutolewa hospitali
  • Inaweza kusababisha ongezeko la damu ya period na kuumwa tumbo. 
  • Inahitajika kuangaliwa kwa mwezi mara moja kwa ajili ya kurudishiwa baada ya period.
  • Mtumiaji wa njia hii lazima awe ametulia  na partner wake awe ametulia  maana hiki kinadaka sana infections. Kama unaona hujatulia au mwenzio hajatulia tumia njia nyingine.

Kufunga kizazi

Ni upasuaji wa kuziba mirija ya kupitisha mayai (kwa mwanamke) au au ya kupita mbegu (kwa mwanaume). Kwa sababu hii njia ni permanent uwe na uhakika na uamuzi wako maana hapa ukishafanya hakuna kurudi nyuma.

Uwezo wa kuzuia mimba: 99%
Uzuri
  • Hii ndio maana inaitwa kufunga, ufunguo unakua umetupiwa baharini, yaani wewe na kuzaa basi tena.
Ubaya
  • Unafanyiwa ki-surgery kidogo, so lazima uende hospitali.
  • Ni bei ghali.
  • Ni njia ya kudumu huwezi kurudi kwenye hali yako ya kawaida ya kupata mtoto.

Emergency contraception

Hii aka ni the morning after pill. Bahati mbaya ikitokea ukajikuta umefanya la kufany a na hujatumia njia yeyote ya kujikinga na mimba. Unakuja kugutukia ushatenda tena, ufanyeje?

Hapa ndio inaingia hiyo the morning after pill. Vidonge hivi vinasaidia kujizuia na mimba vikinywewa hadi siku ya tano baadaya kufanya ngono zembe. The earlier the pill is taken the better, unavyozidi kuchalewa ndio uwezekano wa kufanya kazi unapopungua kwani vidonge hivi havitatoa mimba iliyokwishatungwa.

Pia vinatumiaka kwa watu waliobakwa, maana kwa kweli kutokana na tendo lenyewe kuwa la kikatili kuongezea kubaki na mtoto wa mbakaji ni mbaya zaidi, so vidonge hivi pia huwa vinatolewa kwa mtu aliyebakwa ili kuzuia asipate mimba ya mbakaji.

No comments