Maziwa ya mama ni bora kwa mtoto kuliko aina yoyote nyingine ya maziwa au mchanganyiko wowote wa vyakula vingine
Mwepushe mama maumivu kutokana na michubuko ya chuchu kwa kumweka katika mkao mzuri wa unyonyeshaji. Geuza mwili wote wa mtoto umwangalie mama ili shingo yake isipinde. Subiri hadi atapopanua mdomo wake. Halafu mweke kwenye ziwa. Chuchu na eneo jeusi linalozunguka linapaswa kufunikwa ndani ya mdomo wa mtoto.
Maziwa ya mwanzo ya mama ni sawa na kimiminika cha dhahabu
Maziwa ya mwanzo hutoka katika kiwango kidogo, lakini kiwango hicho ni sahihi kwa mtoto ambaye ndiyo amezaliwa. (Tumbo la mtoto ambaye ndiyo amezaliwa hubeba kiasi cha vijiko vya chai vichache tu vya maziwa kwa wakati.) Maziwa ya kwanza yananata na huonekana ya njano njano. Lakini ingawa huonekana tofauti, ndiyo chakula sahihi kwa mtoto ambaye amezaliwa . Maziwa hayo yana virutubishi muhimu vilivyotengenezwa na mwili wa mama yake kwa ajili ya kumkinga mtoto dhidi ya maambukizi . Usimwage au kupoteza maziwa ya kwanza: ni muhimu kwa mtoto kuliko dawa yoyote ile. Unyonyeshaji ndani ya siku 2 za mwanzo ni muhimu kwa sababu husaidia kufungulia maziwa yaliyokamaa ambayo mama huanza kuzalisha ndani ya siku 3 baada ya kujifungua. Kadri mtoto anavyonyonya ndivyo na wingi wa maziwa ambayo mama yake atazalisha.Je mtoto anapata maziwa ya kutosha?
Usiruhusu mtu yoyote akwambie kuwa huwezi kuzalisha maziwa ya kumtosha mtoto wako, hasa katika siku chache za mwanzo wakati mwili wako ndiyo unaanza kuzalisha maziwa.Kwa sababu ya shinikizo kutoka kwa watu wengine na kutojiamini, akina mama( au mabibi, mashangazi au wakunga ambao wanasaidia kutoa msaada) huanza kuwalisha watoto ambao ndiyo wamezaliwa au watoto wachanga maziwa ya kopo, au uji, au vyakula vingine. Vyakula hivi vya ziada ni kupoteza fedha bure na pia vinaweza kusababisha mtoto kuharisha. Kuharisha husababisha mtoto kupoteza uzito na kuwa dhaifu.Na matumizi ya vyakula hivi husababisha mama atengeneze maziwa kidogo.Hivyo, hujikuta akiamini zaidi kwamba hawezi kumlisha mtoto wake vya kutosha kwa kutumia maziwa yake pekee. Kama wewe ni mfanyakazi wa afya, unaweza kuzuia mduara huu wa matatizo makubwa ya afya kwa kuwaonyesha akinamama kuwa una imani na uwezo wao wa kuwanyonyesha watoto wao. Msaidie mama kumweka mtoto katika mkao mzuri wa kunyonya, lakini pia mpatie mama nafasi ya kujifunza yeye mwenyewe jinsi gani unyonyeshaji unamsaidia mtoto. Ongea naye vizuri, taratibu. Kuwa na subira.
Kutengeneza maziwa ya kutosha
- Nyonyesha mara kwa mara. Kadri unavyonyonyesha, ndivyo utatengeneza maziwa zaidi.
- Tumia vinywaji vya kutosha na kula zaidi. Mlishe mtoto wako kwa kujilisha mwenyewe.
- Pumzika mara kwa mara.Iwapo baba na wanafamilia wengine watasaidia na kazi zingine za nyumbani, mama atamhudumia mtoto vizuri zaidi.
Kadri unavyonyonyesha mara nyingi ndivyo utakuwa na maziwa mengi zaidi.
Watoto wengi hupoteza uzito kidogo katika wiki yao ya kwanza. Hili ni
jambo la kawaida. Lakini baada ya hapo, upunguaji uzito humaanisha
mtoto hapati lishe yakutosha. Vilevile, watoto hawakojoi sana siku yao
ya kwanza, lakini baada ya hapo wanapaswa kutoa mkojo kila baada ya saa
chache. Iwapo mtoto hatakojoa sana baada ya siku 2, atakuwa hapati
maziwa ya kutosha. Je, kama mtoto atakuwa ananyonya mara kwa mara lakini
hakojoi au kuongezeka? Katika hali kama hiyo ambayo siyo ya kawaida,
unaweza kuhitajika kutafuta maziwa mbadala. Usimpe sukari au maji ya
mchele.Usimpe maziwa mbadala ya makopo isipokuwa kama utakuwa na uhakika wa kumpatia kiasi kilichopendekezwa (kuongeza maji husababisha mtoto kuharisha na kuugua). Na usitumie chupa: hazisafishiki kwa urahisi na hivyo hueneza vijidudu ambavyo husababisha mtoto kuharisha.
Maziwa mbadala yanaweza kutolewa iwapo mama atafariki au atatengana na mtoto wake, au kwa nadra sana iwapo atakuwa kweli hatengenezi maziwa ya kutosha. Unaweza kumuomba mama mwingine kumnyonyesha mtoto huyu. Lakini kwanza apate kipimo cha virusi vya UKIMWI kujua iwapo yu salama. Hii ni kwa sababu virusi vya UKIMWI vinaweza kuenezwa kwa mtoto kupitia unyonyeshaji. Njia nyingine ni kutumia maziwa ya wanyama, mfano maziwa ya ngo’mbe au mbuzi yakiandaliwa kama ifuatavyo:
Changanya:
Kipimo 2 vya maziwa ya ngo’mbe au mbuzi | |
Kipimo 1 cha maji | |
Kijiko 1 kikubwa cha sukari |
AU
|
AU
|
Kukamua ziwa kwa mkono
- Nawa mikono yako vizuri na kusafisha chombo cka kukamulia.
- Kamata ziwa kwa vidole vyako na
dole gumba likiwa pembeni mwa eneo jeusi linalozunguka chuchu.
Kandamizia ziwa kwenye kifua chako. Halafu bonyeza vidole vyako pamoja
ukiwa unalekea kwenye chuchu. Jisikie huru na fikiria kuhusu mtoto wako
wakati unakamua maziwa hayo-hii itasaidia maziwa kutoka kwa urahisi
Maziwa ya mama yatabaki salama kwa saa 8 kama hakutakuwa na hali ya joto kali nje.
Maambukizi ya Fangasi/kuvu mdomoni
Tumia kitambaa kidogo kisafi kusambaza dawa ndani ya mdomo wa mtoto.
Jaribu kusuza chuchu na siki (vinegar), na baadaye kwa maji ya kawaida. Au kama huna siki, jitahidi tu kusafisha na kukausha chuchu yako kila baada ya kunyonyesha. Iwapo hii haitasaidia, paka dawa ya Jiivi kidogo kwenye chuchu mara 2 kwa siku 3. Pia paka Jiivi ndani ya mdomo wa mtoto mara moja kwa siku. (Kila kitu kitageuka kuwa na rangi ya zambarau lakini ni salama). Kama Jiivi haitasaidia, mpe mtoto dawa ya nistatini (nystatin).
Kama maambukizi ya kuvu yatakuwa yanapotea na kurudi, mtoto anaweza kuwa na tatizo lingine ambalo linadhoofisha kinga yake ya kupambana na maambukizi. Kwa mfano, watoto wachanga wenye VVU wanaweza kupatwa na kuvu mdomoni mara nyingi zaidi.
Maumivu ya ziwa, uvimbe, kuziba, au maambukizi
Dalili
- Eneo lenye moto, wekundu na gumu kwenye ziwa
- Maumivu katika ziwa wakati wa kunyonyesha
Matibabu
- Pumzika. Tumia vinywaji kwa wingi.
- Nyonyesha angalau kila baada ya saa 2. Unyonyeshaji hata kama ziwa lina maambukizi ni salama kwa mtoto na ndiyo njia pekee ya kuyaondoa maambukizi.
Gandamiza kwa kwenda chini
ili kukanda eneo lililoziba
ili kukanda eneo lililoziba
- Hakikisha upo katika mkao mzuri wa kunyonyesha. Mwili mzima wa mtoto lazima umwangalie mama yake. Mdomo wa mtoto unapaswa kufunguka sana, na chuchu ingizwe ndani ya mdomo wake.
- Nyonyesha upande unaouma kwanza, na uruhusu mtoto kumaliza maziwa yote kwenye ziwa.
- Kukanda polepole kwa kutumia kitambaa kisafi na maji ya vuguvugu, au kuoga maji ya moto vinaweza kusaidia.
Kama kuna homa, mpeleke kituo cha afya ili apate vipimo na matibabu.
VVU na unyonyeshaji
Wanawake wajawazito wenye VVU wanaweza kutumia dawa na kubaki wenye afya, na pia kuzuia watoto wao wasipate maambukizi ya virusi VVU. Ili kuwalinda wanawake na watoto, kila mwanamke mjamzito anapaswa kupata kipimo cha VVU. Na iwapo atakuwa na VVU, anapaswa kupewa dawa za VVU na kwa muda wote atakapokuwa ananyonyesha, hali ambayo itamlinda mtoto wake asipate maambukizi ya VVU na pia kwa manufaa ya afya ya mama mwenyewe. Angalia VVU na UKIMWI (kinaadaliwa).Je, ni salama kunyonyesha iwapo una VVU?
Dawa za VVU zikitumiwa na mama na mtoto huzuia watoto wachanga kupata maambukizi ya VVU wakati wa unyonyeshaji. Mtoto lazima apewe dawa hizo kila siku angalau kwa wiki 6. Kama mama yake hakupata dawa za VVU kwa kipindi chote cha ujauzito, mtoto apewe dawa angalau kwa wiki 12. Kama mama hatumii dawa za VVU, mpe mtoto dawa hadi wiki 1 baada ya kuachishwa ziwa. Afya ya mtoto hulindwa pia kwa kumpatia maziwa ya mama tu kwa miezi 6 ya kwanza( au hadi atakapoota meno yake ya kwanza). Kumpa mtoto uji na vinywaji vingine kabla ya kufikisha miezi 6 siyo vizuri kwa afya ya mtoto na kunaweza kuongeza hatari ya kupata maambukizi ya VVU.
Dawa za VVU kwa mama na mtoto zitawasaidia wote wawili kuwa na afya.
Bila dawa za VVU, kuna hatari ya maambukizi kupitia unyonyeshaji.
Lakini hatari kutokana na kumlisha mtoto vyakula mbadala ni kubwa zaidi.
Akina mama wengi wenye VVU hawana maji safi na salama, nishati ya
kupikia, au fedha za kununua,kutayarisha na kumlisha mtoto kwa usalama
vyakula hivyo mbadala. Watoto wao wana uwezekano mkubwa wakupatwa na
utapiamlo, na ugonjwa wa kuhara, na wanaweza kupoteza maisha. Hii
inamaanisha kuwa maziwa ya mama ndiyo salama zaidi – hata kama mama au
mtoto atakuwa hatumii dawa za VVU.
Kwa watoto na akina mama sehemu zote, ziwa ndiyo bora zaidi
Unyonyeshaji
- Gharama yake ni nafuu. Hakuna haja ya kununua vyakula mbadala, chupa, au chochote kingine.
- Husaidia kusimamisha utokaji damu baada ya mama kujifungua.
- Husaidia kuzuia mimba miezi inayofuatia kujifugua.
- Huwalinda akina mama dhidi ya saratani na matatizo ya mifupa baadaye katika maisha yao.
- Maziwa ya mama yanakuwa ndiyo yametengenezwa, yakiwa na vuguvugu, na tayari kutumika.
- Yana virutubishi vyote ambavyo mtoto anahitaji.
- Husaidia kuwakinga watoto dhidi ya kuhara, kichomi (nimonia) na magonjwa mengine.
- Ni kinga inayodumu muda mrefu dhidi ya ugonjwa wa kisukari, mzio na saratani mbalimbali katika maisha ya mtoto ya baadaye.
- Humweka mtoto salama na mwenye joto la kutosha akiwa pembeni mwa mama yake.
- Humfanya mama na mtoto wake kuwa karibu zaidi.
No comments