Watoto wachanga wanaonyonya maziwa ya mama wengi hawapati tatizo
la gesi kwa wingi kama watoto wanaokunywa maziwa ya kopo (baby formula)
,sababu mtoto anaponyoya kwa chupa anaingiza hewa tumboni kwa wingi na
inakuja kumuumiza tumbo. Ila mtoto anaenyonya ziwa la mama ni kiasi
kidogo cha hewa kinachoingia tumboni.
Watoto wanatakiwa wasaidiwe kubeuwa baada ya kunyonyeshwa. Inamsaidia
:Kutoa gesi baada ya kunyonya
:Kumwepusha na maumivu ya tumbo
:Kumwepusha kucheuwa na macheuwo kupitia puani
Mtoto anapomaliza kunyonyeshwa mweke begani ,mpige pige mgongoni
taratibu kwa dakika chache mpaka umsikie amebeuwa. Epuka kumlaza
kabla haja beuwa – kucheuwa baada ya kumnyonyesha sababu akicheuwa
yatapitia puani na kumfanya ashindwe kupumua na kupata maumivu makali.
No comments