hili ni ongezeko la presha ya macho, kimsingi macho hua yana presha ya 10mmhg mpaka 21mmhg lakini inapozidi hapo mgonjwa hutambulika kama mgonjwa wa presha ya macho.
mara nyingi ugonjwa huu hurithiwa na hauonyeshi dalili zozote mpaka baadae sana mtu anapokua mtu mzima.
ugonjwa huu huathiri mishipa ya fahamu inayohusika na kuona kitaalamu kama optic nerve na mgonjwa asipokua makini na matibabu yake basi huweza kupata upofu wa moja kwa moja na asione tena.
nini chanzo cha presha ya macho?
kitaalamu upande wa mbele ya jicho kuna maji maji kitaalamu tunaita aquous homour ambayo kazi yake ni kuleta virutubisho kwenye sehemu za jicho kama iris, lenzi na cornea pia kuondoa mabaki ya matumizi ya virutubisho hivyo lakini pia hutunza shepu ya jicho sasa maji maji haya yanapozidi ndio presha ya macho inapanda.
kwa kawaida hali hii hurithiwa kutoka kwenye kizazi kimoja mpaka kingine na sababu zingine zinazoweza kuongeza presha hii ni magonjwa ya macho, kuumia jicho kwa kupigwa na kitu au kumwagikiwa na kemikali au baada ya upasuaji wa macho wa kutibu tatizo lingine la macho.
watu gani wako kwenye hatari ya kuugua ugonjwa huu?
- watu ambao ukoo wao una wagonjwa wa hivyo
- watu wenye kisukari
- watu wenye umri zaidi ya miaka 40
- watu walioumia macho
- watu wanaotumia dawa fulani fulani kama predinisolone
- watu waliopata ajali na kuumia macho
- watu wasioona vizuri
dalili za ugonjwa huu ni zipi?
mara nyingi ugonjwa huu dalili zake haziji moja kwa moja na huja kwa
kujificha sana bila muhusika kujua na kuja kugunduliwa kwenye hatua
mbaya kabisa. moja ya dalili ni
- kushindwa kuona mbali na pembeni
- kua na macho mekundu
- maumivu makali ya macho
- kichefuchefu na kutapika
- kuona kama mawingu mawingu
je inagunduliwa vipi hospitali?
daktari atatumia vipimo maalumu kupima presha yako ya macho kisha
atapima kuangalia kama mishipa ya fahamu inayohusika na kuona
imeathirika kiasi gani...kipimo cha tenometry hutumika kupima presha ya
macho.
matibabu yakoje?
hakuna dawa ya kutibu ugonjwa huu kabisa lakini kuna dawa za kutumia kwa
muda wote wa maisha yako ambazo zitakua zinapunguza presha ya macho
yako yaani zile za matone mfano timolol lakini pia wakati mwingine kuna
aina za upasuaji hufanyika kuweka matundu kwenye iris ili kuachia maji
haya kupita na kupunguza presha.
je unaweza kuzuia ugonjwa huu?
huwezi kuzuia ugonjwa huu lakini unaweza kuzuia upofu kwa kuanza
matibabu mapema na kuyafuatilia matibabu kwa umakini. kama kwenye ukoo
wenu kuna ugonjwa huu na uko zaidi ya miaka 40 fanya vipimo kila baada
ya mwaka mmoja au miwili lakini pia kama una kisukari pia fanya hivyo
No comments