PUMU
/asthma ni ugonjwa sugu ambao huathiri njia ya hewa ambazo huingia na
kutoa hewa katika mapafu. Upatapo ugonjwa wa pumu, kuta za ndani za njia
ya hewa huvimba na hivyo kupunguza kiasi cha hewa kinachoingia na
kutoka kwenye mapafu.
Hali hii
husababisha muathirika kutoa mlio kama wa filimbi au mluzi wakati wa kupumua, kifua
kubana, kushindwa kupumua vizuri na kukohoa. Watu wenye pumu hupatwa na dalili
hizi mara nyingi nyakati za usiku na asubuhi sana.
Kulingana
na takwimu za hivi karibuni, huathiri watu milioni 300 duniani kote na
zaidi
ya milioni 22 wakiwa Marekani peke yake.
Ingawa
ugonjwa huu huathiri watu wa rika zote, lakini mara nyingi huanza utotoni,
huathiri
watoto milioni 6 nchini Marekani. Ugonjwa wa pumu huua watu 255,000
duniani
kote kila mwaka.
AINA ZA
PUMU
PUMU YA
UTOTONI (Child-Onset Asthma)
Hii ni
aina ya pumu inayotokea baada ya mtoto kuwa kwenye vizio kama vumbi la
wadudu
mfano mende, manyoya ya wanyama wa kufugwa kama paka na mbwa. Pumu hii hutokea
kwa kuwa mwili wa mtoto hutengeneza kingamwili (Antibodies) za IgE
zinazosababisha pumu. Ugonjwa wa pumu ni ugonjwa sugu uliopo sana kwa watoto
waliozaliwa na uzito mdogo, wenye asili ya kiafrika, walio katika mazingira ya
moshi pia waliolelewa latika mazingira ya dhiki/umaskini.
Watoto
wengi huanza kuonyesha dalili wakikaribia miaka mitano. Huanza kama
ugonjwa
wa njia ya hewa kama mafua na kikohozi. Watoto wa kiume wana hatari zaidi ya kupata
pumu ikilinganishwa na watoto wa kike, ila hali hii huwa kinyume kipindi cha utu
uzima.
Watafiti
wanafikiri hali hizi huwapata watoto wa kiume zaidi kwa kuwa na njia za
hewa
nyembamba zaidi ikilinganishwa na njia za hewa za watoto wa kike. Hali hii hupelekea
watoto wa kiume kuwa kwenye hatari zaidi wanapopatwa na maambukizi ya virusi
mfano mafua.
PUMU YA
UKUBWANI (Adult-Onset Asthma)
Pumu
hii huanza baada ya kufika miaka 20. Pumu hii huathiri sana wanawake kuliko
wanaume
na pia haitokei sana kama pumu ya utotoni. Vizio pia husababisha aina hii ya pumu.
Inakadiriwa kuwa 50% ya pumu ya ukubwani husababishwa na vizio na aina hii
ya pumu
huitwa pumu ya ukubwani ya vizio ( Allergic adult-onset asthma). Na 50% haisababishwi
na vizio (Allergens) nayo hujulikana kama pumu ya ukubwani isiyosababishwa na
vizio (Non-allergic adult-onset asthma/Intrinsic asthma).
PUMU
ITOKANAYO NA MAZOEZI (Exercise-
induced
asthma)
Ikiwa
utakohoa na kukosa pumzi wakati wa mazoezi au baada ya mazoezi, inawezekana una
pumu inayosababishwa na mazoezi. Ingawa kama sio mtu wa michezo kukimbia kwa
kasi kwa angalau dakika 10 kunaweza kusanabisha kukosa pumzi na kukohoa. Ikiwa
utakohoa na kukosa pumzi kwa muda mrefu basi hii itaonyesha una pumu inayosababishwa
na michezo.
PUMU
ITOKANAYO NA KUKOHOA (Cough-
Induced
Asthma) Ni aina ngumu ya pumu kwa daktari kuweza kuigundua. Kwenye pumu hii inawezekana
zisitokee dalili zingine zaidi ya kukohoa. Madaktari hulazimika kuchunguza sababu
zingine za kukohoa sana na kuhakikisha sio zinazosababisha kukohoa huko.
PUMU
ITOKANAYO NA KAZI (Occupational
Asthma)
Aina
hii ya pumu humtokea mtu akiwa mahali pake pa kazi. Huwatokea sana watumishi wa
viwandani ambapo kuna kemikali, moshi na gesi (Nitrogen oxide) zinazoweza
kuamsha pumu.
PUMU YA USIKU (Nocturnal Asthma)
Pumu
hii hutokea kati ya saa 6 usiku na saa 2 asubuhi. Pumu hii huamshwa na vumbi, halufu
kali kama za rangi ya nyumba na halufu ya vinyesi vya wanyama wa kufugwa. Mara
nyingi wagonjwa hushtuka usingizini wakati wa usiku wa maanani baada ya kukosa
pumzi.
PUMU KALI/PUMU ISIYOKUBALI STEROIDI
(Severe
Asthma/Steroidal-Resistant Asthma)
Wakati
wagonjwa wengi wa pumu hupata nafuu baada ya matumizi ya steroidi, wachache
hawapati nafuu. Hivyo wagonjwa hawa huhitaji matababu bora zaidi ya matibabu ya
kawaida.
NINI
HUSABABISHA PUMU?
Visababishi
vya pumu havijulikani waziwazi, ingawa vitu vinavyoongeza hatari ya kupata pumu
ni vizio mfano moshi, harufu, gesi na kemikali. Kila mgonjwa wa pumu ana mzio.
Zaidi ya 25% ya watu hupatwa na mafua yasababishwayo na mzio (Hay
fever/Allergic rhinitis) na kuwashwa macho (Allergic conjuctivitis) pia
wanaweza kupata pumu. Mzio unaweza sababishwa na kingamwili
(Antibodies)
zilizo ndani ya damu zinazopelekea njia ya hewa kuvimba na kusababisha pumu.
Vizio
vinasababisha sana pumu ni kama moshi, vumbi kutoka kwenye manyoya ya wanyama
kama paka na mbwa, wadudu kama mende na halufu kali kama za manukato.
Moshi
wa sigara unahusishwa sana na hatari ya kupata pumu pia hatari zaidi ya kufa
kwa pumu. Watoto wa wazazi wanaovuta sigara wapo katika hatari ya kupata pumu.
Pia watu wazima wanaovuta sigara wapo katika hatari ya kupata pumu. Sababu
zingine za kimazingira kama halufu (Marashi) inayosababishwa na vitu vya kusafishia
nyumba pamoja na rangi za nyumba, hewa itokanayo na majiko ya gesi (Nitrogen
oxide).
Uchafuzi
wa mazingira kutokana na gesi (Sulfur dioxide, Nitrogen oxide) pia mazingira ya
baridi huamsha ugonjwa wa pumu. Vitu hivi husababisha njia za hewa kusinyaa na
kusababisha matatizo ya kupumua. Watu wazima wenye uzito unaozidi kimo chao
yaani wenye Body Mass Index (BMI) kati ya 25 na 30 wanaweza kupata pumu kwa 38%
ikilinganishwa na watu wazima wenye uzito wa kawaida. Watu wanene zaidi wenye
BMI ya 30 au zaidi wapo katika hatari mara mbili.
Watoto
waliozaliwa kwa njia ya upasuaji wana hatari ya kupata pumu kwa 20% ikilinganishwa
na watoto waliozaliwa kwa njia ya kawaida. Pia wajawazito wanaovuta sigara
hupunguza utendaji wa mfumo wa hewa wa mtoto aliye tumboni hivyo huongeza
hatari ya mtoto kupata pumu. Utafiti umeonyesha pia mtoto aliyezaliwa na uzito
mdogo yupo kwenye hatari ya kupata pumu pia.
Watu walio na msongo wa mawazo (Stress) wapo katika hatari kubwa ya kupata pumu kwa kuwa watu wengi wenye msongo wa mawazo hujaribu kujituliza kwa kutumia vileo na kuvuta tumbaku hivyo kuongeza uwezekano wa kupata pumu. Ingawa utafiti wa hivi karibuni umegundua mfumo wa kingamwili hubadirika kutokana na msongo wa mawazo (Stress) kitu kinachoweza kusababisha kutengenezwa kwa kingamwili (Antibodies) za igE zinazosababisha pumu.
Chembe
za urithi pia huhusianishwa na ugonjwa wa pumu. Kuna chembe za urithi 100
zinazohusianishwa na pumu. Uwezekano wa kupata pumu kutokana na
lurithi
kwa wazazi ni 3 ya 5. Taasisi za kudhibiti magonjwa ya Marekani (The Centers
for Disease Control USA) zinasema kuwa na wazazi wenye pumu huongeza hatari ya
mtoto kupata pumu pia mara 3 hadi 6.
Tatizo
la ngozi linalosababishwa na mzio/ allergy (Eczema/Atopic dermatitis). Watoto 40%
hadi 50% wenye tatizo hili hupatwa na pumu na inawezekana wenye tatizo hili hubanwa
na pumu ya mara kwa mara.
DALILI
ZA PUMU
Sio
watu wote wenye pumu huwa na dalili hizi. Vilevile kuwa na dalili hizi
hakumaanishi una ugonjwa wa pumu.
Kukohoa.
Kikohozi
kinachotokana na pumu huwa kinakuwa kikali sana hasa wakati wa usiku au asubuhi
sana.
Kutoa sauti kama filimbi au mluzi wakati wa kupumua.
Kubanwa kifua.
Mgonjwa
huhisi kama kifua kinabanwa na kitu au kuna kitu kizito kimewekwa juu ya kifua.
Kupungukiwa na pumzi. Wagonjwa wenye pumu huhisi pumzi imekosekana,
zaidi
inakuwa ni ngumu kutoa pumzi kutoka katika mapafu.
JINSI
YA KUTIBU & KUDHIBITI PUMU
Pumu ni
ugonjwa sugu usiotibika ila unaweza kudhinitiwa. Ili kudhibiti ugonjwa huu,
uhusiano mzuri kati ya mgonjwa na daktari unahitajika sana. Ili kudhibiti
yafuatayo huhusishwa :-
=>
Kuzuia dalili hatari kama kukohoa na kupungukiwa na pumzi.
=>
Kupunguza uhitaji wa dawa za kutuliza maumivu haraka kama Aspirin
=>
Kufanya kazi kwa kiasi na kulala vizuri wakati wa usiku.










No comments