Jinsi ya kuzuia mafua kwa watoto

Mafua ni moja ya magonjwa ya mfumo wa hewa ambayo mara kwa mara huwapata watoto wa chini mitano. Mafua huweza kuwapa watoto mara 5-10 kwa mwaka mmoja.


Watoto wa chini ya mwaka mmoja wakiwa na mafua huwa katika hali ngumu kwani kushikwa kunyonya vizuri. Wazazi huwa na hofu sana pale wanapoona watoto wanapokuwa  katika hali ya mafua na kikohozi.
Kama hatua ya haraka hazitachukuliwa mwanzoni hapo baadae huwa ni makaribisho mazuri kwa ugonjwa hatari wa homa ya mapafu maarufu kama Nimonia.
Si kila kikohozi au mafua yanahitaji kupewa dawa na si sahihi kujinunulia dawa au kuandikiwa na mtu asiye daktari. Hatari ya kutumia kiholela dawa zake ni pamoja na kujitokeza kwa usugu wa bakteria dhidi ya dawa, kushusha kinga ya mwili na kuharisha.

Zaidi ya asilimia 80 ya mafua ya kawaida husababishwa na virusi ambavyo hakuna dawa ya kuwauwa. Hupona yenyewe ndani ya wiki moja. Virusi hawa ambao hushambulia tando laini za mifereji ya pua na kooni.
Mara zingine virusi wa mafua huweza kuenea katika mfumo mzima na kuenea katika mirija ya hewa kusababisha shambulizi la mirija ya hewa. Inaweza kushambulia tishu za mapafu na kusababisha homa ya mapafu. Ugonjwa unaongoza kusababisha vifo vya watoto chini ya miaka mitono duniani.
Mafua pia husababishwa na mzio, kuvuta hewa chafu yenye vumbi, moshi inayokereketa kama wenye kemikali za sumu na hali ya hewa ya baridi na unyevu. Dalili za mafua na kikohozi kisichozidi wiki mbili, mikoromo wakati ya kupumua, kupiga chafya, pua kuchuruzika maji maji au kamasi.

Kamasi ikiwa haina rangi, yaani hali ya umajimaji inakuwa imesababishwa na virusi wakati ikiwa ya njano au kijani inakuwa imesababishwa na bakteria. Dalili zingine ni joto la mwili kupanda, kushindwa kunyonya na kupumua vizuri, kulia na kutokuwa mtulivu.

Watoto wanaonyonya waendelee kunyonyeshwa kipindi chote cha ugonjwa kwani maziwa ya mama kiasilia huwa na lishe yenye kinga inayomlinda dhidi ya magonjwa. Mtoto ambaye ameanza kutumia chakula cha kawaida ni vyema ukatumia vitu kama chai na ukaidondoshea matone ya limao au machungwa.
Machungwa, limao na ndimu huwa na vitamin C inayosaidia kufupisha dalili za mafua. Hakikisha pia unampatia maji ya kunywa ua kutosha yasiyo baridi kwa ajili ya kuurudishia maji mwili. Ni vyema kutumia maji ya moto kumuogesha na kumkinga na baridi kwa kumvisha nguo zakutanda mwili mzima.

Msafishe na kitambaa safi kisichopukutisha pamba au nyuzi, kufuta mafua yanayochuruzika na kuondoa taka zilizoganda puani

No comments