Kama una
vidonda vya tumbo, matibabu
yako
yatategemea sababu ya vidonda vya
tumbo. Kama
ni bakteria H.pylori, dawa za
kuua na
kuondoa bakteria hutumiwa.
Kama ni
Non-Steroidal Anti-Inflamantory
Drugs
'NSAIDS' mfano Aspirin & Ibuprofen
utapaswa
kutumia Proton Pump Inhibitor
'PPI' mfano
Omeprazole & Esomeprazole.
Ingawa
matibabu ya siku hizi husisitiza
kuchanganya
dawa za kuua bakteria na
Proton Pump
Inihibitors 'PPI'.
Mambo
yafuatayo yatakusaidia kuishi vizuri
ukiwa na
'Vidonda Vya Tumbo':-
1.
Acha kutumia kahawa na chai, kwa
maana vitu
hivi huongeza kiwango cha
asidi
kinachotengenezwa na tumbo lako.
Unaweza
tumia chai ya mitishamba 'Herbal
tea' kama
mbadala.
2.
Kunywa maziwa na ule vitokanavyo na
maziwa kama
maziwa mgando 'Yoghurt',
jibini
'Cheese'. Maziwa hufikiriwa kufunika
utumbo na
kupunguza athari za asidi ya
tumboni.
3.
Jitahidi kupunguza uzito kama uzito
umezidi na
hauendani na kimo chako.
4.
Kula walau kidogo mara kwa mara. Hii
itasaidia
kupunguza athari za asidi
inayotengenezwa
na tumbo.
5.
Acha au kunywa vileo siku maalumu tu
kwa maana
unywaji wa pombe mara kwa
mara
hutonesha kwenye vidonda vya
tumbo
vinavyotaka kupona.
6.
Epuka matumizi ya viungo vya vyakula
kwa maana
hufanya hali kuwa mbaya zaidi.
7.
Acha kuvuta sigara/tumbaku/bangi.
Uvutaji wa
sigara utakuweka kwenye hatari
zaidi ya
kuanza vidonda vipya na kuzuia
vidonda
vingine visipone


No comments