Matatizo ya kijinsia
ni mengi baadhi tunaweza kuyakabili kwa urahisi, na kuna mengine
yanahitaji utaalamu maalumu kuyapatia tiba. Wakati mwingine maradhi husika huwa
na taathira kutokana na mtu…. Na
tutazungumzia moja ya maradhi maarufu ya kijinsia… tutazungumzia tatizo la
wanaume kuwahi kumwaga(PREMATURE EJACULATION).
Premature Ejaculation ni hali ya mwanaume kuwahi kufika kileleni ndani ya sekunde 30 hadi dakika nne baada ya kuanza tendo.
Kwa mujibu wa Shirika
la Afya Duniani, tatizo la kuwahi kumwaga (Premature Ejaculation) ni miongoni
mwa matatizo ya kijinsia yaliyoenea sana kwa wanaume, na ni mzigo mkubwa wa
kisaikolojia kwa mume. Aidha, tatizo hilo humfanya mwanamke akanganyikiwe na
hata kumfanya asiwe na hamu kubwa ya kushiriki tendo au kulikimbia tendo la
ndoa kwa hofu ya kutotoshelezwa.
Tafiti zinaonesha kuwa
asilimia kubwa ya vijana wapya katika ndoa hukabiliwa na tatizo la kumwaga
mapema, na huwenda tatizo hilo likaendelea kwa miaka mingi.
Tatizo hili ambalo
hujitokeza dakika moja kabla ya mwanaume kumuingilia mwanamke au dakika moja
baada ya kumuingilia, humfanya mwanaume asiwe na uwezo wa kuchelewa kumwaga.
Maradhi haya hutokana
na taathira hasi za kisaikolojia na kijamii kwa mwanaume husika, kama vile
wasiwasi na mkanganyiko, na linaweza kumfanya akimbie kushiriki tendo la ndoa.
Kwa mujibu wa tafiti
na ripoti mbalimbali, maradhi haya ndiyo maradhi yaliyoenea zaidi miongoni mwa
maradhi ya udhaifu wa kiume, ambapo inakadiriwa kuwa asilimia 39 ya wanaume
wenye umri kati ya miaka 18 na 64 wanasumbuliwa nao. Tofauti na maradhi mengine
ya udhaifu wa kijinsia (kama vile tatizo la kusimamisha), tatizo hili halina
uhusiano na umri wa mhusika.
SABABU ZAKE
Kuna sababu nyingi
zinazosababisha tatizo hilo. Kuna sababu za kurithi, sababu za kimwili na
sababu za kisaikolojia. Miongoni mwa sababu za kimwili ni pamoja na kutokea kwa
kasoro katika homoni muhimu ya kiume ijulikanayo kama “testosterone”, au athari
za matumizi ya baadhi ya dawa, kama vile dawa za kupunguza shinikizo la damu,
au kutokana na kuacha matumizi ya dawa za matatizo ya kisaikolojia na kiakili.
Na huwenda sababu ikawa ni ongezeko la utoaji wa tezi thioridi (asilimia 50 ya
wanaume wenye kusumbuliwa na tezi thioridi wanasumbuliwa na tatizo la kuwahi
kumwaga), au kibofu sugu (asilimia 77 ya wanaume wenye tatizo la kibofu sugu
wanasumbuliwa na tatizo la kuwahi kumwaga).
Miongoni mwa sababu za
kisaikolojia ni pamoja na fadhaiko, wasiwasi uliopitiliza kuhusu uwezo wa
kufanya tendo la ndoa, au dhulma za kijinsia ambazo alikumbana nazo utotoni
mwake.
HATARI ZAKE
Hatari ya tatizo la
kuwahi kumwaga hutokana na athari zake, ambazo zinamsibu mwanaume na mwanamke
kwa pamoja. Miongoni mwa athari mbaya za maradhi haya ni mhusika kujihisi uduni
na kutouamini uwezo wake wa kiume. Baadhi wa wanaume, wanaweza kukatisha
uhusiano wa ndoa au kutengeneza matatizo ili kuepuka hisia za kushindwa.
Tatizo hili linaweza
pia kumzuia kijana kuingia kwenye ndoa. Aidha, huibua wasiwasi na hofu ambayo
huonekana katika muamala wake sio tu na mkewe, bali pia muamala wake kwa watu
wanaomzunguka.
Ama kwa upande wa mke,
atahisi hali ya kukanganyikiwa na kuhisi kwamba ametengwa kwa sababu ya hatua
za mume zisizokuwa za kawaida za kujitenga na mkewe. Pia inaweza kumfanya mke
asijiamini na kuhisi kuwa mumewe anamtenga kwa sababu anavutiwa na mwanamke
mwingine.
Kuna utafiti unaoonesha kuwa pindi mume
anapokuwa na tatizo la udhaifu wa kiume basi asilimia 42 ya wanawake huhisi
kuwa wao ndio tatizo, yaani wanahisi kuwa tatizo hilo la mume linatokana na wao
kutokuwa na mvuto kwa waume zao.
TIBA
Baada ya kujua sababu,
hatari na athari za maradhi hayo, hatuna budi tujue tiba na dawa ambazo
tunaweza kuzitumia kuondoa tatizo hilo la kumwaga mapema. Njia za kuondokana na
tatizo hilo zimegawanyika katika maeneo 3 kutokana na chanzo chake:
Kwanza unapokuwa ukishiriki tendo jitahidi kufanya taratibu usiwe na papara, Wengi wamrjikuta wakiwa na shida hii kutokana na kuwa na papara au haraka katikati ya tendon a hali hiyo wengi hujifunza kupitia mikanda ya ngono wakidhani kuwa kulala na mwanamke ni lazima ufanye kwa haraka ndio uonekane mwanaume kweli. Lakini ukweli ni kwamba unapofanya taratibu ni njia nzuri zaidi kwani utamfikisha mwenzi wako na wewe utachelewa kufika kilele pia.
Kwanza unapokuwa ukishiriki tendo jitahidi kufanya taratibu usiwe na papara, Wengi wamrjikuta wakiwa na shida hii kutokana na kuwa na papara au haraka katikati ya tendon a hali hiyo wengi hujifunza kupitia mikanda ya ngono wakidhani kuwa kulala na mwanamke ni lazima ufanye kwa haraka ndio uonekane mwanaume kweli. Lakini ukweli ni kwamba unapofanya taratibu ni njia nzuri zaidi kwani utamfikisha mwenzi wako na wewe utachelewa kufika kilele pia.
1.Njia ya kisaikolojia:
Hapa kinachotakiwa kuangaliwa ni yale matatizo ya ndoa. Mke anaweza kuzungumza
na mume kumuondolea wasiwasi na kutafuta njia za kuyashughulikia matatizo yao.
Pia, mume anatakiwa kutokuwa na wasiwasi kuhusu uwezo wake wa kiume.Ni muhimu utambue
uwezo wa mwanaume kushiriki tendo la ndoa huanzia kwenye akili yake. Bila
utulivu wa kiakili sahau kuhusu utendaji mzuri kitandani.
2.
Kutumia Mbinu: Njia
hii inasaidia kuboresha uwezo wa mwanaume katika kudhibiti umwagaji kwa kutumia
baadhi ya mbinu maalumu. Kwa mfano, wakati anapokaribia kumwaga anaweza
kuchomoa dhakari yake na kuanza upya au kutulia kwa sekunde 30 alafu akaendelea. Pia anaweza kutumia mbinu ya kuiminya
dhakari yake.Yaani Jenga utaratibu wa Fanya na kuacha: hii ni ile hali ya unapoona
unakaribia kutoa mbegu basi unaweza kusimama angalau kwa sekundi 30
kisha unaanza upya. Hii husaidia sana kuchelewa kufika kileleni na
hauta weza kumaliza kwa haraka.
3.
Dawa: Ama kuhusu dawa,
kuna dawa fulani iliyopitishwa hivi inaitwa Lejam. Dawa
hii inasaidia kutatua tatizo la kuwahi kumwaga.Pia dawa kama Tramadol japo ni dawa ya maumivu ila tafiti zinaonesha kuwa inaweza kuchelewesha mtu kufika kileleni hivyo kutumika pia kutibu tatizo hili.
Mwisho matumizi ya Condom pia huweza kumfanya mtu kuchelewa kufika kileleni.
Mwisho matumizi ya Condom pia huweza kumfanya mtu kuchelewa kufika kileleni.
No comments