FAIDA ZA MABOGA KIAFYA


Boga ni tunda ambalo watu wengi wanalipuuzia.Ni tunda lenye virutubisho vingi na lina faida nyingi kiafya.Tunda hili ni chanzo kizuri cha virutubisho aina ya BETA CAROTENE  ambavyo vinafanya boga kuwa na Rangi ya njano.Pia ndani ya tunda hili kuna virutubisho vingine kama potassium,Vitamin c,vitamin E,na madini ya chuma kwa wingi.
Betta carotene hii ndio umeng'enywa na kubadilisha kuwa vitamin A.Kula vyakula vyenye Beta carotene nyingi husaidia kuzuia magonjwa kama saratani,shinikizo la damu(high blood pressure),na magonjwa ya moyo.

SHINIKIZO LA DAMU
Boga lina kiwango kikubwa cha Potassium ambayo husaidia kupunguza Kiwango cha Madini ya sodium mwilini ambayo hupelekea kuongezeka kwa shinikizo la damu(high blood pressure) Kwa hiyo boga ni mojawapo ya vyakula muhimu kwa mtu mwenye presha ya kupanda.Vyakula vingine vyenye Potassium nyingi ni kama AVOCADO,NANASI,NDIZI MBIVU,NYANYA,MACHUNGWA NA SPINACH
Pia potassium inasaidia kuukinga mwili dhidi ya magonjwa ya moyo,kiharusi(stroke) na tatizo la mawe kwenye figo

SARATANI(CANCER)
Utafiti uliofanywa na kitengo cha lishe cha chuo Kikuu cha HAVARD USA unaonesha kuwa kula vyakula vyenye beta calotene kwa wingi inasaidia kuzuia saratani ya tezi dume(prostate cancer)

AFYA YA MACHO
Boga lina vitamin C,Vitamin E virutubisho hivi pamoja na Beta calotene husaidia kuimarisha afya ya macho,na huzuia tatizo la kutoona vizuri wakati wa uzee.

UZAZI
Boga pia lina madini ya chuma ambayo ni muhimu kwa wanawake ambao wako kwenye umri wa kuzaa(child bearing age) kwani yanasaidia kuchochea uzazi(promotes fertility)
Pia Vitamin A inayotokana na beta calotene ni muhimu kwa afya ya mama mjamzito na anaenyonyesha.

KINGA YA MWILI(IMMUNITY)
Beta calotene pamoja na vitamin C vinavyopatikana kwenye boga husaidia kuimarisha kinga ya mwili.


3 comments: