Ni msukumo wa damu ulio juu kuliko inavyotakiwa kwa muda mrefu. Msukumo
wa damu huhitajika mwilini ili kusambaza chakula, oksijeni na kutoa
uchafu.
Shinikizo la damu hupimwa kwa kutumia kifaa kinachoitwa Sphygmomanometer
Shinikizo la damu husababishwa na nini?
Vitu vifuatavyo vinaweza kusababisha shinikizo la juu la damu:
Uvutaji sigara
Unene na uzito kupita kiasi
Unywaji wa pombe
Upungufu wa madini ya potassium
Upungufu wa vitamin D
Umri mkubwa
Ongezeko la kemikali kwenye figo (renin)
Kushindwa kufanyakazi kwa kichocheo kiitwacho insulin
Uanishaji wa shinikizo la damu
Presha ya kawaida <120 <80
Presha inayoelekea kupanda 120-139 80-89
Presha hatua ya 1 140-159 90-99
Presha hatua ya 2 160-179 100-109
Presha hatua ya 3 ≥180 ≥110
Shinikizo la damu/BP ni ugonjwa unaosumbuwa watu wengi sana duniani na
hii ni kutokana na kutokujuwa ni nini hasa husababisha ugonjwa huu
mwilini. Shinikizo la damu linaonekana kuwa ni ugonjwa wa kuishi kwa
kufuata masharti.
Katika makala hii tutaona uhusiano mkubwa uliopo kati ya upungufu wa
maji mwilini na ugonjwa huu, mwishoni utakuwa umeelewa sasa ni jinsi
gani ilivyo rahisi kabisa kujiepusha na kujiponya ugonjwa huu. Endelea
kusoma.
Takwimu za Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) zinasema tayari watu
bilioni moja duniani kote, wanaathiriwa na shinikizo la juu la damu huku
likisababisha mshtuko wa moyo (Heart Attacks), kupooza na kiharusi
(Strokes).
Takribani watu milioni nane hufa kila mwaka kutokana na ugonjwa huu wa kupanda kwa shinikizo la damu.
Dalili zitakazokutokea unapokuwa na ugonjwa huu ni pamoja na;
Maumivu ya kichwa (Haswa nyuma ya kichwa mara nyingi nyakati za asubuhi),
Kuchanganyikiwa,
Kizunguzungu,
Kelele sikioni (Mvumo au Mazomeo masikioni),
Kutoweza kuona vizuri au
Matukio ya kuzirai.
Uchovu/kujisikia kuchokachoka
Mapigo ya moyo kwenda haraka
Kutokuweza kuona vizuri
Damu kutoka puani
Uonapo dalili hizi unapaswa kuwahi hospitali kupata vipimo.
‘Mwili wa binadamu unapopungukiwa maji hutoa ishara (indicators),
tumeziita ishara hizo kuwa ni magonjwa, hauumwi, una kiu, usiitibu kiu
na madawa – dr. Batmanghelidj’.
Shinikizo la damu (hasa la juu) ni kiashiria cha mwili kupungukiwa maji
kwa kiwango kikubwa, ni wakati ambapo mwili unajaribu kujizoesha na
upungufu wa jumla wa maji wakati kunapokuwa hakuna maji ya kutosha
kuijaza mishipa ya damu yenye kazi ya kusambaza maji kwenye seli mhimu.
Mishipa ya damu imebuniwa maalumu kuendana na mtiririko uliosawa wa
ujazo wake wa damu na mahitaji mbalimbali ya tishu kwa kufunga na
kufungua mishipa mbalimbali ya damu ndani ya mwili.
Figo hushtuka upesi kulingana na mtiririko wa damu. Hili
linaposhindikana, yaani iwapo mtiririko au ujazo wa damu utapungua, basi
Figo huitoa homoni iitwayo ‘renini’ ambayo yenyewe huzarisha kitu
kiitwacho ‘angiotensini’ ambayo huwa na matokeo mawili; kwanza huzibana
ateri na kupandisha shinikizo la damu, pili huisababisha tezi ya
‘adreno’ kutoa homoni iitwayo ‘aldosteroni’ ambayo huzifanya figo
kuishikilia chumvi na hivyo kusababisha kupanda kwa shinikizo la damu.
Asilimia 94 ya damu ni maji. Kwa ujumla kila seli ndani ya miili yetu
ina bahari ya maji baridi ndani yake na bahari ya maji chumvi nje yake.
Afya bora inategemea uwiano mzuri wa maji ya bahari hizo mbili.
Chumvi inayashikilia na kuyalazimisha baadhi ya maji kubaki nje ya seli
(osmotic retention) na potasiamu inayashikilia maji ndani ya seli.
Wakati mwili unapokuwa katika upungufu wa maji (yaani haunywi maji ya
kutosha kila siku) mwili utaongeza ujazo wa maji chumvi kwenye bahari ya
nje ya seli.
Kupitia mfumo maalumu, homoni iitwayo ‘vasopressini’ hutolewa ambayo
inaweza kuyachuja maji ya chumvi toka katika bahari ya nje ya seli na
kuyachoma maji hayo baridi (baada ya kuwa yamechujwa) ndani katikati ya
bahari ya ndani ya seli kama yanavyohitajika ili kuutunza uwiano sawa wa
maji ndani na nje ya seli.
Lakini ili mbinu hii ifanikiwe, mbinu gani, mbinu ya kuyachuja maji ya
chumvi toka katika bahari ya nje ya seli, vasopressini husababisha
kapilari na mishipa ya damu kujikaza au kupunguza vipenyo vyake na
kukupatia wewe shinikizo la juu la damu (BP) ambalo ni mhimu ili
kuyachuja na kuyachoma maji baridi ndani ya seli toka katika bahari ya
maji chumvi iliyopo nje ya seli.
Kama mishipa ya damu haitapunguza vipenyo vyake, baadhi ya gesi
itaachana na damu ili kuziba nafasi zilizowazi kutokana na kupungua kwa
umajimaji mwilini na hatimaye kukusababishia msongamano wa Gesi (Gas
locks).
Sifa hii ya vipenyo vya mishipa ya damu kujirekebisha kwa ajili ya
mzunguko wa damu, ndiyo mtindo unaotumika zaidi katika kanuni za
kihaidroliki wakati ambapo mzunguko wa damu mwilini umejirekebisha
kuendana na kiasi cha umajimaji kinachopatikana.
Wakati mwili unapokuwa katika upungufu wa maji kwa mfano kutokana na
kutokunywa maji ya kutosha; asilimia 66 ya kuishiwa maji inajionesha kwa
kupungua kwa ujazo wa seli, asilimia 26 inapotea toka ujazo wa
umajimaji uliopo sehemu ya nje ya seli na asilimia 8 tu inapotea toka
katika ujazo wa damu.
Shinikizo la juu la damu ni kiashirio cha mwili kupungukiwa maji kwa
asilimia 8 tu, lakini madhara yanajitokeza sababu ya asilimia 66 ya
kupunguwa kwa ujazo wa seli.
Maji na chumvi vitalirudisha shinikizo la damu katika hali yake ya kawaida.
Hii ndiyo sababu shinikizo la damu linapaswa kutibiwa kwa kuongeza
unywaji wa maji pekee. Dr.Batmanghelidj anasema; Maji peke yake, ni dawa
bora ya kukojosha, pekee ya asili tuwezayo kuiendea.
Kama watu wanaosumbuliwa na shinikizo la damu wangeongeza kiasi cha
uchukuaji maji, hawatazihitaji dawa za kukojosha, watazarisha mkojo wa
kutosha na hivyo kuiondoa chumvi iliyokuwa imezidi!. Watatakiwa pia
kuacha kula vyakula visivyo na chumvi na hivyo kuepukana na mikakamao ya
mishipa (cramps) kwenye miguu yao.
Madhara yanayoweza kuletwa na shinikizo la damu:
Kwa mjibu wa dr.Batmanghelidj, kutokulielewa shinikizo la damu kama moja
ya ishara za mwili kupungukiwa maji na kulitibu kwa dawa za kukojosha
ambazo zinaukausha mwili zaidi, baada ya muda zitasababisha;
Kuzibika kwa ateri za moyo na ateri ziendazo kwenye ubongo
Shambulio la moyo (heart attack)
Mishtuko midogo midogo au mikubwa inayopelekea kuzimia
Ugonjwa wa kibofu cha mkojo
Kiharusi
Kupungua kwa nguvu za kiume kwa upande wa wanaume
Kuharibiwa kwa ubongo na matatizo ya akili kama vile kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).
Daktari mwingine, Dr.David Brownstein katika kitabu chake kiitwacho;
“Salt Your Way to Live”, anasema kwamba alifundishwa katika vyuo vya
kiganga kuwa chumvi husababisha shinikizo la damu na kuwa kila mmoja
lazima ale vyakula vyenye chumvi kidogo. Na hili watu wengi wamekuwa
wakiamini hivi.
Wakati akiwatibu wagonjwa wake, anasema; alianza kuona kuwa wale
wanaotumia vyakula vyenye chumvi kidogo wanapata matokeo ya chini au
wanapata nafuu ndogo sana kutoka katika vyakula hivyo vyenye chumvi
kidogo au bila chumvi kabisa na wengi wao walitokewa kuwa na uhaba
mkubwa wa madini katika miili yao.
Katika utafiti wake ili kuwasaidia wagonjwa wake, ndipo akaja na jibu la
chumvi ya baharini ambayo haijasafishwa (unrefined sea salt) ambayo
huwa na madini mengine zaidi ya 80 ndani yake, alianza kuona kitu kigeni
kinaanza kutokea. Wagonjwa wake hao wakaanza kuona mashinikizo yao ya
damu yanaanza kushuka katika kiwango ambacho wanaweza kuachana kabisa na
matumizi ya dawa.
Dr.Batmanghelidj anasema, ikiwa watu watajishughulisha na mazoezi hasa
mazoezi ya kutembea kwa miguu, watakunywa maji halisi zaidi na kuongeza
chumvi (siyo sodiamu) kidogo ya ziada kwenye vyakula vyao, mashinikizo
yao ya damu yatarudi katika hali yake ya kawaida.
Swali la kujiuliza; Ni zaidi ya miongo minne sasa tangu tulipoambiwa
kula vyakula vyenye chumvi kidogo ili kuepukana na shinikizo la damu,
kwanini sasa Idadi ya watu wanaopatwa na ugonjwa huu inazidi
kuongezeka?.
Narudia tena, mwili unapoanza kuishikilia chumvi, hufanya hivyo ili
kuhifadhi maji, toka katika bahari chumvi hiyo ya nje ya seli, maji
huchujwa na kutumika wakati wa mahitaji ya dharura.
Maji na chumvi kwa pamoja vitalirudisha shinikizo la damu katika hali
yake ya kawaida. Kuikimbia chumvi kunasababisha shinikizo la damu (BP)
kuwa sehemu ya maisha yetu, tutapata nafuu, lakini baada ya muda mfupi
hali hurudi ileile na pengine kuwa watumwa wa kuchagua kula hiki au
kile.
Tofauti na zamani ambapo shinikizo la juu la damu lilipokuwa ni ugonjwa
wa watu wanene au wenye uzito uliozidi pekee, siku hizi wanene kwa
wembamba, watoto kwa wakubwa wanaugua BP



No comments