Tatizo la kubana kwa govi ni nini?


Tatizo la kubana kwa govi (paraphimosis) ni tatizo hatari linaloweza kuwapata wanaume na wavulana ambao bado hawajatahiriwa. Kubana kwa govi kuna maanisha govi limebana na kukwama nyuma ya kichwa cha uume na  huwezi kulirudisha kwenye sehemu yake ya kawaida.

Nini sababu ya tatizo la kubana govi?Kubana kwa govi

Wanaume ambao hawajatahiriwa wakati mwingine wanavuta govi nyuma wakati wa kushiriki ngono, wanapokwenda chooni au wanapokuwa wanasafisha uume. Madaktari au manesi wanaweza pia kuvuta govi nyuma wanapokuwa wakifanya uchunguzi wa uume au kuweka mpira wa mkojo.

Wakati mwingine daktari au nesi anaweza kusahau kurudisha govi mahala pake. Kama govi litaachwa nyuma ya kichwa cha uume kwa muda mredu, uume unaweza kuvimba sana kiasi kwamba govi linakwama na kushindwa kurudi.

Nifanye nini ili kuzuia kupata tatizo la kubana kwa govi?

  • Baada ya ngono, kutoka chooni au baada ya kujisafisha, hakikisha unarudisha govi mahala pake.
  • Kamwe usiache govi nyuma ya kichwa cha uume kwa muda mrefu zaidi ya inavyohitajika
  • Kama umekewa mpira wa mkojo, jiangalie kama govi limerudishwa mahala pake na kufunika kichwa cha uume

Ni nini kinachotokea nikipata tatizo la kubana kwa govi?kubana kwa govi

Tatizo la kubana kwa govi linasababisha maumivu makali, lakini sio wakati wote. Unaweza kupata maambukizi kwenye uume. Unaweza kushindwa kabisa kukojoa. Kama unaona inakuwa ngumu kurudisha govi ni vizuri kumwona daktari haraka sana.

Kitu cha kwanza atakachofanya daktari ni kutibu uvimbe uliopo. Hili linaweza kufanyika kwa kubonyeza uume kwa mikono au kwa kuufunga kwa nguvu kwa bandeji. Baada ya uvimbe kupungua, daktari ataweza kuvuta govi na kulirudiha mahala pake. Kama bado govi limebana, daktari anaweza kuhitaji kukata kidogo sehemu ya govi ili kufanya iwe rahisi kurudisha.

No comments