THAMANI YA MADINI YA ZINC (ZINKI) KATIKA UTUNZAJI WA MIMBA NA KUBORESHA SIFA YA MWANAUME




UTANGULIZI
Ina kadiriwa kuwa mwili wa mwanadamu una kiwango cha 2gm za zinc, ambapo 60% hupatikana kwenye misuli na 30% kwenye mifupa, ingawa hupatikana mwili mzima. Kuna sababu nyingi ambazo zinaweza kupelekea zinc kusharabu lakini matumizi ya pamoja na madini ya chuma, calcium, copper (kopa), na cadmium hupunguza kiwango cha zinc kusharabu.

Ni mara chache jamii yetu hutambua na kuthamini utumiaji wa vyakula kama tiba yenye maboresho katika matatizo mbali mbali yanayotukumba.
Zinc imeonesha kuwa na majukumu mbali mbali mwilini ambapo imeonesha kuimarisha kinga ya mwili, kuimarika kwa mfumo wa fahamu, huboresha sukari mwilini, mafua, huimarisha uponaji wa vidonda, matatzo ya akili, makanda wa jeshi, matatizo ya kupoteza hamu na radha ya chakula, matatizo ya sikio, vidonda sehemu za siri n.k



VYAKULA VYENYE MADINI YA ZINC KWA WINGI

1. Nyama
2. Ini
3. Mayai
4. Samaki wa baharini
5. Jamii ya karanga
6. Nafaka
7. Uyoga
8. Mbegu za maboga
9. Jamii ya maharage ya kijani



DALILI ZA UKOSEFU WA MADINI YA ZINC

1. Kupoteza hamu radha ya chakula
2. Ukuaji wa kusua sua kwa mtoto
3. Mwili kuwasha mara kwa mara
4. Kuhara kwa muda mrefu
5. Upungufu wa kinga ya mwili
6. Vidonda kuchelewa kupona
7. Kupoteza uwezo aa kuona
8. Mabadiliko ya tabia hasa uchovu wa mara kwa mara
9. Kushindwa kusimama kwa uume na kukosa hisia za mapenzi
10. Muda wa momba kupitiliza miezi tisa
11. Uwezekano wa mimba kutoka
12. Mtoto kuzaliwa na vilema
13. Mtoto kuzaliwa na uzito mdogo
14. Mtoto kukosa utulivu karibia miezi sita



JINSI MADINI YA ZINC YANAVYOSAIDIA KATIKA MATIBABU YA UGUMBA KWA MWANAUME NA UTUNZAJI WA MIMBA
Upungufu wa madini ya zinc hupelekea upunguaji wa uzalishaji wa mbegu za kiume na hatimae kuathiri uwezekano wa mwanaume kutunga mimba.

Pia, upungufu wa madini haya hupelekea kupungua uzalishaji wa homoni ya kiume “testosterone” ambapo inaweza kupelekea ukuaji hafifu wa korodani na kushindwa kusimamisha uume.

Kwa wanawake, upungufu wa madini haya huhusishwa na mimba kutoka, mtoto kuzaliwa amekufa, vilema kwa mtoto na matatizo mengine. Ni kwasababu madini haya huhusika zaidi katika uzalishaji wa homoni za kike kama oestrogen na progesterone

NYONGEZA: Madini ya zinc husaidia kutunza vitamin E isipungue mwilini, ambapo vitamin E huhusika zaidi na ulinzi wa chembe hai zetu mwilini
—- Katika masuala ya uzazi Vitamin E husaidia kulinda mbegu za kiume na mayai kwa wanawake.

Karibu kwenye madarasa yetu ya kila siku BURE.
https://chat.whatsapp.com/B9YE3TAEYld7UT3SZUzPQG

No comments