TATIZO LA PUMU YA NGOZI (ECZEMA)

 



Ni hali ambayo hufanya ngozi kuwa nyekundu na kuwasha. Ni hali inayojitokeza sana kwa watoto lakini huweza kutokea kwenye umri wowote ule. Tatizo hili huwepo kwa maisha yote ya mtu ama kwa muda mrefu na huweza kuibuka kwenye muda flani na wakati mwingine dalili zinaweza zikapotea kabisa.

Tatizo hili linaweza kuambatana na pumu ya kifua na mafua yamara kwa mara(hay fever)
Hakuna tiba ponyaji iliyopatikana kwa ajili ya kutibu pumu ya ngozi. Lakini matibabu ya dalili na kujitunza kwa mtu huweza kupunguza dalili na kuzuia kuibuka ibuka kwa dalili.

Kwa mfano mwathirka anatakiwa kuzuia sabuni zenye pafyumu na vikereketa vya ngozi, kuzuia kutumia sabuni zenye madawa au mafuta na kufanya mambo yanayofanya ngozi iwe raini
Unatakiwa kumwona daktari wako endapo dalili unazopata zinakufanya usifanye kazi zako kama ipasavyo au zinakuzuia kulala

Dalili

 

Dalili za pumu ya ngozi hutofautiana kutoka mtu mmoja na mwingine, dalili huwa pamoja na;

  • Kuwashwa ngozi, hali inaweza kuwa mbaya zaidi san asana wakati wa usiku
  • Kupata mabaka mekundu(kwa watu wenupe) au brauni au meusi sana sana katika viganja, miguu, kisigino, kiwiko cha mkono, kiuno, shingo, juu ya kifua, kope za macho, kwenye maungio ya mikono kwa ndani na ya magoti na kwa watoto kwenye uso na kichwani
  • Vipele vidogo vilivoinuka, vinavyoweza kutoa maji maji na kupasuka kama vikikwanguliwa
  • Ngozi kuwa nene, iliyochanika, kavu na yenye magamba
  • Ngozi kuongezeka hisia, kuvimba inapokwanguliwa

Pumu ya ngozi mara nyingi huanza kabla ya umri wa miaka 5 na huweza kuendelea hadi kwenye utoto na utuuzima. Kwa baadhi ya watu unaweza kujitokeza mara kwa mara na wakati wmingine unaweza kupotea kwa muda
Mambo yanayofanya pumu ya ngozi kuwa na dalili kali

Watu wengi wenye pumu ya ngozi wanaambatana kuwa na maambuizi ya ngozi ya bacteria staphylococcus aureus ambaye hukaa kwenye ngozi. Bacteria huyu hukuwa haraka endapo ngozi inamichaniko kutokana na kujikwangua na kukiwa na majimaji. Jambo hili linaweza kufanya mtoto kuwa na dalili kali san asana sana kwa watoto.

Mambo ambayo yanafanya pumu ya ngozi iwe na dalili kali zaidi ni kama vile

  • Ngozi kuwa kavu, inayoweza kutokea endapo mtu anaoga kwa muda mrefu kwenye maji ya moto/uvuguvugu
  • Kujikwangua, kunakoweza kufanya ngozi ikachanika
  • Maambukizi ya bacteria na virusi
  • Msongo wa mawazo
  • Jasho
  • Kubadilika kwa joto na hali ya hewa
  • Madawa ya kuoshea, sabuni na madawa ya kusafisha kwa kukausha(detergents)
  • Kuvaa nguo zenye nylon, polyester, mablanket na kapeti n.k
  • Vumbi na chavu(polen)
  • Kuvuta ugolo na uchafuzi wa hewa
  • Mayai, maziwa, karanga, maharagwe ya soya, samaki na ngano, kwa vichanga na watoto

Pumu ya ngozi inahusishwa na mambo ya alegi. Lakini kuondoa kwa alegi hupunguza kwa kiasi kidogo tatizo la pumu ya ngozi kutoa dalili. Cha kushangaza vitu vinavyoweza kutunza/kudaka vumbi kama mto wa manyoya,zuria, godoro, huweza kusababisha mtu kupata dalili za pumu ya ngozi mara kwa mara.

Wakati gani wa kumwona daktari?

Huna raha na unakosa usingizi kwa kujikwangua ama ratiba zako kuharibika
  • Ngozi ikiwa inauma
  • Unashaka kwamba ngozi yako imepata maambukizi, usaha na kuwa nyekundu)
  • Umejaribu kujitibu mwenyewe kwa kuzingatia kanuni lakini hamna matokea mazuri
  • Unadhani kwamba hali ya ugonjwa wako imeathiri macho ama kuona kwako
  • Kama mwanao akiwa na dalili za pumu mpeleke hsospitali kwa elimu na ushauri pamoja na matibabu

Visababishi vya pumu ya ngozi
  • Sababu za msingi zinazosababisha pumu ya ngozi hazijulikani. Ngozi yenye afya huwa na uwezo wa kutunza unyevu na kuzuia dhidi ya maambukizi ya kwenye ngozi, vikereketa ngozi, n.k. pumu ya ngozi inaonekana kuambatanan na mambo mengi kama
  • Ngozi kavu, ngozi inayowasha, ambayo hufanya ngozi kuwa na uwezo mdogo wa ulinzi kizuizi
  • Mabadiliko ya geni yanayosababisha ngozi isifanye kazi kama kinga kizuizi
  • Mfumo wa kinga wa mwili kutofanya kazi ipasavyo
  • Bacteria kama styphylococcus aureus ambao hufanya uzio unaoziba njia  za tezi jasho
  • Hali ya hewa
Vihatarishi vya pumu ya ngozi
Mambo yanayomuweka mtu hatarini kupata pumu ya ngozi ni kama vile
  • Kuwa na historia katika familia ya pumu ya ngozi, kuwa na alegi, homa ya mafua, au pumu ya kifua
  • Kuwa mfanyakazi wa afya ambayo huambatanishwa na pumu ya ngozi kwenye mikono
  • Vihatarishi kwa watoto ni kama vile
  • Kuishi maeneo ya mjini- sehemu hizi huwa na vikereketa ngozi vingi na uchafuzi wa hewa
  • Kuwa mtu mweusi
  • Kuwa na wazazi wenye elimu ya juu
  • Kuhudhuria kwenye vituo vya kutunzia watoto
  • Kuwa na tatizo la kutokuwa makini na utundu (ADHD)

Madhara ya pumu ya ngozi
  • Pumu ya kifua na homa ya mafua- pumu ya ngozi maranyingi huanza kuonekana kabla
  • Miwasho sugu, ngozi kuwa na mabaka/magamba
  • Maambukizi kwenye ngozi
  • Matatizo ya macho-macho kuwasha kwenye kope macho kutoa majimaji na michomo kwenye macho
  • Kuwasha viganja na mikono
  • Kushindwa kulala
  • Kubadilika kwa tabia kama kushindwa kulala ama kutokuwa mtulivu ADHD. Tafiti zimeonyesha hivyo
Matibabu na dawa
  • Pumu ya ngozi inaweza kuonyesha dalili endelevu, unaweza kuhitajika kujaribu matibabu mbalimbali kwa miezi ili kuweza kupambana na dalili hizo na hata kama ukifanikiwa kutibu dalili, zinaweza kujirudia tena.
  • Ni muhimu kujijua mapema ili kujitahadhari mapema pia kama pumu ya ngozi inaweza kuamka. Kama matibabu ya kufanya ngozi iwe laini na matibabu mengine hayawezi kukusaidia daktari wako anaweza kukushauri juu ya matibabu kama haya
  • Madawa
  • Krimu zinazozuia kuwasha kwa ngozi na michomo. Mafuta ya corticosteroid, ongea na daktari wako kabla ya kutimia dawa hii. Matumizi yasiyo sahihi ya dawa hii yanaweza kusababisha ngozi ibadilike rangi, kuwa nyembamba kupata maambukizi na kupata michirizi.
  • Krimu inayoponya ngozi.
  • Dawa kama tacrolimus na pimecrolimus hudhuru mfumo wa kinga ya mwili. Ikiwa itawekwa kwenye ngozi itasaidia kuamsha kinga ya mwili na kusababisha kupona kama kuna majeraha, kuondoa miwasho na kuzuia kujirudia rudia kwa dalili. Kwa sababu ya madhara yake mengine dawa hii hutumika kwa watu ambao wameshindwa kupona dalili kwa njia zingine
  • Dawa za kupambana na maradhi/aambukizi
  • Dawa za kunywa za kuzuia miwasho
  • Kama dephenydramine huweza kusaidia
  • Madawa ya kunywa ama kuchoma kuzuia michomo inayotokana na kinga ya mwili kujishambulia kama corticosteroid- madawa haya yakitumika kwa muda mrefu hushusha kinga ya mwili na mtu anakuwa hatarini kupata maambukizi

Matibau ya nyumbani

Nguo zenye unyevu
Funga eneo lililoathirika kwa kitambaa/bandeji chenye unyevu ama chenye dawa ya corticosteroid. Imethibitishwa kuwa na uwezo wa kupambana na dalili kwa masaa kadhaa hadi masiku. Wakati mwingine hufanyika hospitali kwa sababu matibabu haya yanahitaji utaalamu, ama unaweza kufundishwa kujitibu mwenyewe nyumbani

Tiba ya mwanga
Weka ngozi yako kwenye mwanga asili wa jua.matibabu ya mwango usio asili huweza kutumika pia, Ingawa matibabu ya mwanga wa jua ya muda mrefu huwa na madhara kama vile ngozi kuzeeka mapema na kuongezeka kwa hatari ya kupata saratani ya ngozi. Kwa namna hii matibabu ya mwanga usio asili hutumika kwa watoto wadogo na vichanga.

Kujitibu msongo wa mawazo
Kutibu msongo wa mawazokwa ushauri tiba kwa watu na watoto ambao wanahosia kuhusu hali zao kunweza kuwasauidia kuondokana na msongo wa mawazo na ugonjwa kuwa mbaya zaidi

Kupumzika na kubadili tabia
Kunaweza kusaidia kuepuka kujikwangua

Pumu ya ngozi kwa watoto
Huweza kutibika kwa
  • Kutambua na kuepusha mtoto na viamsha pumu ya ngozi
  • Kuzuia joto kupita kiasi(maji ama la nguo)
  • Kumpaka mtoto mafuata ya Vaseline yasiyo na perfume

Matibabu mbadala
Madawa megi ya tiba mbadala yamewasaidia watu kupunguza na kudhibiti dalili za pumu ya ngozi. Tafiti zimeonyesha watu wengii waliotumia madawa ya kiasili china yalisaidia kupunguza ngozi kuwasha na kujikuna lakini kwa muda mfupi tu

Vifuatavyo husaidia kwa namna Fulani
Virutubisho lishe kama vitamin D na E, madini ya  zinc na selenium

Mambo mengine ya kuzingatia kutibu dalili za pumu ya ngozi ni kama vile
  • Kutumia nguo za pamba-achana na nguo za nylon ama sil kwani huwa na vikaereketa ngozi
  • Matumizi ya mafuta ya vaselini yasiyo na manukato
  • Matumizi ya sababuni za vipande zisizo na manukato na zisizokausha ngozi kama kuku n.k sababni hizimara nyingi huwa ni zile za kufulia nguo
  • Oga mara tatu kwa siku na jipake mafuta mengi ya Vaseline yasiyo na manukato
  • Usitumie vitu vinavyokausha ngozi kama spiriti n.k

No comments