MAUMIVU MAKALI WAKATI WA HEDHI (DYSMENORHOEA)



leo nitazungumzia hili swala. Hili ni tatizo linawakumba asilimia 25 hadi 30 ya wanawake duniani kulingana na tafiti.
Ntazungumzia kwa kifupi lakini tutaelewa kwa undani sayansi ya tatizo hili kutokea hapo utaelewa njia mbali mbali tunazosahuliwa kufanya ili kutibu tatizo hili ni za kweli au la.
TUNAPOSEMA TATIZO LA MAUMIVU WAKATI WA HEDHI AU DYSMENORHOEA TUNAMAANISHA NINI?
Kila mwanamke wakati wa hedhi anapata maumivu ya tumbo kutokana na kuta za kizazi zinakuwa zinasinyaa ili kutoa damu na uchafu mwingine wa hedhi.
Ila kuna watu wanapata maumivu makali sana kiasi cha kuathiri uwezo wao wa kufanya shughuli zao za kila siku. Hapa ndo tunasema mtu ana tatizo la Dysmenorhoea.
CHANZO CHA TATIZO HILI.
Chanzo kinategemea na aina ya tatizo hili, hivyo tuangalie aina kuu 2 za tatizo hili hapo hapo nitaelezea na chanzo cha aina hyo ya Dysmenorhoea
AINA YA KWANZA : PRIMARY DYSMENORHOEA.
Hii ni pale mtu anapopata maumivu makali wakati wa hedhi wakati hana tatizo lolote kwenye mfumo wake wa uzazi. Aina hii hutokea katika umri wa miaka 16 hadi 30.
Inasababishwa na kutokua na uwiano sawa wa kemikali katika mwili kama ifatavyo.
Unapofika katika hedhi progesterone inavopungua ili uanze hedhi kuta za mji wa mimba huzalisha kemikali inayojulikana kama *PROSTAGLANDIN* hii hufanya kuta za mji wa mimba kusinyaa na kupelekea maumivu wakati wa hedhi. Kwa baadhi ya watu wanakua na uwiano usio sawa wa hormone za uzazi yani progesterone na estrogen. Estrogen inapokua juu sana inapelekea kutengenezeka kwa seli za mafuta (fat cells )kwenye mji wa mimba hivyo kulazimisha kuta hizo kuzalisha Prostaglandin kwa wingi hali inayopelekea kuta za mji wa mimba kubana sana na kupelekea maumivu makali.
Pia kuta zinabana sana hupelekea kubanwa kwa mishipa ya fahamu (nerves) na mirija ya damu inayoleta damu kwenye mji wa mimba hali inayopelekea maumivu zaidi.
Baadhi ya chemikali hizi huingia kwenye mfumo wa damu na kupelekea mwanamke kupata kichefuchefu, kichwa kuuma, kutapika na
wakati mwingine kuharisha na baadhi huzimia
Kwa Baadhi ya watu wenye aina hii ya Dysmenorhoea linaisha lenyewe baada ya kubeba mimba na kuzaa.
AINA YA 2: SECONDARY DYSMENORHOEA
aina hii mtu anapata maumivu makali wakati wa hedhi kutokana na kuwa na matatizo mengine kwenye mfumo wake wa uzazi mfano, vimbe kwenye mayai (ovarian cyst) vimbe kwenye mji wa mimba (cyst), maambukizi kwenye viungo vya uzazi (PID), Endometriosis,tatizo la kizazi kugeuka nk.
DALILI
Utawezaje kutofautisha kati ya PRIMARY na Secondary Dysmenorhoea kulingana na maumivu yake.
Kwa primary PRIMARY Dysmenorhoea maumivu yake yanakua sehemu ya chini ya ya kitovu yanaenda mpaka mgongoni na hadi sehemu ya katikati ya mapaja.
Secondary Dysmenorhoea maumivu yanakuwa sehemu moja tu kama chanzo kipo kwenye mji wa mimba utayasikia tu sehemu ya chini ya kitovu kama ni kwenye ovari au mirija basi utajasikia tumbo la chini upande wa kulia au kushoto hayaendi mgongoni wala katikati ya mapaja
Na kwa primary Dysmenorhoea maumivu huanza siku mtu unaanza hedhi na Secondary Dysmenorhoea mara nyingi maumivu huanza siku 2 au 3 kabla ya kuanza kutokwa damu ya hedhi
MATIBABU
Kwa primary Dysmenorhoea matibabu yanalenga kupunguza dalili za maumivu makali na kuweka sawa uwiano wa hormone ya progesterone na estrogen ili kuzuia lisitokee katika mizunguko inayofatia
Kupunguza maumivu dawa zinazaopunguza kutengenezwa kwa Kemikali ya prostaglandin hutumika hizi zinafanya kazi kwa kupunguza kuzalishwa kwa Prostaglandin
Kwa Secondary Dysmenorhoea matibabu yake ni kutibu chanzo cha tatizo, kama ni cyst,fibroid,PID nk unapotibu hivi vitu basi mtu anaacha kupata maumivu makali wakati wa hedhi.
Ni vyema mtu akafanya vipimo kama ultrasound na hysterosalpingography (HSG) ili kuina kama kuna tatizo kwenye mfumo wa uzazi ili litibiwe
Kwa primary Dysmenorhoea nimezungumza pia kuweka sawa uwiano wa progesterone na estrogen, hapa dawa zenye progesterone hutumika.

Endapo una tatizo hili fika hospitali upatiwe matibabu haya.
Unahitaji kujiunga na masomo kuhusu hormone bure bofya hapa ujiunge na darasa kwa njia ya whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/B9YE3TAEYld7UT3SZUzPQG

1 comment:

  1. Kwa mtu wa kawaida anapopata kiungulia either Kwa kula kitu fulan hii inatokana na nin!?

    ReplyDelete