KIUNGULIA WAKATI WA UJAUZITO

 


Hii ni hali inayowakumba mama wajawazito walio wengi. Inaweza kutokea kipindi chochote cha ujauzito ila mara nyingi hutokea katika umri wa mimba kuanzia miezi mitatu.

Katika makali hii nitaelezea nini kinasababisha hali hii.

KIUNGULIA NI NINI
Kiungulia ni maumivu mithili ya moto yanayotokea kifuani sehemu ya katikat ya kifua. Maumivu haya hayana uhusiano na moyo.Yanatikea pale asidi ya kwenye tumbo inapopanda na kurudi kwenye koo la chakula.
Asidi hii ikiwa tumboni haisababishi madhara wala maumivu kwani inazalishwa muda wote na kuta za tumbo kumeng'enya chakula. Seli za kuta za tumbo haziathiriki na asidi hii ndio maana inapokuwa tumboni haileti shida yoyote.ila seli za kuta za koo la chakula haziwez kustahimili asidi hii ndio maana inapopanda kwenye koo la chakula unapata maumivu ya kiungulia.

Jifunze zaidi kupitia video hii..


No comments